Asante Mungu, deni la HESLB limekwisha

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Wakuu hopefully mko salama

Haikuwa kazi rahisi, Ila atimaye my salary slip haisomi tena makato ya higher education student loan board (HESLB).

Baada ya msoto wa makato kwa muda wa miaka 5 ndani ya nyavu za Bodi ya mikopo, hatimaye deni hilo limekwisha na hati ya mshahara ya mwezi wa tano ime-decrare the deduction is off.

Japo nilitambua umhimu wa malipo hayo, Ila kiukweli, makato hayo yalikuwa mzigo mkubwa na mara nyinyi yalininyima usingizi.

Natambua nimetimiza wajibu wangu wa kulipa mkopo ulionisaidia kupata elimu ya juu. Nitumie wasaha huu pia kuwashukuru wananchi wa Tanzania kupitia serikali ya Tanzania, kwa kunipa fursa ya kujielimisha kwa level of my first degree kupitia kodi za watanzania.

Niombe serikali iendelee kutoa fursa hii kwa vijana wa kitanzania ili wafikie ndoto zao za kujielimisha. Hata ivyo, kwa wazazi wenye uwezo usiruhusu mwanao kumbebesha mzigo huu wa deni la elimu ya juu. Hakika unachosha na kuvujisha jasho kwa kijana ambaye ndo kwanza anaanza maisha.

Mwisho kwa wale ambao mmeshamaliza deni la HESLB naomba kujua taratibu ya kupata loan clearance certificate, coz Kuna rafiki yangu mmoja amenishitua kuwa unawaza ku clear deni kwenye salary slip Ila ukienda bodi ya mkopo unaweza kuta bado unadaiwa, hii imekaaje wakuu?
 
Nenda pale bodi wape index number yako ya form four watakuangalizia. Wakikuta limeisha watakupa hiyo clearance, wakikuta bado itakulazimu urudi umtaiti mwajiri wako kwamba marejesho alikua anapeleka au laa?

Kwa kuanzia anza na huo utaratibu utapata tu clearance letter.
Thanks Mkuu
 
Ushauri Kama una mtoto ebu jaribu kumuandalia mazingira ya ada ya elimu ya juu hapo baadae kwa kuweka akiba asilimia 15 Kama ilivyokua unakatwa na heslb hivyo iwe Kama mwendelezo wa makato
 
Makato ya mkopo ni sahihi kabisa, mtoto akatwe kwenye mshahara wake kwa kuwa alitumia mwenyewe hiyo pesa... waelezwe tu mapema kuwa ‘boom’ ni Salary Advance so waitumbue kwa kujua.

Mzazi kuendelea kusota na kujibana kwa ajili ya msomi, ili tu eti asije kukatwa mshahara ni kuteseka tu... itegemeane tu kipato cha mzazi.
 
Wasiliana na zonal offices kwa sehem uliyopo wao watakupa clearance certificate. Mie nimemaliza mwez wa pili bad luck nilichelewa kutumiwa clearance certificate hivyo ofisini kwangu wakaendelea kunikata, nilikatwa mwez March na April so ni zamu yangu sasa nawadai bodi ya mikopo japo sina uhakika wa kupata pesa yangu.
 
Wakuu hopefully mko salama

Haikuwa kazi rahisi, Ila atimaye my salary slip haisomi tena makato ya higher education student loan board (HESLB).

Baada ya msoto wa makato kwa muda wa miaka 5 ndani ya nyavu za Bodi ya mikopo, hatimaye deni hilo limekwisha na hati ya mshahara ya mwezi wa tano ime-decrare the deduction is off.

Japo nilitambua umhimu wa malipo hayo, Ila kiukweli, makato hayo yalikuwa mzigo mkubwa na mara nyinyi yalininyima usingizi.

Natambua nimetimiza wajibu wangu wa kulipa mkopo ulionisaidia kupata elimu ya juu. Nitumie wasaha huu pia kuwashukuru wananchi wa Tanzania kupitia serikali ya Tanzania, kwa kunipa fursa ya kujielimisha kwa level of my first degree kupitia kodi za watanzania.

Niombe serikali iendelee kutoa fursa hii kwa vijana wa kitanzania ili wafikie ndoto zao za kujielimisha. Hata ivyo, kwa wazazi wenye uwezo usiruhusu mwanao kumbebesha mzigo huu wa deni la elimu ya juu. Hakika unachosha na kuvujisha jasho kwa kijana ambaye ndo kwanza anaanza maisha.

Mwisho kwa wale ambao mmeshamaliza deni la HESLB naomba kujua taratibu ya kupata loan clearance certificate, coz Kuna rafiki yangu mmoja amenishitua kuwa unawaza ku clear deni kwenye salary slip Ila ukienda bodi ya mkopo unaweza kuta bado unadaiwa, hii imekaaje wakuu?
Bei gani
 
Haujamaliza bado kuna amount ambayo huwa wanakata tena ya value for money. Mara nyingi hua wanaanza kukata mwaka mmoja baada ya kumaliza hilo deni. Cha msingi nenda Ofisini kwao wakuangalizie usije ukajiachia na mkopo alafu ukashangaa wamerudi upya na hawaangalii unachukua take home ngapi wapo tayari wakate ubaki na sifuri
 
Back
Top Bottom