Asali ni zaidi ya utajiri

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
389
Nawasalimu wakubwa kwa wadogo ktk jukwaa hili,
Kuna kipindi nilileta uzi kuuliza mazingira ya Tabora yalivyo kwani mke wangu alipangiwa kazi mkoa huo,mwaka jana mwezi wa 12 nilienda kumtembelea kipenzi changu wilayani sikonge kijiji sitotaja kwa ajili ya kuficha uhalisia wangu,naweza kufahamika mapema kwa watu waliomo humu na wanaishi kule.

Nilipokua kule kuna watu waliniagiza ASALI mbichi kama 3 hivi,hivyo nilipokaribia kuondoka niliamua kutafuta kwa wenyeji wa pale,nilitaka kununua ambayo imechujwa lkn kuna mdau akanmbia ninunue ambayo haijachujwa kwani inauzwa shlingi 80000 kwa ndoo ya lita 20,ambayo ukiichuja inatoa asali lita 10 iliyochujwa na safi kwa matumi.

Nilinunua ndoo mbili kwa shilingi 160000,ili nikitegemea nichuje nipate lita 20 niwapelkee wadau walioniagiza,ajbu kwenye ndoo hizo mbili nilipata lita kama 28 hivi badala ya 20 ikawa faida kwangu,ktk zile ndoo mbili yale makapi(masega) nilipata kama ndoo moja iliyojaa ya lita 20,ambayo nayo ni dili make wanayauza kwa kilo moja shilingi 3000,lakini ukiyapika unapa NTA kama kilo 3 hivi,ambayo kwa kule kilo ya NTA ni 10000/12000 hivyo kwa kilo 3 ni 30000.

UTAJIRI ULIPPO-
Katika uchunguzi wangu ASALI kule inavunwa kwa wingi mwezi wa 6/7 ambapo ndoo ya lita 20 inauzwa mpaka 40000/35000 kwa ndoo moja,na inapanda bei kuanzia mwezi wa 10 nakuendelea mpaka wa 3/4/5 wanapoanza kuvuna tena, mimi nimenunua asali kipindi ambacho imepanda bei.

NAENDELEA HAPA..
Sasa kama unamtaji nenda tabora mwezi wa 6au 7 tafuta sehemu wanazovuna asali,kipindi hicho utanunua kwa 40000 mpaka 35000 kwa ndoo ya lita 20, na nzuri nunua ambayo haijachujwa kabisa ndio faida zaidi,tafuta sehemu au chumba cha kupanga chenye ukubwa wa kutosha kutegemea na kiasi unachohitaji,kule vyumba bado bei nafuu sana vya kupanga kwa mwezi haizidi 20000,lipia miezi mitano au sita then chukua ndoo zako za asali paki humo nenda kaendelee na shuguli zako.

Iikifika mwezi wa kumi mpaka kumi na moja nenda kauze pale pale asali yako ndoo moja kwa shilingi 80000 na zaidi,wala usihangaike kutafuta soko lilipo,miezi hiyo kule asali hakuna na inapatikana kwa shida kweli kweli,wanunuzi wapo wakutosha 24/7hrs,wanakutafuta wewe,sio wewe kuwatafuta.

Kama pia unaweza na unasoko tofauti na kuuza kule basi fatilia maliasili wakupe utaratibu wa nini cha kufanya kusafirisha asali.

Kwa maana ukiweka mtaji wa 2m baada ya miezi 4 unapata 4m,ukiweka 5m baada ya miezi hiyo ni 10m,kwa maana kua unanunua asali kwa 40000 kwa ndoo,then unakuja kuuza kwa 80000 kwa ndoo ni mara mbili ya ulichokiweka.
Ukiamua kuchuja mwenyewe kuna faida zaidi kwan yale makapi unatengeneza NTA kwa kuipika utauza 10000 kwa kilo moja.

NJIA NYINGINGINE..
Tafuta pori kule kodi au nunua kwani bado kule ni bei nafuu,unaweza kupata pori hata kwa laki tatu mpaka tano kutegemea na ukubwa na mtu anaekuuzia,chonga mizinga yako ambayo unauwezo nayo,kule mizinga wanachonga kwa 2000 pamoja na kupandisha juu ya miti,hivyo ukichonga mizinga 1000 x kuchonga na kupandisha 2000=2,000,000 jumla kwa idadi ya mizinga 1000.

Ikumbukwe kua mzinga mmoja kwa miezi tajwa hapo juu unaweza kuta kila mzinga unatoa ndoo moja ya asali ambayo haijachujwa,hivyo kwa kipindi cha mwezi wa 3 mpaka 6 kuna maua ambayo nyuki hupendelea kuyatumia ndio msimu wake wa kustawi hivyo uzalishaji unakua mkubwa tofautisha na miezi mingine.

