Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

1. Kutoka CCM(juu) kwenda CHADEMA(chini) ni rahisi lakini kutoka CHADEMA(chini) kwenda CCM(juu) ni shida!...
2. Upepo unavuma toka CCM kwenda CHADEMA.
 
Tasfiri yangu ni hii...

1/Daraja la kisiasa limejengwa kuruhusu wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine baina ya CCM na CHADEMA.

2/Mwelekeo wa hilo daraja unaonyesha kuna wepesi(Mteremko) zaidi kutoka CCM kwenda CHADEMA.

3/Mwelekeo wa daraja unaonyesha Uko imara zaidi kwenye kingo za upande wa CHADEMA kuliko upande wa CCM(Ukijenga picha kubwa kuwa ni salama zaidi kisiasa kuhamia CHADEMA ukitokea CCM kuliko kutoka CHADEMA kwenda CCM.

4/Mlingoti wa bendera wa CCM unaonekana umelegea, kuchoka na kuinama kiasi cha kutaka kuanguka, wakati wa CHADEMA uko imara zaidi. (Hii inatoa tafsiri kuwa, CHADEMA ina uungwaji mkono zaidi kijamii kuliko CCM au Kisiasa CHADEMA ndani wako imara zaidi kuliko CCM).
Hata bendera ya Chadema imetandazwa kinyume na ccm imesinyaa
 
Ukiangalia kwa umakini upande wa chadema hauna surface ya kutosha, means wanaokuja huko wanabanana sana na pia nafasi ndogo inareflect ufinyu wa kufikiri. Daraja ni kivuko cha wanaotoka kwenye upeo mkubwa kwenda kwa wenye upeo na fikra ndogo.
far fetched idea
 
tafsiri yangu,
chadema ipo chini na ccm juu, kwa hivyo ili chadema iweze kuifikia ccm kimafanikio, inatakiwa kuwa/kufanya kazi ya ziada (thats why kuna ngazi)
Mzee ngazi ni tofauti na daraja hilo ni daraja na si ngazi
 
Japo kuna mto mrefu kati ya vyama ( tofauti ) lakini bado wanachama wanavuka kwenda ng'ambo zote
 
Tasfiri yangu ni hii...

1/Daraja la kisiasa limejengwa kuruhusu wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine baina ya CCM na CHADEMA.

2/Mwelekeo wa hilo daraja unaonyesha kuna wepesi(Mteremko) zaidi kutoka CCM kwenda CHADEMA.

3/Mwelekeo wa daraja unaonyesha Uko imara zaidi kwenye kingo za upande wa CHADEMA kuliko upande wa CCM(Ukijenga picha kubwa kuwa ni salama zaidi kisiasa kuhamia CHADEMA ukitokea CCM kuliko kutoka CHADEMA kwenda CCM.

4/Mlingoti wa bendera wa CCM unaonekana umelegea, kuchoka na kuinama kiasi cha kutaka kuanguka, wakati wa CHADEMA uko imara zaidi. (Hii inatoa tafsiri kuwa, CHADEMA ina uungwaji mkono zaidi kijamii kuliko CCM au Kisiasa CHADEMA ndani wako imara zaidi kuliko CCM).
Afu hii Bendera ya CCM mbona ni kama sura ya mtu afu ana likidevu lirefu?

Na anaonekana kama anawaangalia CDM kwa hasira kali.
 
IMG_20171108_220739.jpg
 
Kipanya nae si atangaze nia au aombe kukarbishwa malangoni tu.
Hapa anamnanga yule aliyekataa ujinga wa kuomba kufunguliwa malango?
Sasa nimeelewa lengo la wanachadema wengi wanapenda kuichonganisha CCM... Ili waokote makapi..
Shame on you all
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom