Asante Jaji Lubuva kwa matokeo ya 2015

Ume
Mabadiliko-lowasa
Lowasa-mabadiliko
UKIWA hatutasahau siku Ile tumekwenda kuzungushwa mikono pale jangwani
Umenikumbusha mbali sana. Niligoma kuzungusha mikono siku ile kwa sababu nilikuwa na mgogoro wa kifikra hasa nilipokuwa nikikumbuka namna tulivyokuwa tunamnanga mzee Lowasa kabla. Kilichonistaabisha siku ile ni dua toka kwa yule sheikh( sikumbuki jina lake), ilikuwa dua moja ya kibabe sana😀
 
DECLARATION OF INTEREST: Mimi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa, wala sina utaalamu mkubwa wa mbinu za kisiasa. Mimi ni mtanzania huru na mwenye maoni huru.

Licha ya kazi iliyofanywa na sekretarieti ya CCM katika kulikata jina la Lowasa kwenye kinyang'anyiro cha wagombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, watanzania wengi waliingia mkenge wa kumshabikia fisadi Lowasa baada ya kuhamia UKAWA.

Baada ya tuhuma zake nyingi za ufisadi wa mabilioni ya shilingi, mpaka chama chake kumtupa, tuliona jinsi ndugu Lowasa alivyohangaika kwa uchu wa kutaka urais hata ikabidi kutimkia CHADEMA.

Kwa uzee ule na uchovu aliokuwa nao huku akitetema hovyo, hata mimi nilishawishika kuamini huenda angetutoka punde.

Sifahamu kama ni mbinu za kiintelijensia na usalama wa taifa, au ni figisu, hatimaye Jaji lubuva akamfutilia mbali ndugu Lowasa kupitia sanduku la kura huku wafuasi wake wakiachwa macho kodo wakihuzunika kama makinda ya njiwa.

Wakati tukiwa tunastaajabu kwa butwaa, Magufuli akachanja mbuga kwa kasi mpaka ikulu na kutwaa mamlaka. Lakini kwa uchungu, UKAWA wakabaki na fisadi lao huku wasijue walitupe wapi.

Leo hii Lowasa katimkia CCM, na anasema amerudi nyumbani! Tunajifunza nini? Je, mwanasiasa ni mtu wa kuaminika?

Mtu anayeweza kuwasaliti watu million sita waliokesha kumpigia kura, kumdekia barabara, kumsapoti na kumshangilia, mpaka wengine wakavunjwa miguu na polisi?? Huyu mtu anafaa kuongoza nchi? Ana ajenda gani? Ana aminika vipi?

Asante Lubuva kwa kumfyekelea mbali huyu masai uchwara mwaka 2015. Haukukosea . Viva Lubuva.
Mzee Lowassa hakika dhambi uliwafanyia watu zaidi ya milioni 6 itakuhukumu Mungu atasikia kilio chao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ume

Umenikumbusha mbali sana. Niligoma kuzungusha mikono siku ile kwa sababu nilikuwa na mgogoro wa kifikra hasa nilipokuwa nikikumbuka namna tulivyokuwa tunamnanga mzee Lowasa kabla. Kilichonistaabisha siku ile ni dua toka kwa yule sheikh( sikumbuki jina lake), ilikuwa dua moja ya kibabe sana
 
Ndio wasomi tulionao
Eti anaionea fahari tume feki ya uchaguzi tulionao.
Nachomjua kuhusu Lowasa kakosea sana cz ccm walimwogopa sana akiwa ukawa na upinzani walipata kumheshimu
Na bhado sijutii kwa morani kurudi ccm cz naamini hanaga historia ya kushindwa.
Ccm wanafahamu na usalama wataifa wanajua EL kashinda 2015
EL kaona kupambana na ccm akiwa ukawa ni kupoteza mda bure. Bora ajiunge nao ajue cha kufanya
Ile team wakina mwigul,napee,msukuma sijui mtaweka wapi macho yenu
Wenye ccm kwa sasa ni LOWASSA & MAGU, DESPACITO, NA Dk BASHIRU.
 
Kihalisia upinzani ndani ya nchi hauwakilishwi na nyota ya mtu!,bali ni vuguvugu la wananchi waliochoshwa na utawala mbovu.Utawala ambao tangia uhuru unapiga branda za kisiasa ili kujinufaisha!.Hivi sasa ndani ya nchi upande wa upinzani hata ukisimamisha kisiki basi fahamu kitapata kura hata!,kura hizo hata zikiwa chache zisizowedha kukidhi ushindi lakini ujumbe utakua umefika kwamba wananchi wamechoka.Hivyo walio kwenye mamlaka wasome alama za nyakati kwamba alarm inalia tena kwa kasi,wacha wao wanunue watu tena ikiwezekana watumie propaganda ya kila aina lakini idadi ya wananchi waliouchoka utawala inazidi kukua kwa kasi!.Sasa huko tuendako wanaweza kuthubutu kuchukua mamlaka kwa nguvu!,hivyo tujihadhari tuendako kunatisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuwa mpinzani ni kazi ngumu na yataka moyo. mfano Nyerere alitishwa , na akaammbiwa aache kazi ya ualimu kwa vile alikuwa amedhamiria aka simama imara hadi akawa Rais , Mandera alifungwa kwa uchochezi miaka 27 wa marekani weus walipata taabu sana lakini ushupavu wa Martine uliwafikisha pazuri . wana siasa wa upinzani pamoja na wana harakati wote wasife moyo katika rindi la kiza kinene kuna nuru .kila la heri
 
Ogopa sana mtu anayesema/kuandika kwa kutanguliza kanakwamba hana chama. Ogopa sana. Hata wale ambao hawana kadi za vyama mioyoni mwao wana uchama wa kiimani. Kwa hiyo kutuaminisha kwamba hauna chama kwa maana ya ulivyoandika tuna wasiwasi. Andiko lako ni dhahiri liko biased!,. Unaipenda C.c.m iliyopo madarakani, usingeipenda ya lowassa. Kifupi, hata ukawa hauipendi. Pamoja, na kuzunguka zunguka kwako hivi ukisema wewe ni mwanachama wa chama x. Utapigwa?
 
Back
Top Bottom