Asante sana Wahariri wa magazeti kwa kufanikiwa kumfanya mkuu aelewe

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,141
20,785
Toka jana wajuvi wa mambo wanasema lile tukio la kule gatini ilikua "TAKE ONE......... ACTION". Nia na madhumuni ya director ilikua ni kupata COVERAGE ya NGUVU Leo Asubuhi magazetini.

Lakini ni kama kama vile mmeambizana (sijui utaratibu Wenu wa Kazi ukoje) yaani asilimia ya Magazeti kubwa sana leo mmemzungumzia aliyekua Boss Wenu Mh. NM Nnauye, Inapendeza sana na Inafariji sana kuona sote kwa pamoja tunatambua nani anataka kuturudisha Misri.

Na kuonyesha kwamba Director Alikua kapanga huu mchezo, ona alivyolalama Leo kwa Front Page mlizotengeneza Leo. Ni kama Alikua akisema "yaani kweli mnaweza kupotezea habari yangu ya Maana sana na kumuweka mtu Ambaye hana manufaa yeyote kwa taifa?" Huu ni Mwanzo mzuri kwamba mshajua jinsi ya kumtaimu Director.

Tulipokubaliana kwamba Bashite hatopata Airtime ni kwamba tulilenga na wengine wote ambao wako Upande wake.

Laiti kama mimi ningekua Mhariri Wallah kwa issue ya jana hata habari yake ungeikuta katikati ya makala tena paragraph mbili tu.

Tuheshimiane.. Vyombo vya Habari ni Muhimiri Mwengine Muhimu sana katika ujenzi wa Taifa Lolote.

Nawatakia Kazi njema/ much love much respect.
Tatizo rais wetu hakutumia kauli nzuri pale ubungo. Rais anasema hapangiwi cha kufanya, ajabu yeye anataka kuwapangia wahariri cha kufanya wakati hajasomea uanahabari.

Sasa atambue hata akiwa na nia njema hawezi kujenga nchi peke yake. Anahitaji vyombo vya habari ili kufikisha maono yake ya maendeleo kwa wananchi wake.

Pia, sasa rais atambue kwamba kwa mamlaka aliyonayo hatakiwi kuonyesha upendo/upendeleo wa wazi kwa mtu au taasisi. Yeye anashangaa vyombo vyote vya habari kumpa coverage Nape na yule askari mhuni wakati yeye kazi yake ni kuisifia na kupiga simu Clouds. Je clouds ndiyo pekee wenye vipindi bora? Vipindi anavyovipenda vya Clouds ni vya maendeleo?

Mwisho, hata kama anaona MabashiteKolomije anafanya kazi nzuri, hapaswi kumsifia hadharani, tena mara kibao wakati kijana mwenyewe sio humble. Ni ajabu sana kwamba sifa anamwagiwa yeye tu na wala sio makamu wake au msaidizi wake mkuu(PM) katika shughuli za serikali. Tatizo la kupenda ni kwamba anapoumia mpendwa wako na wewe unaumia. Je yuko tayari kuendelea kupiga simu studio za Clouds? Yuko tayari kuendelea kumsifia koffi Olomide wakati ameshachafuka? Kama yupo tayari, basi asiwapangie wahariri/wamiliki wa vyombo vya habari kitu gani cha kufanya. Atambue hawezi kuwalazimisha wampambe.
Wanahabari Leo nimemsikia Mukulu akivilalamikia vyombo vya habari Kwa kutokuwekwa front page.

Lakini Mukulu unawalaumu wahariri bure kwani nakumbuka Prof Chachage kwenye sociology of knowledge alikuwa anasisitiza kuwa"Press Media belongs to the press owner" kwahiyo wahariri lazima wasikilize au waandike kufuata mlengo wa matajiri wao.

Mbona Habari Leo na TBC wamekuweka front page kabisa tena mubashara? Au ulitaka Mwananchi, Jambo Leo, Mwanahalisi, Majira,Mtanzania na mengine mengi wafanye Kama TBC au Daily News?

Basi nawashauri wahariri wote mtoeni Mkulu front page kila siku maana itamfurahisha sana! Chonde mtoeni kuanzia Kesho moyo wake ufurahi.
Pindi Gazeti la Uhuru linapoacha kuandika baadhi ya habari muhimu au pindi kituo cha Utangazaji cha TBC kinapoacha kuonyesha habari muhimu kuendana na wakati na mahitaji kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla kuna watu huona ni sawa kabisa na inapaswa kuwa hivyo. Lakini pindi vyombo vingine hususani vyombo binafsi vya habari vinapofanya kazi yake na ikatokea kutorusha au kuandika habari zao baadhi ya watu wanaumia mioyo na kuona vyombo hivyo havitendi haki au wajibu wake!

Sikuwahi kuwaza kwamba itatokea siku watu waumie mioyo, kupata ghadhabu na kutoa vitisho kwa vyombo vya habari eti kisa matukio yao hayajapewa kipaumbele, kurushwa au kuandikwa na vyombo hivyo vya habari!

Nadhani kabla wahusika hawajaghafilika na kuona vyombo husika haviwatendei haki ni vyema waathirika wakatumia busara kutafakari na kujiuliza kwanini vyombo hivyo visizipe kipaumbele habari zao na kuzipa kipaumbele habari nyingine. Pili wajiulize wengine huwa wanajisikiaje pindi wanapotenda mambo ya manufaa kwa taifa na bado baadhi ya vyombo vya habari tena vinavyojiendesha kwa kodi za wananchi vikaacha kuzipa kipaumbele, kuzitangaza au kutoziandika kabisa habari zao?!

Mwisho ni vyema wahusika wakatambua kwamba sio lazima vyombo vya habari kuandika au kurusha habari zao au za yeyote yule awaye ilimradi havikiuki sheria za huduma ya vyombo vya habari.

Nakaribisha maoni tofauti.
 
Toka jana wajuvi wa mambo wanasema lile tukio la kule gatini ilikua "TAKE ONE......... ACTION". Nia na madhumuni ya director ilikua ni kupata COVERAGE ya NGUVU Leo Asubuhi magazetini.

Lakini ni kama kama vile mmeambizana (sijui utaratibu Wenu wa Kazi ukoje) yaani asilimia ya Magazeti kubwa sana leo mmemzungumzia aliyekua Boss Wenu Mh. NM Nnauye, Inapendeza sana na Inafariji sana kuona sote kwa pamoja tunatambua nani anataka kuturudisha Misri.

Na kuonyesha kwamba Director Alikua kapanga huu mchezo, ona alivyolalama Leo kwa Front Page mlizotengeneza Leo. Ni kama Alikua akisema "yaani kweli mnaweza kupotezea habari yangu ya Maana sana na kumuweka mtu Ambaye hana manufaa yeyote kwa taifa?" Huu ni Mwanzo mzuri kwamba mshajua jinsi ya kumtaimu Director.

Tulipokubaliana kwamba Bashite hatopata Airtime ni kwamba tulilenga na wengine wote ambao wako Upande wake.

Laiti kama mimi ningekua Mhariri Wallah kwa issue ya jana hata habari yake ungeikuta katikati ya makala tena paragraph mbili tu.

Tuheshimiane.. Vyombo vya Habari ni Muhimiri Mwengine Muhimu sana katika ujenzi wa Taifa Lolote.

Nawatakia Kazi njema/ much love much respect.
Kwani huko vijijini wanasoma magazeti au wanasikiliza tbc taifa.

Hili ndo kosa la ukawa, wao wanendesha vita kwenye mitandao na mijini.
 
Leo waandishi wa habari wamenifurahisha sana.Mkulu anafikiri kukimbia kimbia bandarini kama askari au mkuu wa Takukuru ni habari ya maana.Watanzania wanataka uwajibikaji, ueledi, na utumishi uliotukuka.Itafike kipindi hata habari zake zisitangazwe kabisa hasa haya zile za kuharibu mafuta kwa ziara za kushtukiza.Amesema serikali ina pesa mbona miradi mingi inafadhiliwa na wahisani?Ukweli ni kwamba yeye na Bashite wameonyesha mapungufu makubwa kiuongozi.Bashite anaharibu jiji letu na Mkulu anaharibu nchi yetu.Kama anaukubali uwezo wa Daud ampeleke Geita akaijenge Chato
 
Kuanzia sasa marufuku kurusha muda mrefu habari za migogoro ya ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji. Fuatilia hotuba ya leo ya Mkulu
 
Toka jana wajuvi wa mambo wanasema lile tukio la kule gatini ilikua "TAKE ONE......... ACTION". Nia na madhumuni ya director ilikua ni kupata COVERAGE ya NGUVU Leo Asubuhi magazetini.

Lakini ni kama kama vile mmeambizana (sijui utaratibu Wenu wa Kazi ukoje) yaani asilimia ya Magazeti kubwa sana leo mmemzungumzia aliyekua Boss Wenu Mh. NM Nnauye, Inapendeza sana na Inafariji sana kuona sote kwa pamoja tunatambua nani anataka kuturudisha Misri.

Na kuonyesha kwamba Director Alikua kapanga huu mchezo, ona alivyolalama Leo kwa Front Page mlizotengeneza Leo. Ni kama Alikua akisema "yaani kweli mnaweza kupotezea habari yangu ya Maana sana na kumuweka mtu Ambaye hana manufaa yeyote kwa taifa?" Huu ni Mwanzo mzuri kwamba mshajua jinsi ya kumtaimu Director.

Tulipokubaliana kwamba Bashite hatopata Airtime ni kwamba tulilenga na wengine wote ambao wako Upande wake.

Laiti kama mimi ningekua Mhariri Wallah kwa issue ya jana hata habari yake ungeikuta katikati ya makala tena paragraph mbili tu.

Tuheshimiane.. Vyombo vya Habari ni Muhimiri Mwengine Muhimu sana katika ujenzi wa Taifa Lolote.

Nawatakia Kazi njema/ much love much respect.
Mkulu analilia kuandikwa vizuri. Hehehehehe
 
Kwani huko vijijini wanasoma magazeti au wanasikiliza tbc taifa.

Hili ndo kosa la ukawa, wao wanendesha vita kwenye mitandao na mijini.
Wewe umewahi kutembelea vijiji gani?

Solar za mchina, viredio vya mchina, vitochi vya mchina na simu za mchina.

Wewe endelea kujitia dole halafu nusa kama unadhani vijijini hawaendi na wakati, kwa taarifa yako wanazo mpaka wasapu group zao.

Wewe kaa Lumumba hapo kupimkia chai Polepole utakuwa shuhuda wa kifuatacho.
 
Ya
Leo waandishi wa habari wamenifurahisha sana.Mkulu anafikiri kukimbia kimbia bandarini kama askari au mkuu wa Takukuru ni habari ya maana.Watanzania wanataka uwajibikaji, ueledi, na utumishi uliotukuka.Itafike kipindi hata habari zake zisitangazwe kabisa hasa haya zile za kuharibu mafuta kwa ziara za kushtukiza.Amesema serikali ina pesa mbona miradi mingi inafadhiliwa na wahisani?Ukweli ni kwamba yeye na Bashite wameonyesha mapungufu makubwa kiuongozi.Bashite anaharibu jiji letu na Mkulu anaharibu nchi yetu.Kama anaukubali uwezo wa Daud ampeleke Geita akaijenge Chato
Ni Lazima ajua Diplomacy sio Science... Democracy sio Pythagoras.
 
Back
Top Bottom