Asante Rais Samia Suluhu kwa kuwakumbuka vijana lakini baadhi ya wazee uliowaacha ni wachapa kazi na waadilifu sana. Naomba usiwasahau

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Mhe. Rais, nakushukuru na kukupongeza kwa kutekeleza ahadi uliyotoa ukiwa ziarani mkoani Mwanza juu ya kuteua vijana tu kwenye nafasi ya U-Dc.

Mhe. Rais kwa hakika umedhamiria kwa dhati ya moyo wako kuleta mabadiliko makubwa kupitia vijana. Naamini vijana ni jeshi muhimu La mabadiliko kwenye nchi yoyote hivyo uwezo na ujuzi wao unatakiwa kutumika ipasavyo kama ambavyo umefanya.

Lakini Mhe. Rais, nafasi za wazee na watu wazima bado ni muhimu sana, bado tunahitaji ushauri wao na uzoefu wao katika ujenzi wa taiga letu. Naamini kuna baadhi ya wazee wameachwa ili vijana wawepo, wazee hao bado hawakutimiza umri wa kustaafu. Bado wanahitajika kwenye uongozi na utawala wako, nakuomba Mhe. Rais uwakumbuke waweze kulisaidia taifa hili.
 
Mama anatenda haki sana hata Wamangi nao kwenye teuzi zake wamekuwepo hakika mama anajenga taifa la Watanzania na si kundi la wachache kama ilivyokuwa hapo awali .Awamu zote 1-4 na hii ya sita walau zinazingatia jiografia ya nchi yetu .
 
Wamangi ni kina Nani hao,na kwa nini waliachwa?
 
Back
Top Bottom