Asante Mh. Magufuli kwa kutuamini vijana

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,668
Kwa muda sasa kumekuwepo na dhana potofu kuhusu vijana na utendaji wa kazi. Ni miaka mingi nchini kumegubikwa na upotoshaji wa kuwa vijana hawastahili kupewa nyadhifa kubwa za kuongoza kwa hofu ya kuwa hawana uzoefu na kutilia shaka uwezo na uzalendo wao.

Nakupongeza Mh. Magufuli kwa kukaa kukaririshwa dhana potofu ambazo hazina uyakinifu wa kitafiti kwa kutuamini vijana katika kushika nyadhifa mhimu katika nchi. Kitendo chako cha kijasiri katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala mikoa na wilaya tunaona mwanga mbele asante kwa hilo.

Binafsi hoja za wanaodai vijana hawana uwezo ulikuwa mkakati wa kikundi kidogo cha watu waliokuwa wamejimilikisha nchi hii na kuigeuza kuwa yao, ulikuwepo utaratibu wa watu kuwaandaa watoto wao washike nyadhifa za baba zao mara baada ya kustaafu wao hii hali imekuwepo muda mrefu sana tangu uongozi wa mzee Ruksa na imeota mizizi kipindi cha mzee wa uwazi na ukweli ikakomaa awamu ya mzee wa msoga kiukweli ilikuwa ni upilato usiovumilika na tushukru kwa ujio wako maana pona yetu ilikuwa ujio wako ambao ulighubikwa na jinamizi la ombwe ya uchaguzi ulikuwa na drama za kukatisha tamaa vijana.

Mwisho niwaombe vijana mlio aminiwa na Mh. Rais mchape kazi kuleta mapinduzi na kuhakikishia umma kuwa wakichelewesha maendeleo ya nchi hii kwa kutowaamini vijana. Na pia niwashauri wateule wote kuweka mikakati ya kuwaandaa vijana katika kubuni na kutumia fursa za kiuchumi katika nchi yetu.

Niwapongeze wazee walio amua kulalamika kimya huku wakiomba vijana waharibu kuprove theory yao huku wakisahau kuwa vijana ndiyo wenye HISA kubwa katika umiliki wa taifa hili na wanatakiwa kuchangia sana zaidi yao. Niwashukru sana kwa kukubali shingo upande kukadhi ofisi kwa vijana.

Mwisho nikuombe mh. Rais wangu MAGUFULI usitulaamu vijana wako kuwa tu wavivu wa kuchapa kazi ls hasha shida ni kuwa mfumo wa kiuchumi nchi hii hautuwezeshi VIJANA kuwa wazalishaji wakubwa na WANUFAIKA wa kwanza wa uzalishaji ebu waangalie vijana kwa jicho la ziada hasa graduates ambao unawezs kuwatumia kuwaongoza VIJANA wenye elimu ya katika uzalishaji na kukuza pato la nchi. Ilivyosasa kuna shida moja kwamba GAPE la mawasiliano kati ya vijana wasomi na waliokosa fursa ya elimu hawa wote ni mhimu katika kuzalisha na maendeleo ya nchi ila sasa mfumo wa uchumi hauwakutanishi badala yake ni maadui wakubwa hawapikwi chungu kimoja.

Wako kijana wako mzalendo.
 
Vijana walioteuliwa wasituangushe sasa. ni wakati wa kuthibitisha kwa vitendo kua tunaweza
 
Nashukuru sana vijana kutambua nia njema aliyonayo rais JPM kwenu. Ilibaki kidogo tu mlitumbukize taifa hili katika janga kubwa pale mtu mmoja mfano wa mpiga filimbi wa Hamelini alipoteka akili zenu na kuwazungusha mikono hewani kama majuha huku akiwaimbish' ...... mabadiliko, mabadiliko ......' Na huyo mabadiliko angezama Magogoni, kamwe msingepata hizi nafasi. Kuna wazee toka upande wa pili walikuwa wanasubiri mabadiliko aukwae ukuu wamfuate na lazima angewateua hivyo vijana kuwekwa kando.

Anachofanya JPM kuwaamini vijana ni jambo jema sana kwa afya ya taifa letu. Kwa neema ya Mungu atakapomaliza uongozi wake 2025, bila shaka ataacha viongozi wenye working spirit kama yake.

Come 2025, uongozi wa juu utokane na viongozi vijana wa leo na si wazee wa kizazi cha JK.
 
Kwa muda sasa kumekuwepo na dhana potofu kuhusu vijana na utendaji wa kazi. Ni miaka mingi nchini kumegubikwa na upotoshaji wa kuwa vijana hawastahili kupewa nyadhifa kubwa za kuongoza kwa hofu ya kuwa hawana uzoefu na kutilia shaka uwezo na uzalendo wao.

Nakupongeza Mh. Magufuli kwa kukaa kukaririshwa dhana potofu ambazo hazina uyakinifu wa kitafiti kwa kutuamini vijana katika kushika nyadhifa mhimu katika nchi. Kitendo chako cha kijasiri katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala mikoa na wilaya tunaona mwanga mbele asante kwa hilo.

Binafsi hoja za wanaodai vijana hawana uwezo ulikuwa mkakati wa kikundi kidogo cha watu waliokuwa wamejimilikisha nchi hii na kuigeuza kuwa yao, ulikuwepo utaratibu wa watu kuwaandaa watoto wao washike nyadhifa za baba zao mara baada ya kustaafu wao hii hali imekuwepo muda mrefu sana tangu uongozi wa mzee Ruksa na imeota mizizi kipindi cha mzee wa uwazi na ukweli ikakomaa awamu ya mzee wa msoga kiukweli ilikuwa ni upilato usiovumilika na tushukru kwa ujio wako maana pona yetu ilikuwa ujio wako ambao ulighubikwa na jinamizi la ombwe ya uchaguzi ulikuwa na drama za kukatisha tamaa vijana.

Mwisho niwaombe vijana mlio aminiwa na Mh. Rais mchape kazi kuleta mapinduzi na kuhakikishia umma kuwa wakichelewesha maendeleo ya nchi hii kwa kutowaamini vijana. Na pia niwashauri wateule wote kuweka mikakati ya kuwaandaa vijana katika kubuni na kutumia fursa za kiuchumi katika nchi yetu.

Niwapongeze wazee walio amua kulalamika kimya huku wakiomba vijana waharibu kuprove theory yao huku wakisahau kuwa vijana ndiyo wenye HISA kubwa katika umiliki wa taifa hili na wanatakiwa kuchangia sana zaidi yao. Niwashukru sana kwa kukubali shingo upande kukadhi ofisi kwa vijana.

Mwisho nikuombe mh. Rais wangu MAGUFULI usitulaamu vijana wako kuwa tu wavivu wa kuchapa kazi ls hasha shida ni kuwa mfumo wa kiuchumi nchi hii hautuwezeshi VIJANA kuwa wazalishaji wakubwa na WANUFAIKA wa kwanza wa uzalishaji ebu waangalie vijana kwa jicho la ziada hasa graduates ambao unawezs kuwatumia kuwaongoza VIJANA wenye elimu ya katika uzalishaji na kukuza pato la nchi. Ilivyosasa kuna shida moja kwamba GAPE la mawasiliano kati ya vijana wasomi na waliokosa fursa ya elimu hawa wote ni mhimu katika kuzalisha na maendeleo ya nchi ila sasa mfumo wa uchumi hauwakutanishi badala yake ni maadui wakubwa hawapikwi chungu kimoja.

Wako kijana wako mzalendo.
Hukumbuki wakati akiwa waziri wa ujenzi aliwapa vijana mliomaliza vyuo nafasi nyingi Tanroads mkaharibu? Mkaanza kuwa wala rushwa wakubwa. Wengi mliowekwa kwenye mizani mkawa mnapokea rushwa na kuruhusu magari yaliyozidi uzito kuendelea na safari ili hali mkijua yanaharibu miundo mbinu yetu? Nyie graduates wenye degree moja hamfai. Mnatoka vyuoni mkiwa na tamaa yakuwa na maisha mazuri ndani ya muda mfupi. Kwa hiyo mtafanya lolote liwezekanalo kwa kugushi nyaraka hata kulipa malipo hewa ili tu mtimize uchu mliotoka nao vyuoni. Bora mkae pembeni kwanza msote mitaani labda siku mkipewe nafasi mtafanya kazi kwa nidhamu kubwa.
 
Ndugu hawa wala rushwa waliambukizwa upuuzi huo na maboss wao wakuu wa idara ambao walikuwa mizee tupu, make unaapewa shift kesho linauliza kawaida iko wapi hapo kijana lazima ukaombe rushwa tuuh..
 
Mkuu hahahaha, ulichosema ni sahihi kabisa. Mimi yaliwahi kunikuta hayo. Boss kanaipa trip ya kwenda Uganda. Kurudi ananiambia vipi bwana mbona huwakumbuki wazee? hujui hii ni privilege umepata. Kuna wafanyakazi wangapi hapa mpaka uwe wewe tu? Nilicheka tu nikamyeyusha. Basi tokea hapo safari kwangu hakuna. Hahahaha, Yaani umepiga kwenyewe kabisa
 
Iko hivyo mkuu ambaye hajui system iliyopita ndiye anayemwona magufuri yuko wrong haya madingi yametunyanyasa vya kutosha etii..!
 
Back
Top Bottom