Arusha: Yaliyojiri kutoka mahakamani Arusha, dhamana ya Mbunge Lema yashindikana

Baada ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali maombi ya mawakili wa Lema ya kufanya marejeo ya hukumu ya dhamana. Na Mawakili wa Lema kukata Rufaa kwa hati ya dharura kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena kuanzia leo siku ya jumatatu Mbele ya Jaji Massengi, Jaji Mwandamizi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.


Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.


Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.

Taarifa ambazo tumezipata Mbunge Godbless Lema atafikishwa ndani eneo la mahakama kuanzia saa tatu asubuhi.
Ulinzi umeimarishwa sana
Maskari waliovaa kininja na silaha za kali za moto wametapakaa kila sehemu.
View attachment 440540 View attachment 440541
View attachment 440543
=============
Mbunge Godbless Lema ameshafikishwa katika viwanja vya mahakamani.
Mbunge Godbless Lema atapandishwa kizimbani majira ya saa sita
Kwa ulinzi huo ninaoona katika picha Namuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa.
Wanaoweka ulinzi kama huu sidhani kama wanaeleewa a long term impact yake.
Kuonyesha silaha kali hadharani kwa kesi ambayo hata kwa virungu tu pangekuwa na utulivu ni ku sensitize watu na mwisho watakuwa hawaogopi.
Social scientist wa majeshi yetu mnafanya kazi gani?
 
Kuna wakati ni muhimu kwa askari Kuficha ID zao endapo wapo na kesi yenye Maslahi na Ugaidi Ama Vibginevyo. Sioni Shida ...tayari Umeambiwa Hao wapo mahakamani Kwa Kesi ya Walipuaji mabomu.
Kama kesi ya ugaidi ni Sawa lkn sio kumpeleka Lema mahakamani ndio uvae vile.
 
CCM wangekuwa na mtazamo wa mbali wangebadilisha Jina la chama Cha Masela.
Wakaita majina mengine, maana naona kama chama Chao kitapata nuksi sana
 
Huu uvaaji hauko sahihi,sio sare za jeshi,wanaovaa vile ni watu wasiotaka watambuliwe kwa maana wana nia ovu, kwa tafsiri jinsi alivyovaa ni kwamba wako kwa jambo baya. Askari anatakiwa avae vizuri na abandike no yake ya kazi na Jina kifuani upande wa kushoto ili mwananchi amtambue, kwa sura, namba yake ya kazi na Jina pia,huu ni uhuni.
Ni askari wa CCM ambao hawataki kutambuliwa. Au labda mlenga shabaha anapotezea
 
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro ,Mbunge wa Jimbo la Monduli Julias Kalanga wameshawasili tayari mahakamani .
Jaji bado hajafika.
IMG-20161128-WA0258.jpg
 
Back
Top Bottom