Asante Magufuli kwa kuelewa hoja, sasa fanya kweli

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa ufupi kilichotokea jana - kwa wale ambao labda wanahitaji tafsiri zaidi - ni kuwa Rais amesema tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Paul Makonda hazijamfanya afikilie mara mbili uteuzi wake. Hili nilazime lieleweke vizuri. Ni kweli kuwa Rais ndiye aliyemteua na ni yeye pekee anayeweza kutengua uteuzi wake. Bila ya shaka njia nyingine pekee ya kawaida kuondolewa katika nafasi yake ni kama Makonda atashtakiwa kwa makosa ya uhalifu ambayo yanamfanya apoteze sifa ya kuwa kiongozi wa umma chini ya sheria ya Maadili ya viongozi. Hivyo, Magufuli amesikiliza yote ambayo watu wengi wameyasema, kuanzia ya vyeti (ambalo kwangu nilisema ni dogo sana) na hili la kutumia madaraka vibaya n.k na ameona kuwa bado Makonda anamfaa.

Rais ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi imesema ina imani na Makonda na kuwa aendelee kufanya kazi. Hoja ya Makonda kuondolewa imefungwa hapo. Period.

Lakini pia Rais amesema kitu kingine kizuri ambacho wengine tumekipazia sauti; kwamba taifa limejikuta kwa karibu miezi miwili tunazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa hayaongezi unga kwenye sufuria, wala kuongeza chaki kwenye shule. Tumekaa kana kwamba tumegeuka na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Wambeya wa Tanzania (JMWTZ). Na kwenye mitandao ndio kabisa tunafuatilia ni udaku, ubuyu, umbeya gani umeingia leo na kwa namna fulani imekuwa ni burudani ya aina yake kwenye inbox za watu mbalimbali. Nani anatuhumiwa nini, nani kalala wapi na nani?

Sasa Rais ameona hili na kauli yake jana imenipa matumaini; kwamba, amewataka wananchi wa Dar-es-Salaam (na bila ya shaka wa Tanzania nzima) kuwa "tujiendeleze katika masuala ya maendeleo, na ustawi wa Watanzania. Tumejielekeza mno kwenye masuala ya udaku, yanayotupotezea muda, ambayo hayatupunguzii hata njaa tuliyonayo, hayatoi matatizo ya msongano katika jiji la Dar-es-Salaam, hayatuongezei hata shibe... haya ndiyo yanachukua muda wetu mwingine." na akaongeza kuwa inatupasa "tuzungumze uchumi na Watanzania na maendeleo yao. Tujiendeleze katika mambo ya maendeleo"

Mimi nakubaliana na Rais na labda niseme labda Rais anakubaliana na mimi pia. Lakini haitoshi kwa yeye kututaka sisi wengine wote tuzungumze mambo ya maendeleo. Haitoshi kwa yeye kutaka watu wa Dar-es-Salaam wazungumze mambo ya uchumi wakati yeye na serikali yake ndio wanawaondoa watu kwenye mazungumzo ya maendeleo na uchumi!

Kama nilivyosema katika makala yangu moja huko nyuma; kwa sisi tuliomuunga mkono na kukataa mabadiliko yale feki kinachotuudhi sana na kukera kwa wakati mmoja ni kuwa tunaanza kuona yale yale ambayo tuliyoyakataa! Matamanio yetu ni kuwa serikali ya awamu ya tano kweli ingejikita kwenye "kazi tu"! Bahati mbaya sasa imekuwa ni "Hapa Mikwara Tu", "Hapa Vitisho Tu", "Hapa Kukomoana Tu" na "Hapa Udaku tu!"

Rais hafanyi tena ziara za kushtukiza, viongozi wengi wanaonekana wamerudi kwenye default position - ya kutegeana, kuangaliana na kusubiriana. Siyo hivyo tu, hata huko juu sijui kama wanataka watu wajadili mambo mengine au la; tangu mwishoni mwa mwaka jana tumezungumza masuala ya Godbless Lema, mara ya mambo ya Zitto, mara madudu gani sijui Bungeni, mara hili mara lile; sasa hao Watanzania watakaa saa ngapi na kujadiliana masuala ya muhimu ya kitaifa au mahali wanapoishi?

Kuna habari kwa mfano huko Dodoma - Makao Makuu ya nchi kuna mahali kina mama wanaambiwa waendee na maji yao kwenye kituo cha afya ambacho kinatarajiwa kuwa hospitali teule kwa sababu kituo hakina maji na sisi tumekaa tunashindana juu ya cheti cheti cheti! Taifa zima! Tumekaa Lissu asigombee asigombee, tunatumia raslimali kumkamata toka Dodoma na kumleta Dar na baadaye kumuachia! Halafu watu wazungumze kuhusu maendeleo yapi? Kwenye eneo hilo hilo Dodoma watu wamejenga mochwari sijui genius gani na sasa haiwezi kutumika kwa sababu imejengwa hovyo na sisi tumekaa kushindana kwenye nani anajua zaidi undani wa chumba cha mwingine!*

Hivyo, na kubaliana na Rais kwamba imetosha kujitoa kwenye mijadala ya maendeleo. Watu maskini wa taifa kama la kwetu "kupoteza" muda ni uhalifu kwa vizazi vijavyo. Watoto wetu wanakaa na kutuangalia tunavyojibishana kwenye luninga na wanatuona tunavyokenua macho tunapopeana mipasho wenyewe tukiamini tunatunishiana misuli! Tunawalaani hawa watoto na uzao wao! Hakuna kiongozi anayezungumzia Maktaba katika kila wilaya au kila kijiji - si mpaka watoto waende maktaba umewahi kuona lini waziri au mbunge ameenda maktaba!? Tunawatendea dhambi isiyosameheka watoto ambao wanahangaika kupata chanzo, tunatenda dhambi isiyosameheka baada ya kuwapa matumaini watoto masuala ya madawati lakini bado tumewalaani kwenye madarasa yasiyo salama na shule ambazo ziko chini ya viwango vya matumizi ya binadamu!

Wakati mwingine tunaafikiria kweli Tanzania ni Dar na hivyo porojo za watu wa Dar zinatakiwa zimeze mijadala ya watu wa Kigoma, Rukwa, Katavi, Singida, Taboda n.k! Kuna watu wanadhani tumelaaniwa, ukweli ni kuwa tunajilaani sisi wenyewe kila kukicha na kupitisha laana hiyo kwa watoto wetu na Mungu aturuhumie tusije kupitisha kwa watoto wa watoto wetu!

Ni kwa sababu hiyo miye nina maombi tu kuwa Raisa ameonesha kuelewa haja ya mjadala wa kitaifa kurudi kwenye masuala ya kitaifa. Basi atengeneze njia.

1. Siyo kila anayembishia awe na ugomvi naye -iwe Bungeni au nje ya Bunge. Aache Bunge lifanye mambo yake.
2. Kesi zile za kisiasa hasa ambazo zinaonekana kukandamiza haki za wanasiasa mbalimbali zifutwe ili watu waendelee na shughuli zao na raslimali zetu zitumike kwenye mambo mengine.
3. Kamata kamata nayo ikome; inapotokea mtu anakamatwa basi iwe kwa kitu ambacho kweli kina uhalifu au tishio la uhalifu ndani yake.
4. Kesi zinazohusiana na uhuru wa maoni na mawazo zifutwe nazo kwani kama alivyosema Rais mwenyewe watu wana uhuru mkubwa wa kusema. Waachwe watu waseme, wale watakaosema vitu vya kihalifu kweli wakamatwe kama ilivyo sehemu nyingine duniani. Tusikamate watu kwa sababu wamesema jambo la kukera au kuudhi hata kama ni la kweli. Tunawapa watu sababu ya kusema mambo mengi na kuyaacha ya maendeleo.
5. Serikali iendelee na shughuli za kusimamia nidhamu, kufanya kazi na utendaji kazi. Tuachane na mambo petty na Rais mwenyewe aoneshe hili. Afanye kama ni kujisahihisha na kuiweka timu yake pamoja. Hakuna sababu ya yeye kuonekana anashindana na watendaji wake kwani inawafanya watu waseme mambo mengine ambayo labda hata hayana ukweli lakini kwa vile wamepewa sababu watasema!

Ni ombi langu kuwa Rais arudi kwenye ahadi zake za uchaguzi, na kuwa alikuwa amesema yeye ni Rais wa wanyonge na wanyonge ni wote; na kuwa alisema hatowaangusha. Ni ombi langu na kilio changu kuwa asituangushe! Kama aliahidi kutukuvumilia ubovu, uzembe, ufisadi n.k basi asionekane kuvumilia fulani fulani. Aliahidi kuwatumikia Watanzania sikumbuki kama aliahidi kuwalingishia Watanzania urais wake!

Na niseme neno moja tu kwa Makonda. Una bahati kuwa Rais ameonesha imani yake kwako. Ni wakati wa wewe mwenyewe kujiangalia, kujisahihisha na kutengeneza ulipobomoka. Usije kukaa na kutegemea imani ya Rais tu ukaamini unaweza kufanya lolote. Kikwete alikuwa na mtu wa karibu kama Kitwana Kondo; na tunajua ukaribu wake na Ditopile lakini tulisema humu sisi wakati ule na sheria ilifuata mkondo. Magufuli amekuacha si kwa sababu unafanya vizuri; amekuacha ili kufunga vinywa vya sauti zilizokuwa zinampigia kelele; amekuacha ili kuwaambia watu "yeye ndiyo alfa na omega wa utawala nchini" kitu ambacho ni kweli. Usichukulie hili kama kukubalika kwake. Sasa hivi unajukumu la kujenga imani ya wananchi unaowaongoza na hasa ambao wamekwazwa na kauli zake ambazo hazijapimwa wakati mwingine ne vitendo vyako ambavyo vinaonekana kutumia madaraka vibaya. Rais kakuambia uchape kazi, tafadhali nenda kachape kazi, tatua matatizo ya watu wa Dar, onesha heshima kwa mkubwa na mdogo (sijui kwanini kijana mdogo hukuweza kujishikia muamvuli wakati umeenda kufungua barabara bandari juzi ile!?). Ni lazima uanze kuonesha unakomaa katika hekima vinginevyo, ukiondolewa au ukiondoka hakuna atakayekusikitikia au kukulia!

Haya turudi kwenye mijadala ya maendeleo:

NB*: WAJAWAZITO NA WAGONJWA WATAKIWA WAENDE NA MAJI HOSPITALI!

Mwanakijiji,
Nimekusoma.

Maalim Faiza nimekuja mwalimu wangu.
Hebu Mwanakijiji nami nisome kidogo.

Haya niliyoandika nimewaandikia rafiki zangu kuwatahadharisha bila
kuwahofisha:

''Ndugu zanguni kuna mtu akiitwa Papa Doc akitawala Haiti...

Huyu jamaa alikuwa na stori nzuri sana za kusisimua kama we ni msikilizaji
isiwe mkasa uko kwako...

Alikuwa na kijeshi chake kinanaitwa Ton Ton Macoute...
Hawa jamaa walikuwa mabingwa sana kwa hakika walikuwa wataalamu...

Ton Ton walikuwa wakiogopewa sana na wananchi si kwa yale marungu
yao au bunduki au nondo zao za chuma kigumu la hasha.

Ton Ton wakitisha kwa zile ''sun glasses,'' yaani miwani ya jua waliyokuwa
wakivaa hadi usiku...

Hawa jamaa wakijua kazi yao...
Maana wananchi hawagwai kwa zile silaha za moto au vitu vyenye ncha kali...

