Asante Rais Samia na Mzee Warioba kwa kuukemea ukabila na ukanda

haha

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,101
2,000
Nimefurahishwa sana na viongozi hawa kujitokeza na kuwa wawazi kwa yale yaliyojiri katika awamu ya iliyopita

Ni ukweli japo mchungu kwa baadhi yetu

Sisi kama Taifa kuna mahali tulikua tunaelekea kupoteza dira na umoja wetu

Ukabila na ukanda zikawa ndio qualities (sifa) za MTU kuwa viongozi

Watu kutoka kanda Fulani walijaza idara mbali mbali za umma kama ukuu wa idara,ukuu wa wilaya ,ukuu wa mikoa,nk bila hata kujali taaluma zao!! Ilifikia mahali hata MTU aliyefoji vyeti (ambalo ni kosa) alifumbiwa macho mradi katoka maeneo Fulani walijaa viburi, matusi, kebehi kisha wakaota pembe.

Kufumba na kufumbua ikaja awamu nyingine. Wakikosea wanaadhibiwa wanalalama kuonewa kwakuwa wanatoka ukanda Fulani!

Rais Samia endelea kufanya haki taifa liinuke
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom