VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
- Agosti 24, 2015 siku moja baada ya CCM kuzindua kampeni zake za Urais, Ubunge na Udiwani katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, niliandika hivi:
Mimi VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa,kada nguli wa CCM na mshiriki wa shughuli za kila siku za kampeni,najitoa rasmi kwenye timu ndogo za kampeni zilizoundwa na chama. Mimi, bila ya kushurutishwa na nikiongozwa na dhamira yangu safi ya demokrasia safi, sitashiriki kwenye kampeni za jukwaani,mitandaoni na mitaani kumnadi mgombea wetu Dr.John Pombe Magufuli.
Ufunguzi wa kampeni za chama changu umetoa taswira ya kuogofya kwa wananchi kutuonesha kuwa tumeishiwa sera na hatuzitaki kura. Mikoa niliyopangiwa kwenda ya Iringa, Mbeya,Rukwa na Katavi nitawajibu nini wakiniuliza kama kweli wao ni malofa na wapumbavu? Jana, CCM yetu imeonesha ilivyo mahiri wa kusema chochote bila malengo ya kuomba kura. Dr. Magufuli amehutubu kwa dakika 53 bila ya kuomba kura.
Siwezi kushiriki kampeni ambazo hazijikiti kwenye Ilani yetu. Waratibu 32 wa kampeni ya Magufuli wamepania kushambulia watu badala ya kusema kilichofanyika na kitakachofanyika kwa miaka ijayo. Wameapa kushambulia personalities badala ya kuzungumzia realities. Siwezi na hata sitamani kushiriki kampeni za aina hiyo kwakuwa mimi ni mfuasi wa siasa safi chamani na nchini.
Lakini,sihami chama. Kura yangu bado iko pending. Kila la heri makada!
- Dr. Magufuli akashinda Urais na sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa utawala wake, kimaneno na kimatendo, nasema ASANTE MUNGU KWA KUNIWEKA NAYE MBALI TANGU MWANZO. Ningekuwa muungaji mkono wake tangu mwanzo, leo hii nisingekuwa na amani moyoni mwangu na furaha ya raha.
Niliona mbali kwa darubini kali!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam