Asante sana Sadifa Juma Khamis, umelibeba vyema bango la UVCCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,071
2,000
Kukamatwa na kushtakiwa kwako kwa rushwa si jambo la kushangaza. Umeonesha picha halisi ya rushwa ilivyo ndani ya CCM yetu hasa kipindi cha uchaguzi. Umeonesha kwa umahiri mkubwa jinsi rushwa inavyolelewa na kukua ndani ya CCM huku 'tukiigiza' kupambana nayo. Asante sana Sadifa!

Sadifa nakumwagia sifa. Umejiweka wazi kuwa hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Uenyekiti wa Rais Magufuli ni mtu wa rushwa. Umeuonesha umma na ulimwengu kwa ujumla kuwa bila rushwa, uchaguzi ndani na nje ya CCM haunogi. Ubarikiwe sana Sadifa!

Najua kuwa ulikuwa unamuunga mkono Mwenyekiti mpya wa UVCCM Kijana Kheri James. Najua ulikuwa ukihusishwa naye tangu mwanzo. Mrithi wako atafanya jambo kichama ili uweze kusaidiwa. Sadifa, una kila sifa za kuwa ndani ya CCM na ndani ya Kamati Kuu ya chama chetu. Kudos!

Sadifa, CCM ndiyo hiyo uliyoianika Dodoma. Tutaendelea kusema kuwa tunapambana na rushwa na huku tukiiachaacha itusaidie nyakati muhimu hasa uchaguzini. Penye udhia, penyeza rupia.

Mambo ya extension joints hayo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
 
swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,660
2,000
IMG-20171206-WA0282.jpg

Swissme
 
Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,595
2,000
Kukamatwa na kushtakiwa kwako kwa rushwa si jambo la kushangaza. Umeonesha picha halisi ya rushwa ilivyo ndani ya CCM yetu hasa kipindi cha uchaguzi. Umeonesha kwa umahiri mkubwa jinsi rushwa inavyolelewa na kukua ndani ya CCM huku 'tukiigiza' kupambana nayo. Asante sana Sadifa!

Sadifa nakumwagia sifa. Umejiweka wazi kuwa hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Uenyekiti wa Rais Magufuli ni mtu wa rushwa. Umeuonesha umma na ulimwengu kwa ujumla kuwa bila rushwa, uchaguzi ndani na nje ya CCM haunogi. Ubarikiwe sana Sadifa!

Najua kuwa ulikuwa unamuunga mkono Mwenyekiti mpya wa UVCCM Kijana Kheri James. Najua ulikuwa ukihusishwa naye tangu mwanzo. Mrithi wako atafanya jambo kichama ili uweze kusaidiwa. Sadifa, una kila sifa za kuwa ndani ya CCM na ndani ya Kamati Kuu ya chama chetu. Kudos!

Sadifa, CCM ndiyo hiyo uliyoianika Dodoma. Tutaendelea kusema kuwa tunapambana na rushwa na huku tukiiachaacha itusaidie nyakati muhimu hasa uchaguzini. Penye udhia, penyeza rupia.

Mambo ya extension joints hayo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
Si nasikia anampelekea moto kijana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom