Asante Nyerere, Hakika sisi ni Taifa Moja

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,883
5,186
Salaam WanaJF!

Baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kazi kubwa aliyoifanya katika utawala wake ni kujenga Taifa. Bara la Afrika mataifa yako machache sana, wengi wao ni nchi tu yaani kusanyiko la watu walio ndani ya mpaka mmoja, lakini ndani ya mipaka hiyo kila watu wana lugha zao, desturi zao, mambo yao, maono yao, changamoto zao, matarajio yao, fursa zao. Sisi kwetu ni watu tulio ndani ya mipaka ambapo tuna lugha moja, maono ya aina moja, matarajio ya aina moja na fursa za pamoja. Bila kujali dini zetu, rangi zetu, nasaba zetu, koo zetu, au mikoa yetu. Kinachotokea Mtwara leo, kinafanana na kinachowagusa watu wa bukoba kwenye sera za serikali. Tuko na taifa moja, lenye fursa sawa bila kujali unatoka wapi au jinsi yako ni ipi.

Nimekutana na picha hii mtandaoni ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi wa Jumuiya ya Kikristo. Rais Samia ni Muislam, ni Mzanzibar na ni mwanamke. Jumuiya hiyo ni ya Kikristo. Ni jambo la nadra sana. Haitokei hata nchi zilizoendelea ambao kila siku wanajifanga kutuhubiria Demokrasia na usawa wa binadamu. Kule Marekani imewachukua miaka zaidi ya 200 kuwa na VP mwanamke. Kule Uingereza ni ngumu sana kuwa mkatoliki na ukawa kwenye UPM. Mimi binafsi kama feminist, kuona Tanzania tumefikia hatua hii kwenye picha hii, ni faraja kubwa. Picha hizi zinaeleza na kusema mengi.

20210627_131624.jpg
20210627_131651.jpg
20210627_130633.jpg
 
Nimekutana na picha hii mtandaoni ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi wa Jumuiya ya Kikristo. Rais Samia ni Muislam, ni Mzanzibar na ni mwanamke.

Mkuu, kumbuka kuwa waislamu safi huwa hawana hiyana na wakristo, kadhalika wakristo safi hawana hiyana na waislamu, makundi haya mawili huonekana ni maadui kwasababu ya watu wachache walioshindwa kuelewa misingi ya dini hizo mbili, natambua moja ya misingi mikuu ni upendo, kwa taarifa yako Mkuu Rais Ally Hassan Mwinyi amekuwa mlezi wa chombo fulani cha kikristo, kama sijakosea ni CSSC kwa miaka mingi tu, hata huyu Mama ni mwenye hofu ya Mungu.

Jumuiya hiyo ni ya Kikristo. Ni jambo la nadra sana. Haitokei hata nchi zilizoendelea ambao kila siku wanajifanga kutuhubiria Demokrasia na usawa wa binadamu.

Kuna kiongozi mmoja tu hapa katikati alitaka kutuharibia uhusiano uliopo kati ya waislamu na wakristo, sidhani hata kama alikuwa na hofu ya Mungu, kumbuka vizuri utatuambia Mkuu, nyumba za ibada zilianza kuunguzwa, mashekh waliwekwa ndani, waandishi wa habari walilipuliwa na mabomu mpaka miili kusambaratika hadharani, wengine walitekwa na kung'olewa kucha, macho na meno, hakuna dini inayofundisha haya yote.
 
Mkuu, kumbuka kuwa waislamu safi huwa hawana hiyana na wakristo, kadhalika wakristo safi hawana hiyana na waislamu, makundi haya mawili huonekana ni maadui kwasababu ya watu wachache walioshindwa kuelewa misingi ya dini hizo mbili, natambua moja ya misingi mikuu ni upendo, kwa taarifa yako Mkuu Rais Ally Hassan Mwinyi amekuwa mlezi wa chombo fulani cha kikristo, kama sijakosea ni CSSC kwa miaka mingi tu, hata huyu Mama ni mwenye hofu ya Mungu.



Kuna kiongozi mmoja tu hapa katikati alitaka kutuharibia uhusiano uliopo kati ya waislamu na wakristo, kumbuka vizuri utatuambia Mkuu
Inatia matumaini sana kuona tuko watanzania wenye mtazamo huu wa umoja wa kitanzania.
 
Alienda kuwa aminisha kuwa corona tz ipo,pia ni harakati za kuomba ushawishi kuhusu mpango wa kipuuzi kuwachanja watz wote.
 
Back
Top Bottom