Asante Rais Magufuli kwa kuwakumbuka Vijana waliokupaigania wakati wa Kampeni Uchaguzi Mkuu...

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,816
Baada ya Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na baadhi ya mikoa kufanyika,kulikuwa na "minong'ono" mimgi kwenye korido za Lumumba na Makao Makuu,kuwa vijana wengi waliopigania chama kuanzia mitandaoni mpaka "field" wametupwa kapuni,hali iliyozua sintofahamu na kushusha morali.

Vijana hawa walipigana kufa na kupona kuhakikisha chama kinarudi madarakani licha ya kuwepo upinzani mkali sana uliotishia "uhai" wa chama,upinzani wa nje na ndani ya chama ulitikisa kweli kweli harakati za kuingia Ikulu kwa mara ya Tano.Juhudi za vijana hawa wakiwa field na mitandaoni zilichangia kwa kiasi ushindi wa CCM.Licha ya matusi na kejeli mitaani na mitandaoni vijana hawakukata tamaa.

Hatimaye uteuzi wa makatibu Tawala wa Wilaya nchini umekumbuka kundi kubwa la vijana waliokuwa mstari wa mbele field na mitandaoni kukipaigania chama.Hongera sana kwa vijana wenzangu ambao mmepikwa na mmeiva kulitumikia Taifa. Nyinyi ni zao la Uvccm na Shirikisho la Vyuo Vikuu. Nendeni mkapige kazi kwa uadilifu mkawatumikie watanzania vyema. Hakika tumefurahi sana. Tunawatakia kila la Kheri katika majukumu yenu mapya.

* Joseph Chitinka Meshack
* Kheri James
* Asenga Abubakar
* Husna Sekiboko
* David John Mwakiposaa
* Edward Jonas Mpogoro
* Mtela Mwampamba
* Hashimu Komba
* Gift Isaya Msuya
* Jasinta Venant Mboneko
* Ally Nyakia Chilukile
* Faiza Suleiman Salim
* Adam H. Mzee
*Lameck Lusesa

Mwisho.Tunapongeza sana mamlaka za uteuzi kwa kuweka imani hii kubwa kwa vijana. Ahsante Dr.Magufuli kwa kutuamini vijana.
 
Hatimaye Lumumba buku 7 wameonekana kwa mbaaaali.
Hope Lizaboni hajaachwa
 
Bado
Wema Sepetu
Mwana FA
Wastara
Shishi Baby
Hadija Kopa
Chibu Dangote
. Wangefikiriwa kupewa Utendaji kata Bwana Mkubwa atakapoanza kuteua, maana mwaka mzima huu ni wa kutumbua na kuteua,kutengua na kuteua,kustaafisha na kuteua
Huku bei ya sukari sehemu nyingine ni shs 4000-
 
Hii kali sana, hao jamaa wataajiriwa na kupandishwa cheo hapo hapo bila kujali taratibu za utumishi wa umma zikoje. Mnaangalia kadi ya kijani.

Halafu tunadanganyana kuwa Tanzania ya viwanda inakuja, utajenga viwanda gani kama hauthamini ubobezi na weledi. Umaskini tulionao Afrika sio laana bali ni wa kujitakia kwa vile aina ya watu wanaotuongoza ni wa hovyohovyo na kubahatisha
 
Vipi Ray kigosi, Diamond ,Steve nyerere, Dr.slaa, prof. Lipumba,Augustine Mrema n.k. hata utendaji wa mitaa?
 
Hii kali sana, hao jamaa wataajiriwa na kupandishwa cheo hapo hapo bila kujali taratibu za utumishi wa umma zikoje. Mnaangalia kadi ya kijani.

Halafu tunadanganyana kuwa Tanzania ya viwanda inakuja, utajenga viwanda gani kama hauthamini ubobezi na weledi. Umaskini tulionao Afrika sio laana bali ni wa kujitakia kwa vile aina ya watu wanaotuongoza ni wa hovyohovyo na kubahatisha
Kwakweli hili jambo limenisikitisha sahv nafanya yangu tu simuamini mtu wala serikali sijawahi ona kitendo hiki popote pale haya ni matusi kwa wafanyakazi
 
lizabon hongera sana nakuona hapo. japo kwa jina jingine
 
Hakuna Morali hapo. Faiza aliutaka Ukuu wa Wilaya kwa nguvu zote,unakuja kumpa Katibu Tawala?

Anyway,hongereni. Mkapige kazi na muwe busy. Hatutaki tena kelele zisizo na maana. Mlizidisha uongo na uzadikina ili angalau mpate fursa. Sasa mmepata. Hatutegemei tena thread zenu zisizo na kichwa wala kiwiliwili.......
 
Nashangaa mm mpaka Leo hawajanipa cheo chochote wakati mm nipo chichiem mpaka Leo lakini huyo aliyetoka Chadem na kuhamia CCM hana hata miaka 9,ss wengine toka 2004 tunaipigia debe Chichiem kimya kimya
 
Baada ya Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na baadhi ya mikoa kufanyika,kulikuwa na "minong'ono" mimgi kwenye korido za Lumumba na Makao Makuu,kuwa vijana wengi waliopigania chama kuanzia mitandaoni mpaka "field" wametupwa kapuni,hali iliyozua sintofahamu na kushusha morali.

Vijana hawa walipigana kufa na kupona kuhakikisha chama kinarudi madarakani licha ya kuwepo upinzani mkali sana uliotishia "uhai" wa chama,upinzani wa nje na ndani ya chama ulitikisa kweli kweli harakati za kuingia Ikulu kwa mara ya Tano.Juhudi za vijana hawa wakiwa field na mitandaoni zilichangia kwa kiasi ushindi wa CCM.Licha ya matusi na kejeli mitaani na mitandaoni vijana hawakukata tamaa.

Hatimaye uteuzi wa makatibu Tawala wa Wilaya nchini umekumbuka kundi kubwa la vijana waliokuwa mstari wa mbele field na mitandaoni kukipaigania chama.Hongera sana kwa vijana wenzangu ambao mmepikwa na mmeiva kulitumikia Taifa. Nyinyi ni zao la Uvccm na Shirikisho la Vyuo Vikuu. Nendeni mkapige kazi kwa uadilifu mkawatumikie watanzania vyema. Hakika tumefurahi sana. Tunawatakia kila la Kheri katika majukumu yenu mapya.

* Joseph Chitinka Meshack
* Kheri James
* Asenga Abubakar
* Husna Sekiboko
* David John Mwakiposaa
* Edward Jonas Mpogoro
* Mtela Mwampamba
* Hashimu Komba
* Gift Isaya Msuya
* Jasinta Venant Mboneko
* Ally Nyakia Chilukile
* Faiza Suleiman Salim
* Adam H. Mzee
*Lameck Lusesa

Mwisho.Tunapongeza sana mamlaka za uteuzi kwa kuweka imani hii kubwa kwa vijana. Ahsante Dr.Magufuli kwa kutuamini vijana.

Tulidhani tumepata Raid ambaye anamacho ya kuuna mzaha kwa sura take. Niliamini Nonsense sasa imekosa nafasi.
Utumishi wa umma mnapeana zawadi tena waziwazi.
'Darwin's nightmare'

Kweli Umasikini Huanzia kichwani sio mikononi.
Alivyoanza Magufuli Hapafanani na uteuzi huu wa Wampum I za Vuvuzera.
Rais ameishiwa pumzi amerudi kuwasikiliza walewale.

Eti yanapongezana, aibu ya mama Afrika.
Tulihitaji kuliepuka taifa LA uchaguzi. Tufuate new destination. Taifa LA maendeleo.

Kwa mtindo huu kumbe Magufuri hana anachokiamini Tutasubili sana.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom