Asante Makonda, siku hizi hata uswahilini kuna magari ya doria

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,833
Kama nusu saa hivi nimekuwa nikisikia gari inaunguruma nje ya uzio wangu, ikabidi niamke nikae niangalie ni gari gani na lengo lake nini.

Liliposimama siwezi kuliona naona taa tu na kusikia mlio, sasa lilipoanza kuondoka ndio nimegundua ni Land Cruiser ya Polisi, zile zilizokarabatiwa kwa ubunifu wa Makonda roho ikatulia maana watu wasiojulikana siku hizi ni wengi.

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Makonda manaake siku hizi hata huku Uswahilini kwetu tunaona magari ya doria.
 
Wanaume wa dar yaani gari kunguruma nje ukajua majambazi na ungesikia milio ya risasi si ungejificha kabatini.

Embu ukuje Arusha nikufundishe roho ngumu
Kwahio wewe unasikia gari inaunguruma nje kwako nusu saa nzima usiku mkubwa wala hushtuki?
 
Usikute hao polisi walikuwa wakikutafuta wewe, halafu wakuweke kwenye plastic bag nyeusi. Na wakutupe baharini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom