Moja kwa moja kwenye mada.
Ni kwa maslahi ya taifa hili na kwetu sote kuona kuwa covid-19 inadhibitiwa au hata kuuondoshwa kabisa nchini.
Huu ugonjwa ni hatari na kwa bahati mbaya zaidi, hauwezi kuondoka wenyewe pasipo na jitihada za kutosha kutoka kwetu na hasa serikali.
Duniani kote hata magaidi wasiokuwa na huruma wamelazimika kusitisha harakati zao zote katika kipindi hiki. Pia hata ambako vita vilikuwa vikirindima, silaha kwa sasa zimewekwa chini kuipa nafasi vita dhidi ya Corona kupiganwa kwanza vilivyo.
Ni kwa kutambua umuhimu huo, zimekuwapo jitihada mbali mbali za dhati tokea kwa wadau mbalimbali tangia awali mno, zenye mikakati iliyokuwa wazi ili kuona:
1. Corona haingii nchini, wakati ilipokuwa bado haijaingia nchini:
Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums
(Uzi wa March 14 kabla ya Corona kuingia nchini)
2. Corona haisambai pale ilipokuwa imeingia tokea siku alipopatikana mgonjwa wa kwanza hapa nchini:
Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums
(Uzi wa March 20 baada ya Corona kuingia nchini March 16).
Jitihada zote (kama hizo) zimekuwa kila wakati na mikakati ambayo kwa #1 ufanisi wake ungepimwa kwa kuona ugonjwa hauingii nchini.
Wakati jitihada za #2 hapo juu ilipaswa kupimwa kwa kuona ugonjwa hausambai.
Mikakati iliyokuwa hapo, kwa #1 na #2 haikupewa umuhimu wowote na serikali. Serikali iliamua kufanya yake kwa namna yake.
Matokeo yake ugonjwa ukaingia na bado unaendelea kusambaa kwa kasi:
Kwenu: Ummy, Taskforces, mabibi na mabwana katika mapambano ya dhati dhidi ya Corona - JamiiForums
Kwa maana kamili kuwa mikakati waliyoamua wao kama serikali kuichukua, ilishindwa kutusaidia kuzuia ugonjwa kuingia na hata imeshindwa kutusaidia kuzuia ugonjwa huu kusambaa:
Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO! - JamiiForums
Hata hapa tulipo imekuwa ikipendekezwa kuwapo kwa mwelekeo tofauti bila mafanikio huku maambukizi yakizidi kusambaa zaidi.
Umuhimu wa kuwa na mikakati mingine japo tukiwa tayari tumechelewa mno unazidi kukua zaidi na zaidi. Ni muhimu sana kwa kigugumizi kilichopo serikalini kuweza kuangaziwa vilivyo.
Hii ya maombezi, dawa za kienyeji na sasa dawa zisizothibitishwa tokea kokote kule, si uchaguzi unaotushawishi sote kama suluhu ya tatizo hili la kisayansi dhidi ya mausia yote tokea WHO na hata marafiki zetu.
Kwa mujibu wa Raila Odinga:
"Viongozi wa kanda wamekuwa wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio."
Kwa mujibu wa Cyril Ramaphosa:
"Jitihada zote za kumtaka mwenyekiti wa nchi za SADC kuitisha mkutano wa video baina ya wakuu wa nchi hizi kujadili masuala ya Corona zimegonga mwamba".
Kwa mujibu wa Kaguta Museveni:
"Alikuwa na mazungumzo marefu kuhusiana na suala la Corona na marais Kagame, Magufuli na Kenyatta. Katika wote, walikuwa na makubaliano mazuri isipokuwa kwa Dr. Magufuli."
Si sahihi kuendelea hivi wakati watu wanakufa na mkakati wa kuudhibiti huu ugonjwa vilivyo haupo:
Rais Magufuli kuhusiana na Corona bora ukachukua hatua bila kuchelewa zaidi unauweka uongozi wako njia panda - JamiiForums
Ni katika kutafuta uwezekano zaidi wa usalama wetu sote, mchango wa marais wetu wastaafu katika kushauriana, hauwezi kudunishwa (labda na misukule tu):
Waraka wa wazi kwa Marais wetu Wastaafu kuhusiana na hali ya Corona nchini - JamiiForums
Ni wazi kuwa tunaendelea kuishiwa mawazo kwani jitihada zote zilizokwishafanywa zimeaangukia kwenye masikio viziwi.
Ninawasilisha, Itifaki yote ikiwa imezingatiwa na hasa kwa kuutambua uwepo wote wa misukule.
Ukweli usiopingika, kwa mwendo huu tunakoelekea tunazidi kuishiwa mawazo.