ARV bandia - Udhaifu wa Serikali wazidi kudhihirika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ARV bandia - Udhaifu wa Serikali wazidi kudhihirika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Oct 12, 2012.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Serikali kupitia MSD wamesimamisha usambazaji wa dawa zote zilizo katika maghala ya TPI na MSD ambazo zimetegenezwa na TPI

  Akiongelea sakata hilo Waziri mwinyi alisema “Tumeona tuchukue hatua kutokana na uzembe wa watendaji wa MSD. Lakini pia kusitisha uzalishaji wa TPI pamoja na usambazaji wa dawa zote zilizokwisha kutengenezwa na kiwanda hicho hadi uchunguzi utakapokamilika,” alisema Dk. Mwinyi.

  Alisema tayari makopo 9,570 ya dawa hiyo, yamekamatwa na kuondolewa kutoka katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya na kurudishwa MSD.

  Udhaifu wa Serikali
  Moja, Dunia nzima watu wanaotengeneza fake products hujaribu kutumia jina na product inayokubalika, inayoaminika kutoka kwa manufacturer anayetambulika, mfano mtu anatengeneza simu fake afu anaita nokia wakati haijatengenezwa na nokia (inakua sio nokia, isipokua mtu mbaya katengeneza simu yake anataka watu wandhanie ni nokia, mara nyingi ni kwa sababu nokia inakua imeishaaminika sokoni)

  TPI wanatengeneza tu ARV hawasambazi, wakishakutengeneza wanazipeleka MSD ambao huzihakiki na kuzisambaza, pia tukumbuke MSD hupata dawa kutoka sehemu nyingine nyingi sio TPI tu, ARV fake iliyosambazwa imeandikwa imetengenezwa na TPI, lakini TPI wamekanusha wao kutengeneza dawa fake lakini pia common sense inagoma kwamba TPI watatengeneza fake ya dawa yao, kwamba ukiona nokia fake basi unaenda kufunga kiwanda cha nokia, kwamba unaamini wao ndio waliotengeneza hiyo fake.

  Mbili, Kama kawaida kitu cha kwanza alichosema waziri mwinyi ni kile ambacho wote tulitegemea, hii nd style yao, wanategemea kufanya uchunguzi, kwa hiyo tutegemee tume au kamati kama wanavoita siku hizi (baada ya mvutano wa kikatiba/kisheria).

  Tatizo kubwa na la msingi, Waziri mwinyi anasema wamekwishakamata makopo 9,570 ya hizo dawa fake, kama ni mimi nahitaji siku moja tu kukwambia hizo dawa zimetengenezwa wapi, waziri mwinyi anahitaji uchunguzi

  Ni rahisi kujua zimetengenezwa na nani, pale zilipokamatwa, wahusika waseme wamezitoa wapi (kwa kuonesha vielelezo), bila shaka MSD kwa sababu wao ndio wasambazaji pekee wa ARVs, MSD waseme wamezitoa wapi (kwa kuonesha vielelezo) unarudi nyuma hadi kufika kwa mtengenezaji, hakukua na haja ya 'kukurupuka' kuzuia dawa zote za TPI, hata common sense inasema tofauti, common sense inasema dawa hizi fake haziwezi kuwa zimetengenezwa TPI, kwa hili TPI ni victim na kamwe hawezi mshutumiwa, inakuwaje waziri mwinyi na serikali yake wanafikiri TPI wanaweza kufake dawa yao wenyewe is beyond me.


  Tatu; Jukumu la kuhakikisha vitu fake havifiki kwa walaji ni la serikali, kwamba hii dawa fake imekuwepo sokoni inatuambia mambo mengi kuhusu serikali yetu (bila kujali nani katengeneza na nani kasambaza) , inatukumbusha kauli ya John mnyika kwa serikali hii ni DHAIFU! kama kawaida yao, wameshajiweka pembeni, wameshatoa watu kafara na maisha yanaedelea
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye "TATU". SERIKALI IWAJIBIKE: hivi ni nani asiyejua kuwa waziri mwinyi hawezi kufanya kazi?, kila wizara anayo host inakuwa na mambo ya ajabuajabu: tazama. Wizara ya ulinzi- mabomu ya kambi za jeshi, upotevu wa fedha nyingi na ndege ya jeshi ya jeshi kuodishwa kwa watalii wa kigeni. Inafurahisha zaidi kuwa inasemekana kuwa anaandaliwa kuwa RAIS, tusubiri, huenda kwa hili atajipima na kuchukua uamuzi sahihi.
   
 3. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,317
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu USWE, kabla ya kupost hapa ilitakiwa uulize kwanza maana ya huo u-fake ni nini, TPI wanatengeneza dawa feki kwa kutoweka aina fulani ya dawa katika mchanganyiko unaotakiwa kuwa na dawa tatu, Nevirapine,lamivudine na Stavudine, wao wameweka mchanganyiko wa dawa mbili katika kila kidonge(hii inafanyika makusudi ili kupunguza gharama ya dawa ya tatu) mfano rahisi ni kama wewe unatengeneza mkate unaambiwa uwe na UNGA, MAYAI na MAFUTA, then wewe unaweka UNGA NA MAFUTA tuu unakwepa gharama ya mayai ndicho walichofanya TPI.

  Cha pili huwezi kusema TPI wanashutumiwa bure eti MSD waseme walizitoa wapi hizo dawa, kwa taarifa yako tuu uchunguzi uliofanyika katika bohari za MSD unaonesha hakuna sehemu nyingine inapotoka hiyo dawa na MSD hainunui mtaani, dawa hizo huwa zinapelekwa MSD na malori ya TPI wenyewe.
   
 4. awp

  awp JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nchi yangu Tanzania inakwenda wapi? kwanini wenye vitambi wanataka kuua walalahoi?
   
 5. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Serikali dhaifu! rais dhaifu! wabunge wa CCM dhaifu! majaji vilaza dhaifu! tusitegemee miujiza.
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kwamba dawa hizo huwa zinapelekwa MSD, sasa inapotekea dawa zilizopelekwa MSD tunazikuta hospitali, tena tunaambiwa ni fake, nani wa kuwajibika?

  kabla hatujajua walizitoa wapi, (ninaamini hazijatoka TPI), ilikuwaje MSD wakasambaza dawa fake?
   
Loading...