Asante Rais Magufuli kupambana na mafisadi TANESCO, sasa umeme sio kero tena na haukatiki muda mrefu

Sijawahi kuvutiwa na vyama vyenye siasa za kijamaa. Mimi sio muumini wa siasa za kikondoo na kinafiki. Na wala sintokaa nivutiwe na chama chochote cha kijamaa kutokana na siasa zao za shuruti bila hoja.
Tanzania Sio nchi ya kijamaa ila mafisadi cha mtema kuni wanakiona
 
Sijawahi kuvutiwa na vyama vyenye siasa za kijamaa. Mimi sio muumini wa siasa za kikondoo na kinafiki. Na wala sintokaa nivutiwe na chama chochote cha kijamaa kutokana na siasa zao za shuruti bila hoja.
Huwenda ikawa ni dhana tu ya ujamaa lakini kwenye utendaji isiwe hivyo.kama alivyo Zito,ni mjamaa lakini matendo yake ni ya kibepari.
Njoo nyumbani ujiunge huwenda tukaonganisha fikra tukabadiri sera ya kijamaa ndani ya CCM.
 
Wewe kama haujui kitu kaa kimyia, zamani tulikuwa tunalipishwa service charge umetumia au haujatumia mwisho wa mwezi lazima kulipa, imeondoka wakati wa Magufuli, wewe unaongea eti wamepandisha kiasi kutoka sh 10 hadi 20 kweli wanadamu hawana shukurani mateso mengi sana tuliyoyapata kutoka 2000 hata 2015 kuhusu umeme sio ya kusimulia. Mungu ambariki Rais Magufuri.
Ndio maana nasisitiza kusema kama akili yako ya kawaida unaweza ukawa unasifia vitu NON-SENSE ,Sasa wewe ulikuwa unaona kawaida kukatwa Services Charges? Ule ulikuwa ni wizi na tuliupigia kelele tangia 2004,sasa unafuta Service charges halafu unaweka Tozo kununua umeme wakati tayari kuna VAT ishakatwa huo ni wizi pia na tutaupigia kelele uondoke.
 
Huwenda ikawa ni dhana tu ya ujamaa lakini kwenye utendaji isiwe hivyo.kama alivyo Zito,ni mjamaa lakini matendo yake ni ya kibepari.
Njoo nyumbani ujiunge huwenda tukaonganisha fikra tukabadiri sera ya kijamaa ndani ya CCM.

Sio wajamaa parsee bali ni wajamaa uchwara ndio maana mnajichanganya. Sisi tunaoamini kwenye nguvu ya soko, huwezi kutuona tukiwa wanafiki wala kujipendekeza kwa yoyote. Huwezi kuniona nikatamani hata kujiunga na wajamaa uchwara, maana mtaishia kuniharibia pozi tu.
 
Duh,,,ndo umetoa shit hivi mkuu!!!.
Haya bwana lakini ipo siku utakuja tu
 
Serikali yako unayosema imeondoa ufisadi imeongeza tena tozo ya kununua umeme kutoka 1% hadi 2% yaani mara mbili ya bei ya mwanzo,zamani ukinunua umeme wa buku unakata Tsh 10 ila leo unakatwa Tsh 20,huo ndio upigaji tunaousema,mkuu nasisitiza akili hii ya maono tumepewa watu wachache sana! Mtu mwenye akili/uelewa ya/wa kawaida hawezi kujua kiundani.
Anae chukua hiyo 2% ni kampuni ya Simu na si vinginevyo. Tumia akili kidogo. Nenda kwa wakala wa LUKU na nunua umeme wa 10,000 then uone kama utaombwa Sh. 200 nyingine.
 
Mimi simkubali Magufuli kwa mambo mengi sana, lakini kwa hili la umeme kapatia. Lakini hawezi kupata kura yangu maana hafai kuwa rais, kwani ana mapungufu mengi.

Huo ni mtazamo wako na hauwezi kupingwa lakini kwa wengine ni Rais bora na wanalilia aongezewe muda kuongoza kuwa Rais wao
 
Tanesco iligeuzwa chombo cha kisiasa ambacho mafisadi waliitumia Tanesco kuifanya serikali ya CCM ichukiwe na wananchi ili upinzani ushinde

2015 karibu na uchaguzi mkuu nilikuwa Arusha mjini umeme ulikuwa unazimwa siku nzima unawashwa saa saba usiku na kuzimwa saa tisa usiku. watu vyakula viliwaozea kila ukipita kila kona CCM ilikuwa ikiporomoshewa matusi ya nguoni kumbe mifisadi ikishirikiana na mifisadi mifanyakazi us Tanesco iliamua kutumia Tanesco kama chombo chao cha kuipiga chini CCM

Na hili lilifanyika sana mikoa ya kaskazini na majiji ya Mbeya, Dar, Arusha na Mwanza na sehemu mbalimbali za miji kama Iringa nk Hali iliyosababisha maeneo hayo kuchukuliwa na upinzani kirahisi tu kwa kutumia kero ya Tanesco tu

Baada ya Raisi Magufuli na kutumbua mafisadi Tanesco na kuibana mifisadi ya umeme sasa hivi hali shwari tuna enjoy umeme wananchi kero imeisha. nyumba hata za vijijini za majani zina umeme wa Rea na haukatiki hovyo

Mtu akibeza mafanikio ya Magufuli muulize tu vipi umeme ukilinganisha na kabla 2015 Magufuli kuingia madarakani hali unaionaje? Raisi Magufuli asante kutuondolea kero ya umeme kuanzia ugumu wa kuupata, kukatika vipindi virefu, nk

Ilikuwa 2015 kurudi Numa kabla Rais Magufuli hajashika urais wafanyakazi wa Tanesco wakionekana mtaani na magari yao watu walikuwa watu mtaani walikuwa wakiwazomea na kuwaombea dua mbaya na wengine kuwarushia mawe kuwa wamekuja mtaani kukata umeme!!!

Watanzania waliehuka umeme kuwaka ilikuwa sherehe kubwa ya kushangilia kuliko ushindi wa simba na yanga umeme uliokatika unaporudi!!! Yaani ukirudi watu wanashangilia kama wehu ngoma za madebe zinapigwa mitaani kwenye mabaa watu wanaruka ruka juu kama ngoma ya masai kufurahia umeme adimu uliorudi!!

Toka mheshimiwa Magufuli ashike madaraka sherehe Hiro zimekufa. Umeme raha mstarehe. aAsante Raisi Magufuli kwa kutatua kero hii kubwa iliyokuwa inagusa watu wote wa juu hadi wa chini kabisa nchi nzima.Anayebisha mafanikio ya Raisi Magufuli aangalie kipengele cha umeme pekee nchi nzima na alinganishe na kabla hajaingia madarakani 2015
Kwa hili mh.rais kafanya vizuri sana kongole kwake,ujenzi wa hospital,zahanati na miundombinu ya usafiri katekeleza kwa ufanisi sana
 
Tanesco iligeuzwa chombo cha kisiasa ambacho mafisadi waliitumia Tanesco kuifanya serikali ya CCM ichukiwe na wananchi ili upinzani ushinde

2015 karibu na uchaguzi mkuu nilikuwa Arusha mjini umeme ulikuwa unazimwa siku nzima unawashwa saa saba usiku na kuzimwa saa tisa usiku. watu vyakula viliwaozea kila ukipita kila kona CCM ilikuwa ikiporomoshewa matusi ya nguoni kumbe mifisadi ikishirikiana na mifisadi mifanyakazi us Tanesco iliamua kutumia Tanesco kama chombo chao cha kuipiga chini CCM