Aaa...wananchi wao wanaogopa miwani ya jua...
Ikiwatisha.

Usisikie bwana Afrika sisi mabingwa wa kuiga...
Tukikuusudu tunakuiga...

Komando Hamza Kalala - waimbaji wamesimama kuimba wameachia ala
zitembee.

Komando Hamza Kalala anatia gita la Franco na vyombo vyote hapo
wanashusha mipigo ya TP OK Jazz - Tout Puissant (Kushinda Zote).

Unakuja kujua kuwa si OK Jazz pale utakaposikia mwimbaji anaita, "Oh! Kalala!"

Hapo ndipo unabaini kuwa hakuwa Franco na akina Madilu System au Josky
Kaimbukuta
, hawa ni watoto wa hapa hapa nyumbani.

Kuna Dally Kimoko...mtoto ana balaa na gita la Maestro Lwambo...ukimsikiliza
unasema ndiye mwenyewe Lwambo Makiadi kafufuka...

Sasa siku nyingi tumeanza kuiga vitu vya ki-Ton Ton Macoute...
Kitu Zombies hivi...

Ndugu zetu wa Zanzibar wao haya wana uzoefu nayo yaani ya Ton Ton Macoute
na kuvamiwa kwa FM Stations.

Fela Kuti alitunga nyimbo kuhusu hawa jamaa...yaani Zombie kisha akatunga
na nyimbo, ''ITT - International Thief Thief.''

Tunakwenda vizuri katika haya mambo ya kuiga ila itabidi kuboresha kidogo kwa
kuvaa miwani ya jua tuwapo kazini...

Unajua hizi CCTV camera nuksi kidogo.
Clip zake zinakera sana zikimwagwa hadharani mtu hawezi kujificha.

Si hilo tu Ton Ton Macoute walikuwa wanapendeza sana kwenye picha wakiwa
ndani ya ''sun glasses.''

Lakini kubwa wananchi wakawa sasa wanaogopa hii miwani ya jua kuliko bunduki
na nondo zao.

Ndipo pale mwanzo nikasema hawa jamaa walikuwa wataalamu sana.
Walikuwa wanajua umuhimu wa kuvaa miwani ya jua hata usiku wa manane.''

Mwanakijiji,
Nadhani kwa kiasi umenielewa...
Ulipotea siku nyingi na Majlis ikawa imepooza.
 
Wana dar hatuwezi tawaliwa na mtu ambaye vyeti vyake havisomi. Hili tutalisimamia hadi mwisho.
5
Tulikuonya mapema sana,omba msamaha kwanza
Vibaraka wote wa huyu msukuma ni lazima tuwaeleze waziwazi tena kwa kauli kali, hakuna mtu wa kushindana na umma na akaushinda umma.

Hii ni vita mpya tunapamba dhidi ya madawa ya kulevya madaraka, hili ndio muhimu kuliko yote, kama Tanzania haina maendeleo kwa miaka 50 hatuwezi kuwa na maendeleo leo ya kutowa parole kwa vibaka kama Bashite ambao hata mahakamani hajapelekwa.

Mamlaka ya Rais ni kusamehe wafungwa tu na si kutowa msamaha kwa watuhumiwa.

Rais anavunja katiba na hatuwezi kulikubali hili hata waletwe vibaraka wangapi hapa JF na thread zao zilizojaa unafki kama huyu MM.
 
Halafu na huyu aliyemsimamia kidete kumtetea ndo alikwenda studio kulazimisha shirika la wambea duniani (shilawadu) iruke hewani ili mkulu afurahie umbea tena kwa mtutu wa bunduki
Kitu kinachonifurahisha zaidi wale watetezi wa upuuzi safari hawatokuja na ule utetezi wao uchwara kwamba Rais anashauriwa vibaya, yeye mwenyewe ameshaweka wazi haambiwi wala kuelekezwa na yeyote afanye nini.

Ningependa kwa sasa washauri wote wa Rais muwatenge na madudu haya yanayofanywa na mungu wa Tanzania.
 
Boss Mzee Mwanakijiji leo umeandika vizuri sana, Hongera.

Mimi ombi langu kwa Rais, aanze kusoma Hotuba, asiwe anahutubia kutoka kichwani. Hii ndio iwe Hotuba yake ya mwisho ya kutoa kichwani.

Nakuunga mkono Hotuba za Rais zimejaa Hasira, Vitisho, Vijembe baada ya kujaa Busara na Hekima.

U Rais ni Cheo cha mwisho kabisa na Taasisi yake. Rais anatakiwa awe anaelekeza, anatoa majibu, anapanga, anaongoza njia, anakuwa Mfano.

Am still Speechless na Hotuba yake aisee.

Kikarara,
Rafiki yangu mmoja nimemwandikia haya ili nimefikirishe kidogo:

''Kughushi ni kosa la jinai.

Mathalan ikiwa mwajiri wake alimpa kazi kwa vyeti hivi vinavyozungumzwa
ni wazi ni kuwa walijua ni vyeti halali.

Serikali isingeweza kumwajiri mtu aliyefoji vyeti. Lakini sasa serikali imeelezwa
kuwa hivyo veti ni vya kughushi.

Wanaosema haya ni wananchi.
Wajibu wa serikali sasa ni kufanya uchunguzi na kusema ukweli wa jambo hili.

Mambo haya yanataka ubongo uuweke wazi ndipo utakapofaidi.
Tatizo ni dogo sana.

Vyeti ni halali au si halali?
Kwani mwajiri hataki kujua hili?

Ukiambiwa na jirani yako nyumbani kwako kuna sege la nyuki unaingia ndani
kuangalia liko wapi ulitoe.

Humlaumu jirani yako kwa kukutahadharisha.
Wala humwambii kwa hamaki aje yeye kuliondoa.

Serikali ina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi vinginevyo itaweka "precedent"
mbaya kuliko ubaya wenyewe...''
 
Taratibu mjomba , Unatueleza Watanzania kuwa kutumia matokeo ya mtu mwingine kujiendeleza kielimu ni Jambo dogo?, Wewe nadhani unaelewa vizuri unachokisema lakini umeamua kujitoa ufahamu katika hilo!. NIKUKUMBUSHE TU KUWA HILO NI KOSA LA JINAI NA KIFUNGO CHAKE NI MIAKA SABA JELA!

Nakubaliana na wewe kuhusu Mijadala, Watanzania tuna haki ya kujadili chochote ilimradi hatuvunji sheria, hakuna mwenye haki au power ya kudictate Watanzania wajadili nini katika hayo wenye haki nayo!. Kama wewe unataka kujadili uchumi fine, jadili uchumi, kama mtu mwingine anataka kujadili mpira fine, wacha ajadili mpira!, Kama mtu anataka kujadili Shilawadu mwache ajadili Shilawadu

Nashangaa katika kuzungumza yote, unajaribu kupiga polish Makosa mabaya kabisa yaliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, This is ridiculous, Nilitegemea Kuwa Ungesimamia Principle ya sheria ni msumeno, Kwamba imani ya Rais kwa Makonda si kinga yake ya Kushtakiwa kwa Makosa aliyoyafanya, Nilitegemea Uungane na wananchi kutaka Makonda ashitakiwe kama wananchi wengine wengi wanavyoshtakiwa kwa makosa kama yale yale aliyoyafanya Makonda,na kama akihukumiwa basi kwa kuwa Rais anaridhika na anamuamini ampe msamaha wa Raisi kisha amteue tena kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, hili limo ndani ya mamlaka ya Raisi.

Lakini huu Ushauri unaoutoa kwa Makonda, Ni kama Ushauri kwa Mtoto Mtundu mwnye Tabia ya Kuwazibua Vibao wageni, halafu anakimbilia kwa baba yake huku analia, Baba anambembeleza kwa kumwambia "Usilie mwanangu eeeh, lakini usirudie tena eeeeh, haya chukua hii elfu kumin ukanunue chipsi na kuku".Nikukumbushe wewe Mwanakijiji MAKONDA HATUHUMIWI KWA MAKOSA YA KAWAIDA YA KIKAZI, MAKONDA ANATUHUMIWA KUFANYA JINAI!

Na unapotwambia kuwa Raisi katika nchi hii ni Alfa na Omega hiyo siyo kweli, Siyo kweli kwa sababu Raisi hana Nguvu za Kuufanya Uongo uwe Kweli au kuufanya Ukweli uwe Uwongo!, Raisi hana Mamlaka kuifanya haki iwe batili au batili iwe haki, Kiufupi Kama kweli tunafuata Utawala wa Sheria nchini basi Haitakiwi raisi kuzuia Sheria isifuate Mkondo wake kama kuna jinai imetendeka!.

Ni lazima Tuseme Ukweli, Msema Ukweli ni mpenzi wa Mungu.
Mkuu hilo la raisi kwamba ni alfa na omega kwa Tz mbona limeshajidhihirisha kwa maneno na vitendo? "Mimi ni raisi, sipangiwi na hakuna wa kunielekeze nini cha kufanya".

Ni kweli hakuna anayempangia cha kufanya. Angalia matumizi ya fedha za serikali ambazo bunge ndilo pekee lenye mamlaka ya kupanga na kupitisha bajeti, anafanya anavyotaka. Amesema anaweka katiba pembeni kwa sababu anataka kunyoosha nchi, na ndivyo anavyofanya, kapiga marufuku mikutano na maandamano ambayo ni halali na yapo kisheria.... mambo ni mengi, sasa hapo utasemaje kuwa raisi kwa Tz siyo alfa na omega?

Naamini tungekuwa na bunge imara, ambalo halitishwi na kauli kwamba msipofanya hivi.."nitavunja bunge", hapo raisi hawezi kuwa alfa na omega kwa sababu wangemuwajibisha.
 
nilijua upele umepata mkunaji...na nikawa nasubiri kwa hamu hiyo mahakama ya mafisadi ianze kuwapeleka watu jela na kuwafilisi kabisa kwa makosa ya kuifisadi nchi.
Kinachotokea sasa ni disappointment...
Umenena vema mkuu,kuna nyumbu wa Lumumba humu kila siku hawaishi kupotosha ''eeeeeh mlitaka raisi dikteta sasa mbona mnalalamika''ovyo kabisa, tulitaka raisi asipepesa macho wala kumwangalia mtu usoni inapofikia mtu kavunja sheria,kala rushwa au kafisadi sasa imekuwa kinyume chake wananchi hao kila uchao anawaita wanyonge biashara zimedoda kitaa kwenye majanga hakuna msaada wowote.
 
  • Thanks
Reactions: GSL
Walishakwapua akili zake huyu hekima na busara za miaka ya nyuma. Sasa kabaki kubwabwaja tu na cheo anachokitafuta kwa nguvu zote hajakipata. Inashangaza sana mtu kubadili misimamo yake kiasi hiki.

Anatuambia tuache udaku wakati ni yeye juzi aliyesema anapenda SHILAWADU? Inashangaza sana.

BTW leo kwa mara ya kwanza nimesoma bandiko lako lote,naam...unaanza kurudi kwenye ubora wako.
Bila shaka ule mgao wa 'mihogo' umeanza kupungua au umeisha kabisa hahahaaa.
 
Mzee mwanakijiji nawe ni mbaguzi wa hali ya juu inamaana huna huruma kwa wale waliofukuzwa kazini kisa cheti si chao! Walioporwa mafao yao, Je mtumishi wa serikali aliyetoa taarifa kuwa naTanzania kuna chembe chembe ya ugonjwa wa Zika na anayeteka nyara kituo cha habari nani anastahili kufukuzwa kazi?? Watu hawana chuki na makonda ila wanachochukizwa nacho ni ubaguzi wa kiwango cha juu kati ya mtu na mtu huku katiba yetu ikisema watu wote ni sawa.

Mtu aliyejibu swali huku amelewa mheshimiwa kitwanga na anayevamia kituo cha habari nani atumbuliwe??

Mdada aliyetoa taarifa zisizo sahihi juu ya scanner za uwanja wa ndege na aliyevamia kituo cha habari na bunduki nani afukuzwe kazi

Mmmh naiona Tanzania wakisahau Watanzania wenzao waliopoteza ajira na mafao yao kwa kosa ambalo mwingine ana kosa hilo na kosa la ujambazi lakini anasifiwa na Rais na watu wengine kama mzee wa kijiji ila hongereni mungu hamfichi mnafiki. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Watu wanafanya kazi sana,yeye pekee yake ndio labda afanyi kazi kwasababu anapata mda wa kuangalia vipindi vya umbea km shilawadu.
Ni kweli kabisa anajifanya bulldozer kumbe ni ufagio wa mkia wa ng'ombe! Anashindwa hata kuteua kwa wakati walio chini ya mamlaka yake!!
 
Soma makala ile nyingine..ukiso.a kwa kuruka mistari utaishia kunitukana bure tu

Mkuu MM mimi ni moja ya kundi linaloangukia katika paragraph ya sita lakini nimeshakata tamaa.

Tukirudi kwenye maada, nilichoandika nimejumuisha yoote uliyoyaandika, wakati mwingine inakubidi ujifunze kuandika kwa kifupi baadala ya kuandika saana mpaka unajichanganya mwenyewe, samahani kwa kukukosoa..

Kiujumla tulipofikia ni bora tuamie kule kwenye kuzungusha mikono na mengine yatajulikana mbele huko potelea mbali, kuna kitu hakiko sawa kwa mtu huyu..

risk taking its not the sin...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa ufupi kilichotokea jana - kwa wale ambao labda wanahitaji tafsiri zaidi - ni kuwa Rais amesema tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Paul Makonda hazijamfanya afikilie mara mbili uteuzi wake. Hili nilazime lieleweke vizuri. Ni kweli kuwa Rais ndiye aliyemteua na ni yeye pekee anayeweza kutengua uteuzi wake. Bila ya shaka njia nyingine pekee ya kawaida kuondolewa katika nafasi yake ni kama Makonda atashtakiwa kwa makosa ya uhalifu ambayo yanamfanya apoteze sifa ya kuwa kiongozi wa umma chini ya sheria ya Maadili ya viongozi. Hivyo, Magufuli amesikiliza yote ambayo watu wengi wameyasema, kuanzia ya vyeti (ambalo kwangu nilisema ni dogo sana) na hili la kutumia madaraka vibaya n.k na ameona kuwa bado Makonda anamfaa.

Rais ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi imesema ina imani na Makonda na kuwa aendelee kufanya kazi. Hoja ya Makonda kuondolewa imefungwa hapo. Period.

Lakini pia Rais amesema kitu kingine kizuri ambacho wengine tumekipazia sauti; kwamba taifa limejikuta kwa karibu miezi miwili tunazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa hayaongezi unga kwenye sufuria, wala kuongeza chaki kwenye shule. Tumekaa kana kwamba tumegeuka na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Wambeya wa Tanzania (JMWTZ). Na kwenye mitandao ndio kabisa tunafuatilia ni udaku, ubuyu, umbeya gani umeingia leo na kwa namna fulani imekuwa ni burudani ya aina yake kwenye inbox za watu mbalimbali. Nani anatuhumiwa nini, nani kalala wapi na nani?

Sasa Rais ameona hili na kauli yake jana imenipa matumaini; kwamba, amewataka wananchi wa Dar-es-Salaam (na bila ya shaka wa Tanzania nzima) kuwa "tujiendeleze katika masuala ya maendeleo, na ustawi wa Watanzania. Tumejielekeza mno kwenye masuala ya udaku, yanayotupotezea muda, ambayo hayatupunguzii hata njaa tuliyonayo, hayatoi matatizo ya msongano katika jiji la Dar-es-Salaam, hayatuongezei hata shibe... haya ndiyo yanachukua muda wetu mwingine." na akaongeza kuwa inatupasa "tuzungumze uchumi na Watanzania na maendeleo yao. Tujiendeleze katika mambo ya maendeleo"

Mimi nakubaliana na Rais na labda niseme labda Rais anakubaliana na mimi pia. Lakini haitoshi kwa yeye kututaka sisi wengine wote tuzungumze mambo ya maendeleo. Haitoshi kwa yeye kutaka watu wa Dar-es-Salaam wazungumze mambo ya uchumi wakati yeye na serikali yake ndio wanawaondoa watu kwenye mazungumzo ya maendeleo na uchumi!

Kama nilivyosema katika makala yangu moja huko nyuma; kwa sisi tuliomuunga mkono na kukataa mabadiliko yale feki kinachotuudhi sana na kukera kwa wakati mmoja ni kuwa tunaanza kuona yale yale ambayo tuliyoyakataa! Matamanio yetu ni kuwa serikali ya awamu ya tano kweli ingejikita kwenye "kazi tu"! Bahati mbaya sasa imekuwa ni "Hapa Mikwara Tu", "Hapa Vitisho Tu", "Hapa Kukomoana Tu" na "Hapa Udaku tu!"

Rais hafanyi tena ziara za kushtukiza, viongozi wengi wanaonekana wamerudi kwenye default position - ya kutegeana, kuangaliana na kusubiriana. Siyo hivyo tu, hata huko juu sijui kama wanataka watu wajadili mambo mengine au la; tangu mwishoni mwa mwaka jana tumezungumza masuala ya Godbless Lema, mara ya mambo ya Zitto, mara madudu gani sijui Bungeni, mara hili mara lile; sasa hao Watanzania watakaa saa ngapi na kujadiliana masuala ya muhimu ya kitaifa au mahali wanapoishi?

Kuna habari kwa mfano huko Dodoma - Makao Makuu ya nchi kuna mahali kina mama wanaambiwa waendee na maji yao kwenye kituo cha afya ambacho kinatarajiwa kuwa hospitali teule kwa sababu kituo hakina maji na sisi tumekaa tunashindana juu ya cheti cheti cheti! Taifa zima! Tumekaa Lissu asigombee asigombee, tunatumia raslimali kumkamata toka Dodoma na kumleta Dar na baadaye kumuachia! Halafu watu wazungumze kuhusu maendeleo yapi? Kwenye eneo hilo hilo Dodoma watu wamejenga mochwari sijui genius gani na sasa haiwezi kutumika kwa sababu imejengwa hovyo na sisi tumekaa kushindana kwenye nani anajua zaidi undani wa chumba cha mwingine!*

Hivyo, na kubaliana na Rais kwamba imetosha kujitoa kwenye mijadala ya maendeleo. Watu maskini wa taifa kama la kwetu "kupoteza" muda ni uhalifu kwa vizazi vijavyo. Watoto wetu wanakaa na kutuangalia tunavyojibishana kwenye luninga na wanatuona tunavyokenua macho tunapopeana mipasho wenyewe tukiamini tunatunishiana misuli! Tunawalaani hawa watoto na uzao wao! Hakuna kiongozi anayezungumzia Maktaba katika kila wilaya au kila kijiji - si mpaka watoto waende maktaba umewahi kuona lini waziri au mbunge ameenda maktaba!? Tunawatendea dhambi isiyosameheka watoto ambao wanahangaika kupata chanzo, tunatenda dhambi isiyosameheka baada ya kuwapa matumaini watoto masuala ya madawati lakini bado tumewalaani kwenye madarasa yasiyo salama na shule ambazo ziko chini ya viwango vya matumizi ya binadamu!

Wakati mwingine tunaafikiria kweli Tanzania ni Dar na hivyo porojo za watu wa Dar zinatakiwa zimeze mijadala ya watu wa Kigoma, Rukwa, Katavi, Singida, Taboda n.k! Kuna watu wanadhani tumelaaniwa, ukweli ni kuwa tunajilaani sisi wenyewe kila kukicha na kupitisha laana hiyo kwa watoto wetu na Mungu aturuhumie tusije kupitisha kwa watoto wa watoto wetu!

Ni kwa sababu hiyo miye nina maombi tu kuwa Raisa ameonesha kuelewa haja ya mjadala wa kitaifa kurudi kwenye masuala ya kitaifa. Basi atengeneze njia.

1. Siyo kila anayembishia awe na ugomvi naye -iwe Bungeni au nje ya Bunge. Aache Bunge lifanye mambo yake.
2. Kesi zile za kisiasa hasa ambazo zinaonekana kukandamiza haki za wanasiasa mbalimbali zifutwe ili watu waendelee na shughuli zao na raslimali zetu zitumike kwenye mambo mengine.
3. Kamata kamata nayo ikome; inapotokea mtu anakamatwa basi iwe kwa kitu ambacho kweli kina uhalifu au tishio la uhalifu ndani yake.
4. Kesi zinazohusiana na uhuru wa maoni na mawazo zifutwe nazo kwani kama alivyosema Rais mwenyewe watu wana uhuru mkubwa wa kusema. Waachwe watu waseme, wale watakaosema vitu vya kihalifu kweli wakamatwe kama ilivyo sehemu nyingine duniani. Tusikamate watu kwa sababu wamesema jambo la kukera au kuudhi hata kama ni la kweli. Tunawapa watu sababu ya kusema mambo mengi na kuyaacha ya maendeleo.
5. Serikali iendelee na shughuli za kusimamia nidhamu, kufanya kazi na utendaji kazi. Tuachane na mambo petty na Rais mwenyewe aoneshe hili. Afanye kama ni kujisahihisha na kuiweka timu yake pamoja. Hakuna sababu ya yeye kuonekana anashindana na watendaji wake kwani inawafanya watu waseme mambo mengine ambayo labda hata hayana ukweli lakini kwa vile wamepewa sababu watasema!

Ni ombi langu kuwa Rais arudi kwenye ahadi zake za uchaguzi, na kuwa alikuwa amesema yeye ni Rais wa wanyonge na wanyonge ni wote; na kuwa alisema hatowaangusha. Ni ombi langu na kilio changu kuwa asituangushe! Kama aliahidi kutukuvumilia ubovu, uzembe, ufisadi n.k basi asionekane kuvumilia fulani fulani. Aliahidi kuwatumikia Watanzania sikumbuki kama aliahidi kuwalingishia Watanzania urais wake!

Na niseme neno moja tu kwa Makonda. Una bahati kuwa Rais ameonesha imani yake kwako. Ni wakati wa wewe mwenyewe kujiangalia, kujisahihisha na kutengeneza ulipobomoka. Usije kukaa na kutegemea imani ya Rais tu ukaamini unaweza kufanya lolote. Kikwete alikuwa na mtu wa karibu kama Kitwana Kondo; na tunajua ukaribu wake na Ditopile lakini tulisema humu sisi wakati ule na sheria ilifuata mkondo. Magufuli amekuacha si kwa sababu unafanya vizuri; amekuacha ili kufunga vinywa vya sauti zilizokuwa zinampigia kelele; amekuacha ili kuwaambia watu "yeye ndiyo alfa na omega wa utawala nchini" kitu ambacho ni kweli. Usichukulie hili kama kukubalika kwake. Sasa hivi unajukumu la kujenga imani ya wananchi unaowaongoza na hasa ambao wamekwazwa na kauli zake ambazo hazijapimwa wakati mwingine ne vitendo vyako ambavyo vinaonekana kutumia madaraka vibaya. Rais kakuambia uchape kazi, tafadhali nenda kachape kazi, tatua matatizo ya watu wa Dar, onesha heshima kwa mkubwa na mdogo (sijui kwanini kijana mdogo hukuweza kujishikia muamvuli wakati umeenda kufungua barabara bandari juzi ile!?). Ni lazima uanze kuonesha unakomaa katika hekima vinginevyo, ukiondolewa au ukiondoka hakuna atakayekusikitikia au kukulia!

Haya turudi kwenye mijadala ya maendeleo:

NB*: WAJAWAZITO NA WAGONJWA WATAKIWA WAENDE NA MAJI HOSPITALI!
Mbona hujaongelea kauli yake kuwa nae ni mpenzi wa Shilawadu? Hilo nalo jambo la maendeleo?
 
Halafu na mimi nifungue posti nyingine kujibu?
Hapana andelea kujibia hapa hapa
Wanabodi,
Hili ni bandiko la kumjibu mwana JF mwenzetu, Mkuu Mzee Mwanakijiji, aliyesema rais Magufuli ni Alfa na Omega, hapa mimi natofautiana naye kuwa rais Magufuli sio Alfa na Omega, Alfa na Omega ni Mungu tuu pekee, rais Magufuli sio Mungu, ni mkuu wa nchi yetu, lakini yeye sio kila kitu, hivyo hawezi kuwa Alfa na Omega.

Tukiacha yaliyo ya Kimungu, tukija kwa yaliyo ya Kaisari na kwenye utawala wa nchi, pia rais sio Alfa na Omega, bali katiba ya nchi ndio kila kitu, rais yuko chini ya katiba. Kitendo chá rais Magufuli kuikanyaga katiba na kuachwa tuu hivi hivi akiangaliwa, ndiko kumepelekea baadhi yetu kumuona yeye ndio kila kitu hadi kumfananisha na Alfa na Omega.
Hata mimi jana nilimsikia rais Magufuli alipozungumza kuwa kwenye mambo ya uteuzi, yeye ndio kila kitu, hakuna yoyote anayeweza kumpangia kitu, hii sii kweli, kiukweli rais sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu hivyo kuna vitu hata rais anapangiwa na kulazimishwa avifanye atake asitake, apende asipende.

Hii maana yake kuna vitu ambavyo rais anavifanya at his discretion kwa mapenzi yake na kuna vitu anatakiwa kuvifanya not at his discretion bali kwa lazima kwa mujibu wa katiba.

Kwanza sote tunakubaliana kuwa Magufuli ndiye rais wetu, ndio mamlaka kuu kupita zote za kiutawala nchini mwetu mwenye nguvu kubwa hivyo anapaswa kuheshimiwa, lakini sio kuogopewa au kuabudiwa as if yeye ni Mungu!. Hili nimelizungumza hapa Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Hizo mamlaka alinazo rais Magufuli, sii malí yake kama John Pombe Joseph Magufuli, bali tumeuazima tuu kama dhamana baada ya sisi (we the people) kumuajiri kazi ya kututawala kupitia taasisi ya urais, sisi ndio waajiri wake, ndio tunayemlipa mshahara wake, tunaemlisha, kumvisha na kumuhudumia yeye na família yake kwa kodi zetu na hizo powers alizonazo kama rais ni tumemuzima tuu kwa mujibu wa katiba na atafanye kile sisi waajiri wake tulichomtuma pale kwenye Ikulu yetu tulipompangisha na sio kufanya chochote anavyotaka yeye.

Rais ana powers, ila sio absolute powers, yuko chini ya katiba, katiba ndio kila kitu, hata rais akimess, anaondoshwa!. Kuhusu mamlaka ya rais kumteua yoyote, nimeieleza hapa. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Magufuli japo ni rais wetu na yeye ni binadamu kama sisi na sio malaika, hivyo ana mapungufu yake, na moja ya mapungufu yake makubwa ni hili kwa vile yeye ndio rais wetu, hivyo anajidhania yeye ndio kila kitu. Lakini kwa bahati mbaya sana, japo ameapa kuilinda katiba, lakini imetokea kuwa kumbe Magufuli haijui hata hiyo katiba yenyewe aliyoapa kulinda ndio maana baadhi ya maamuzi yake yanakwenda kinyume cha katiba, kwake it's OK kwa vile hajui atendalo ni kinyume cha katiba, na anatenda kwa nia njema, na hili hata mimi simlaumu kwa sababu yeye sio mwanasheria ila ni ajabu kwa wanasheria wanaojua rais anavunja katiba lakini wanamnyamazia Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Kwa vile ni yeye ndiye aliyemteua Makonda, anaamini hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumtoa huyo Makonda, kiukweli sio tuu Watanzania wakiamua wanaweza kumtoa huyo Makonda, bali hata yeye ampende vipi Makonda, bali Watanzania tukiamua kwa kauli moja kuwa hatumtaki Makonda kwa sababu za msingi ambazo ni justifiable, sio tuu tunamtoa huyo Makonda wake, bali tunauwezo wa kumtoa hata yeye Magufuli na Makonda wake kwa mujibu wa katiba mradi tuu ziwepo sababu za msingi.

Sababu ya msingi ya kumtoa Makonda, ni iwapo ikithibitika kuwa ni kweli jina halisi la Makonda ni Daudi Bashite, ni kweli alifoji vyeti na akafanya udanganyifu kwa kutumia vyeti vya Paul Chistian kujipatia elimu, ajira hadi uteuzi, then kwa kutumia vipengele fulani vya kisheria, kwa kupeleka shauri mahakamani, then Mahakama inamlazimisha rais Magufuli kutengua uteuzi wa Makonda kwa lazima kwa kutumia nguvu za kisheia, hata Magufuli ampende vipi Makonda ni lazima amtengue!.

Kitu ambapo Magufuli anaweza kukifanya kumuokoa Makonda wake, kwa vile anampenda sana kwa uchapa kazi wake, na rais anayo kinga ya kutokushitakiwa, anaweza kummegea kidogo Makonda hiyo kinga yake ya kutokushitakiwa, hivyo kumkingia kushitakiwa kwa jinai ya kufoji na kufanya udanganyifu, lakini jina la wizi lazima livuliwe hivyo lazima atengue uteuzi wa Paul Makonda kama RC wa Da es Salaam na papo hapo kumteua Daudi Albet Bashite kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Da es Salaam na kuendelea kuchapa kazi.

Na hili likifanyika then tunawashauri wabunge wetu waanze impeachment process kwa hoja ya reaching the highest stages of mind incapacitation hivyo amekuwa a person of unsound mind, amini msiamini, Bunge letu litapitisha unless hizo 2/3 majority inayotakiwa kupitisha hoja hiyo nayo ni ya wabunge of unsound mind kwa upofu wa siasa za vyama!.

Nawaomba mnipe muda niwatafutie vifungu vya katiba na sheria vinavyoonyesha kuwa rais sio kila kitu bali katiba ndio kila kitu, na rais anaweza kufanya maamuzi fulani na mahakama ikayatengua maamuzi hayo kwa kutumia vipengele vinavyoitwa writs or prerogative ordes kama prohibition, certiorari, mandamus, harbea copus na quo warranto ambapo rais analazimishwa kufanya kitu fulani kwa lazima, apende au asipende na akigoma, Bunge linaitishwa na kumfukuza kazi!. Hili lipo, sheria hizi zipo, ila sisi hapa Tanzania hatujawahi kuitumia, lakini anamuondoa madarakani mteule yoyote wa rais hata rais ampende vipi. Kwa vile sheria zetu tumezirithi kutoka India Para materiale, kuna sheria nyingi tunazo lakini hatujazitumia, kwa vile mimi sio practicing lawyer, kuna sheria zipo tuu kama just persuasive tuu, with time tutawathibitishia kuwa rais Magufuli sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu!.
Kuna mtu alifukuzwa kazi na rais, mahakama ikaamuru arudi kazini.
Kuna mtu alitiwa kizuizini kwa amri ya rais, mahakama ikamtoa.
Kuna ile kesi ya Bawata etc.

NB. Katiba yetu imempa rais wetu mamlaka ya kuwa kila kitu endapo tuu atatangaza hali ya hatari, hili likifanyika, hapo ni kweli rais ndio anakuwa kila kitu maana katiba huwekwa pembeni!.

Kuna vitu kibao rais wetu Magufuli alitangaza kuwa atafanya, wakati akitangaza, yeye alitangaza kwa mamlaka kabisa akijidhania anao uwezo huo, au mamlaka hayo lakini kiukweli kabisa, kuna vitu rais anatangaza kuwa anao uwezo lakini hana uwezo huo na mifano
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Rais amefanya mambo mengi tuu kinyume cha katiba lakini kwa vile amefanya kwa nia njema, hakuna aliyelalamika.

Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
Paskali

Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?

Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi!

Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!

Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!.

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Paskali
Paskali
 
Visasi,chuki,ukanda,ukabila kamwe havitasaidia kuongoza nchi.Kinachoendelea ni kuangamia kwa taifa hili.Ee mungu tenda miujiza tuokoe.
 
Kama nilivyosema katika makala yangu moja huko nyuma; kwa sisi tuliomuunga mkono na kukataa mabadiliko yale feki kinachotuudhi sana na kukera kwa wakati mmoja ni kuwa tunaanza kuona yale yale ambayo tuliyoyakataa! Matamanio yetu ni kuwa serikali ya awamu ya tano kweli ingejikita kwenye "kazi tu"! Bahati mbaya sasa imekuwa ni "Hapa Mikwara Tu", "Hapa Vitisho Tu", "Hapa Kukomoana Tu" na "Hapa Udaku tu!"

Mkuu MMMJ nichofurahi hujakata tamaa kama muda fulani zamani kidogo ulivyotishia kuachana na siasa majitaka.
Maisha ndivyo yalivyo! Ni kweli wengine mlikataa Mabadiliko Feki lakini mkakumbatia jezi na viatu vipya mkitumai vitawasaidia ! Bahati mbaya hata hili badindiko lako ni sehemu ya Udaku uliozungumzwa na Bwana mkubwa.

Nadhani faida ya badiliko Feki inaweza kuwa nafuu kuliko kuwa na Jezi na viatu vipya wachezaji na uwanja ule ule.
Tujitafakari sana mbele ya Safari kama kweli wengine wetu ni waumini wa ustawi wa Jamii na si masilahi na kutimiza wajibu kwa mwajiri.

Kama nilivyosema katika makala yangu moja huko nyuma; kwa sisi tuliomuunga mkono na kukataa mabadiliko yale feki kinachotuudhi sana na kukera kwa wakati mmoja ni kuwa tunaanza kuona yale yale ambayo tuliyoyakataa!
 
Kama tunapenda umbea ..udaku,na kuacha kujadili vitu Vya msingi lakini hapohapo kuna MTU anapiga simu anadai anawapenda shilawadu!!!napata mashaka sana..lakini IPO Siku tutafika...kuna watu wanajifanya hawaoni..wanajitoa ufahamu...MTU kabisa anadai tusimfundishe...wala kumuelekeza nini chakufanya..?so tukae kimya?tusifu tuuu...
 
mie napita leo ila nina neno moja kuwa kama kuna watu wamesimamishwa kazi kisa cheti na hao wote ni wenye miili ya udongo wa kitanzania na watarudisha udongo huo baadaye udongoni na huyo naomba aangaliwe pia. kuna kitu rule of law ni nani aifafanue ila nina imani mnaijua wote.
 
Back
Top Bottom