Asante Igunga na watanzania-Dk Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Maneno yake kwa watanzania kupitia facebook wall page yake leo:

· Dr. Willibrord Slaa

Napenda kutoa shukrani za pekee kwa wana IGUNGA wote kwa ushirikiano wao,na kwa kutupigia kura nyingi. KURA ZENU HAZIJAPOTEA ZIMETOA MWANGA KWA WATANZANIA.Tumalize kazi ya kusambaza ujumbe kwa vijiji vyote TANZANIA. Umoja wetu ndio Msingi wetu.

MYTAKE:

Dr Slaa tunawashauri chadema mbali ya kuwashukuru wana Igunga itisheni mkutano mkubwa Dar muwaeleze wafuasi wa chadema kilichotokea Igunga na kitakachofuata.Dr kumbuka tokea uchaguzi mkuu mwaka jana hamjalitikisa jiji la Dar kupitia viwanja vya jangwani.

Tunataka mkutano mkubwa Dar utakaotetemesha Magamba. Muda sio mrefu Nape amezungumza na waandishi akaropoka maneno mengi kuhusu Igunga na akasema Magamba watafanya mkutano mkubwa Dar kumtambulisha huyo mbunge wao Kafumu.
 
Maneno yake kwa watanzania kupitia facebook wall page yake leo:

· Dr. Willibrord Slaa

Napenda kutoa shukrani za pekee kwa wana IGUNGA wote kwa ushirikiano wao,na kwa kutupigia kura nyingi. KURA ZENU HAZIJAPOTEA ZIMETOA MWANGA KWA WATANZANIA.Tumalize kazi ya kusambaza ujumbe kwa vijiji vyote TANZANIA. Umoja wetu ndio Msingi wetu.


Bravo Dr. Slaa.
Ombi langu kwako:
Elekeza nguvu vijijini. Angalau kila kata kuwe na ofisi imara ya CDM. Basi, then they will be done!!!!!
 
Kushukuru ni Uungwana,what next Dr? Kumbukeni pia kwenda kuwashukuru wana Igunga huko huko Igunga.mwitikio wao umeleta matumaini makubwa ya mabadiliko.
 
Namuunga mkono Dr...hii inaonesha wazi kwamba watanzania wamechoshwa na mkoloni CCM na mwisho wa ccm upo karibu mno...Hata watu wa kenya hakutegemea KANU ingefutika katika uso wa siasa lakini ilitokea now second independence for TZ is near..Viva chadema viva forever.
 
Dr. Slaa nakukubali mkuu wangu, jua kabisa kuwa igunga wamekuchagua wewe na chama chetu, ila hawa waliozoea wizi wa kura wamebadili mwelekeo, siyo kitu wape heshima zao watu wa igunga kama kawaida, ipo siku mambo yatakuwa sawa sawa tu.
 
Maneno yake kwa watanzania kupitia facebook wall page yake leo:

· Dr. Willibrord Slaa

Napenda kutoa shukrani za pekee kwa wana IGUNGA wote kwa ushirikiano wao,na kwa kutupigia kura nyingi. KURA ZENU HAZIJAPOTEA ZIMETOA MWANGA KWA WATANZANIA.Tumalize kazi ya kusambaza ujumbe kwa vijiji vyote TANZANIA. Umoja wetu ndio Msingi wetu.

Afadhali leo umezinduka aisee jana hali ilikuwa mbaya mpaka ukazimia ! jikaze kiume hiyo ndio ccm na hukutegemea jamaa wanaweza kuwafanya vibaya kiasi hicho , mie nilijua tu huwezi kupambana na ccm wao ni jeshi kubwa na lenye rasilimali nyingi . Sasa inakuwaje mmebomoa benki kiasi cha kwamba tshs 1.345bn zimetumika igunga na hamkuapata kitu na chama ndio muflisi sasa
 
mkubwa penda kukubaliana na ukweli hata kama unauma utkusidia kujua wapi ulipojikwaa kauli ya DR inadhihirisha waz kuwa kakubaliana na matokeo na ndio maana kasema inabidi wafanyekazi ya ziada vijijni, huna haja yakutumia lugha ya jazba politics iz not like that

Unajua kwann Cdm hawaja saini matokeo? Kwani Cdm ni nani?
 
Bravo Dr. Ni suala la muda tu Mkuu, the win is just round the corner. Tujiimarishe vijijini kwenye wengi ambao bado wanahitaji kuijua CDM na ukamilifu wake
 
Omr nashushauri ukapimwe akili mental clinic ya karibu kama unaishi ughaibuni. Iwapo upo Bongo basi panda basi la Shabiby uende hospitali ya vichaa inayoitwa Mirembe iliyopo mkoani Dodoma. Baada ya kupewa majibu kuwa mental faculties zako ziko timamu ndipo uandelee kutoa hoja au kuchangia humu jamvini a.k.a jamiiforums. Naomba kuwasilisha rai yangu kwako.
 
Bravo dkt slaa kwani katoka na nini?.si cdm imetoka patupu.mnasema hawana elimu.je watu wa k'ndoni hawana elimu?.suala ni kwamba chama kijenge mahusiano mazuri na BAKWATA na sio kiburi na kuibeza.pia mkubali ccm ni nomaaaaa...mzeewa watu alirukaruka juu ya jukwaa wanaigunga wamemtoa nduki.haamin kilichotokea na nimeshangaa anaibukia FB.CCM OYEEEE NAJUA INAWAUMA ILA NDO HIVYO IPOTEZEENI.MASKINI SILAA HATA NA KAFUMU AMEMFUMUA.
 
Dr. Fanya haya:1. zingatia sana uchaguzi wa selikali za mitaa, nadhani umeona kazi ya mabalozi wanavo2miwa na ccm. 2. Katiba mpya ipatikane kabla ya kuingia kwny uchaguzi mkuu 2015
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom