Asante Mwigulu kwa kutoa funzo la kuwa na moyo wa kusaidia

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Ni Upendo Imani na Miujiza tu kuwapata watu wenye roho ya kujitolea ya kuwasaidia wengine. Wakati Msanii wa miondoko ya HIPHOP Chidbenz akihojiwa radio Wasafi FM kipindi cha malavidavi alipata nafasi ya kueleza namna Dr Mwigulu alimtafuta kwa udi na uvumba kumsaidia pale alipopata janga la kuwa muhanga wa madawa ya kulevya.

Watu wengi baada ya kupotea na kupata majanga kinachowatokea kwao ni kukimbiwa na watu wao wa karibu pamoja na wanaowajua kwa kuamini wameishapotea. Ila Mwigulu anaonyesha utofauti wa kuguswa na tatizo la Chidbenz na kuamua kumtafuta kwa nguvu zote kumsaidia na kuhakikisha anarudi katika hali yake ya kawaida.

Kuguswa kwa mtu mmoja kunaweza kupelekea kurudisha furaha ya watu wengi. Chidbenz ni mwanamuziki ambaye alipotea kisanaa kwa muda mrefu baada ya kuingia kwenye dimbwi la Madawa ya kulevya lakini tatizo lake linaisha na kuendeleza kipaji chake cha muziki. Jana ilikuwa ni furaha ya watu wengi kuona msanii wao anarudi katika ubora wake baada ya kuzindua album yake mpya baada ya kupona kutoka kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Licha ya Mwigulu kuwa kiongozi mkubwa lakini alichukulia tatizo la Chidbenz kama la kwake na kuguswa nalo. Hii inatufundisha kwamba uongozi au madaraka uliyonayo unaweza kutumia kurudisha furaha za watu zilizopotea na kuwapa tumaini jipya la maisha yao. Wenye hekima zao walitutangulia kwa kusema kutoa ni moyo usambe ni utajiri. Ni wakati wa kila mtu kuchukulia tatizo la mwenzake kama la kwake na siyo kutumia muda mwingi kushangilia matatizo ya wenzako.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni Mwigulu na Paul walichofanya kwa Chidbenz ni heko sana.
#kutoanimoyo
#mlimwengumimi
 
Anafanya hivyo kuwarubuni nyie mabwege!! Huyo ni mtu muovu anaficha makandokando yake
 
Back
Top Bottom