Basi tufanye umehangaika wee ukapata ndoo zako 400 badala ya ndoo 1000,na hii ni makadirio ya chini kabisa na haiwezi kua hivyo hata ukose vipi make nikipindi ambacho uzalishaji ni mkubwa sana kule, chukua hizo ndoo 400 tunza,njoo uza mwezi wa 10/11 kwa 80,000 kila ndoo.hivyo ndoo 400 x 80,000=32,000,000m.

Ukisafirisha unaweza kupata zaidi ya hapo,mimi ndio nimeanza kufanya hivyo sio mjuzi sana bado najifunza,nikivuna ntaleta mlejesho nini kimetokea.

SIKU NJEMA KWENU WOTE.
 
Kama vipi niwe partner wako kwenye hiyo ishu niliyakaga kuifanya ila niliyetaka kufanya nae hakuwa hapa tz alivyokuja akawa busy kama tunaweza kuwa partner au unielekeze pa kupita ntashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viwango vya ku export asali from TZ ikidhi hizo sifa hapo chini
Screenshot_2019-04-05-20-58-33.jpeg
Screenshot_2019-04-05-20-56-55.jpeg


***
 
Mie sijaelewa bado hii habari ya baadhi ya viongozi wetu wanatuekea mazingira magumu wajasiriamali kiasi kwamba ili ufanikiwe inabidi utumie njia za panya nyingi ama ukisema ufate process zao basi tegemea anguko tuu katika malengo yako.

China wamefanikiwa sana kwenye masuala ya EXPORT yaani viongozi wao wanacho angalia ni ulipe kodi tuu stahiki, kuhusu viwango hayo mambo hawataki hata kujua, ndo maana bidhaa zao nyingi hafifu lakini wana support ya serikali yao.

Kwenye suala la EXPORT serikali inabidi iregeza baadhi ya sheria zake zisizo na tija ili kuruhusu vitu vingi viuzwe nje na hapo ndo itapata pesa nyingi za kigeni, hii issue ya viwango sio kila soko huko nje wanaangalia viwango vya kimataifa.




***
 
Laiti ungepitia sheria za asali ndo ungejua ni kitu chenye masharti mengi kiasi kwamba kama mjasiriamali ni vigumu kuweza kustahimili,

Mpaka uwe na mtaji mkubwa ndo unaweza fanya biashara hii ya asali
Nina mashaka sana na hii bidhaa maana ingekuwa na soko ingekuwa vurugu sana ila sasa mpaka mtu unasahau kuwa kuna zao linaitwa asali

***
 
Mie sijaelewa bado hii habari ya baadhi ya viongozi wetu wanatuekea mazingira magumu wajasiriamali kiasi kwamba ili ufanikiwe inabidi utumie njia za panya nyingi ama ukisema ufate process zao basi tegemea anguko tuu katika malengo yako.

China wamefanikiwa sana kwenye masuala ya EXPORT yaani viongozi wao wanacho angalia ni ulipe kodi tuu stahiki, kuhusu viwango hayo mambo hawataki hata kujua, ndo maana bidhaa zao nyingi hafifu lakini wana support ya serikali yao.

Kwenye suala la EXPORT serikali inabidi iregeza baadhi ya sheria zake zisizo na tija ili kuruhusu vitu vingi viuzwe nje na hapo ndo itapata pesa nyingi za kigeni, hii issue ya viwango sio kila soko huko nje wanaangalia viwango vya kimataifa.




***


Wako sahihi kwenye kudhibiti viwango maana itaharibia reputation nchi yetu. Kwa kudhibiti viwango ndio hata asali ya nchi yetu inaheshimiwa
 
Kwa upande mwingine upo sahihi sanaa, lakini Tufumbe macho tuu kwa vitu vingine tuwaige china tukipata pesa tutakua na mtaji mkubwa then tutaweka viwango wanavyotaka,

Ama serikali ingesimamia hilo suala naamini tungeingiza pesa nyingi sanaa
Wako sahihi kwenye kudhibiti viwango maana itaharibia reputation nchi yetu. Kwa kudhibiti viwango ndio hata asali ya nchi yetu inaheshimiwa

***
 
Kwa hiyo watu wa Rwanda ndio wateja wakubwa? Kwa nini Kenya ambako ndio kuna uchangamkiaji mkubwa wa fursa wao wakenya wasijae kuja kununua hapa nchini?
Kwa kukusaidia Tanzania ndio mzalishaji mkubwa wa Asali eneo hili kutokana na Jiografia yake lakini Jiulize inapitwa na Nchi zote za Kenya, Uganda na Rwanda kwenye Export ya Asali.

Swali wanaipata wapi Asali? Ni hii ya kwetu inaenda kwa mandoo na gallons kwasababu kwetu kuexport ni dhambi kwa mamlaka


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

45 Reactions
Reply
Back
Top Bottom