Na hili lilifanyika sana mikoa ya kaskazini na majiji ya Mbeya, Dar, Arusha na Mwanza na sehemu mbalimbali za miji kama Iringa nk Hali iliyosababisha maeneo hayo kuchukuliwa na upinzani kirahisi tu kwa kutumia kero ya Tanesco tu

Baada ya Raisi Magufuli na kutumbua mafisadi Tanesco na kuibana mifisadi ya umeme sasa hivi hali shwari tuna enjoy umeme wananchi kero imeisha. nyumba hata za vijijini za majani zina umeme wa Rea na haukatiki hovyo

Mtu akibeza mafanikio ya Magufuli muulize tu vipi umeme ukilinganisha na kabla 2015 Magufuli kuingia madarakani hali unaionaje? Raisi Magufuli asante kutuondolea kero ya umeme kuanzia ugumu wa kuupata, kukatika vipindi virefu, nk

Ilikuwa 2015 kurudi Numa kabla Rais Magufuli hajashika urais wafanyakazi wa Tanesco wakionekana mtaani na magari yao watu walikuwa watu mtaani walikuwa wakiwazomea na kuwaombea dua mbaya na wengine kuwarushia mawe kuwa ni geita mtaani kukata umeme!!!

Watanzania waliehuka umeme kuwaka ilikuwa sherehe kubwa ya kushangilia kuliko ushindi wa simba na yanga umeme uliokatika unaporudi!!! Yaani ukirudi watu wanashangilia kama wehu ngoma za madebe zinapigwa mitaani kwenye mabaa watu wanaruka ruka juu kama ngoma ya masai kufurahia umeme adimu uliorudi!!

Toka mheshimiwa Magufuli ashike madaraka sherehe Hiro zimekufa. Umeme raha mstarehe. aAsante Raisi Magufuli kwa kutatua kero hii kubwa iliyokuwa inagusa watu wote wa juu hadi wa chini kabisa nchi nzima.Anayebisha mafanikio ya Raisi Magufuli aangalie kipengele cha umeme pekee nchi nzima na alinganishe na kabla hajaingia madarakani 2015
Hapa eneo la mkoani geita hatuna umeme toka saa tano asubuhi leo tarehe 19/06/2020
 
Ukweli ni kuwa tatizo la umeme lilitengenezwa. Mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa yakifunguliwa na kuruhusu maji yatoke. Ndio maana kila siku tulisikia tatizo la kina cha maji kupungua. Lengo kuu ilikuwa ni kutengeneza mgao wa umeme ili watuuzie umeme wao. Na kwa hili walifanikiwa. Mafisadi waliweza kuvuna mabilioni kutokana na kuiuzia umeme Tanesco. Lakini mheshimiwa Magufuli alilijua hili na akatoa angalizo wakati wa kampeni zake. Toka ameanza kazi ya urais hatujashuhudia mgao wa umeme. Hongera kwake kwa kutatua tatizo la umeme. Hongera nyingine za ziada kwa kumaliza tatizo la ujambazi. Hakika anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano..
 
Huo ni mtazamo wako na hauwezi kupingwa lakini kwa wengine ni Rais bora na wanalilia aongezewe muda kuongoza kuwa Rais wao

Hata akina Elbashir, Mugabe nk walikaa madarakani muda mrefu, huku wapambe wao wakisema wao ni bonge ya marais, wakawa wanachezea chaguzi za nchi zao ili kukaa madarakani kama afanyacho Magufuli na ccm hivi sasa. Lakini siku wananchi walipochoka na kutawaliwa kwa mabavu waliingia mtaani.
 
Ukweli ni kuwa tatizo la umeme lilitengenezwa. Mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa yakifunguliwa na kuruhusu maji yatoke. Ndio maana kila siku tulisikia tatizo la kina cha maji kupungua. Lengo kuu ilikuwa ni kutengeneza mgao wa umeme ili watuuzie umeme wao. Na kwa hili walifanikiwa. Mafisadi waliweza kuvuna mabilioni kutokana na kuiuzia umeme Tanesco. Lakini mheshimiwa Magufuli alilijua hili na akatoa angalizo wakati wa kampeni zake. Toka ameanza kazi ya urais hatujashuhudia mgao wa umeme. Hongera kwake kwa kutatua tatizo la umeme. Hongera nyingine za ziada kwa kumaliza tatizo la ujambazi. Hakika anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano..
Ni kweli kabisa anastahili kuongezewa awamu nyingine
 
Anae chukua hiyo 2% ni kampuni ya Simu na si vinginevyo. Tumia akili kidogo. Nenda kwa wakala wa LUKU na nunua umeme wa 10,000 then uone kama utaombwa Sh. 200 nyingine.
Achukue tigo au serikali mie alinihusu kwanini wakate fedha ya zangu ya ziada kununua umeme? Awali ukiweka buku unanunua wa Buku safi tu......Hata akichukua tigo then wakikusanya Serikali inakuja kuwakata Kodi kama mapato yao!! Huu ni Wizi serikali inakimbia majukumu ya kutoa huduma!! Mwanzo walikuwa wanawalipaje hayo makampuni?
 
Hii nchi ni kubwa sana ili uijue vizuri huna budi kutembelea maeneo mbalimbali, Umeme bado ni tatizo sana, sana sana...Vijiji vingi vipitiwa na mradi wa REA lakini raia hawana Umeme,mambo ambayo serikali inapaswa kushughulika nayo kwa sasa ni pamoja na REA kwani Umeme wanaweza sehemu nyeti tu kama shule na zahanati na wananchi wengi wanabaki bila Umeme. Ningepata nafasi ya kumshauri Rais basi ningemshauri aunde tume huru izunguke nchi nzima, ifanye tathmini hali ya Umeme wa REA kwa wananchi, naamin majibu yakitoka huko yanaweza kumliza mh Rais, maana watu wanahitaji Umeme ila ndo hivo hawapati
 
Lowasa alikuwa na mtandao wa kuhujumu kikwete viongozi wengi serikalini aliwaweka yeye akiwa Waziri mkuu walipogeukana na Kikwete akamtoa uwaziri mkuu akamuweka Mizengo pinda akaanza hujuma kikwete aonekane dhaifu utendaji baadaye akajiunga chadema kisirisiri akijua hawaivi na Kikwete Hivyo akipigwa chini aende chadema!!! Alivyoenda chadema mtandao wote alioiweka serikalini na mashirika ya umma wakawa naye wakiwemo wa Tanesco kuhakikisha kila mtu kwenye nafasi yake anahujumu ili Serikali ya,CCM ionekane boya!! Tanesco Ni moja ya mashirika yaliyofanikisha chadema kupata wabunge!! Kwa kuzalisha kero nyingi za umeme kwa wapiga kura zilizofanya watu wachukie CCM Hadi Basi.Hicho ndicho kilifanya Hadi akina God bless lema wakashinda Arusha!!!

Ndio maana Raisi Magufuli aliposhika tu katika maeneo alianza kutumbua ni Tanesco
Aiseee!!!!!
 
Ukweli ni kuwa tatizo la umeme lilitengenezwa. Mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa yakifunguliwa na kuruhusu maji yatoke. Ndio maana kila siku tulisikia tatizo la kina cha maji kupungua. Lengo kuu ilikuwa ni kutengeneza mgao wa umeme ili watuuzie umeme wao. Na kwa hili walifanikiwa. Mafisadi waliweza kuvuna mabilioni kutokana na kuiuzia umeme Tanesco. Lakini mheshimiwa Magufuli alilijua hili na akatoa angalizo wakati wa kampeni zake. Toka ameanza kazi ya urais hatujashuhudia mgao wa umeme. Hongera kwake kwa kutatua tatizo la umeme. Hongera nyingine za ziada kwa kumaliza tatizo la ujambazi. Hakika anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano..
Aiseee
 
Back
Top Bottom