Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Wengine tunashindwa kuchangia mada za humu sababu wachangiaji wanachangia kwa mihemuko ya kisiasa.
Mimi ni mtaalamu wa kodi. Ngoja nikupe darasa kidogo kama utaweza kunivumilia kuandika kidogokidogo.
Charitable
Hilo darasa hamna asiye jua umuhimu wa kodi nchi hii, pia hiyo hiyo taasisi inaweza kuwa fimbo kuonea watu.
 
Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu, ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
...Ni kweli Mkuu. Hata kwa kuangalia hizo picha zao tu hapo. Hapana Mzazi Masikini hapo, kwa maana halisi ya neno ' Masikini'.
Wanaitumia tu hiyo Fursa ya kusomeshewa watoto, ambayo Luna wanaoistahili kweli.!

Kama ni suala LA kuandama basi walitakiwa kuandamana dhidi ya Viongozi wa Shule kwa nini hawajalipa Kodi inayotakiwa had I wanasabisha akaunti ya Shule kuwa freezed.
Hawapaswi kuandama dhidi ya TRA ambao wanafanya Wajibu wao...
 
Kama mnavyoona kwenye mitandao ya wassap, TRA inefreeze account za shule za St. Jude kwa kisingizio kuwa wamekuwa hawalipi kodi wakati wanasomesha watoto wa Kitanzania bure kabisa kwani Gharama zote na Mishahara ya Walimu imekiwa ikilipwa na serikali ya Austria kama ufadhili. Chanzo cha kazi hii ni kwamba wakati wa kampeni serikali ya mkoa na wilaya iliiomba shule itoe magari ili waweze kusomba wapambe wake lakini shule ikasema wao lama NGO hawaruhusiwili kisheria kuegemea chama chochote cha siasa..Sasa kwa kuwa kijani wako madarakani wameamua kuanza nal kuwa wanakwepa kodi hivyo shule ifilisiwe na watoto elf 1 inabidi warudi kwao nawafanyakazi zaidi ya 300 kukoswa ajira.Je TRA kwa hili anafanya haki.?je wanmkomoa nani?
 
Kama mnavyoona kwenye mitandao ya wassap, TRA inefreeze account za shule za st Jude kwa kisingizio kuwa wamekuwa hawalipi kodi wakati wanasomesah watoti wa Kitanzania bure kabisa kwani Gharama zote na Mishahara ya Walimu imekiwa ikilipwa na serikali ya Austria kama ufadhili.Chanzo cha kazi hii nikwamba wakati wa kampeni serikali ya mkoa na wilaya iliiomba shule itoe magari ili waweze kusomba wapambe wake lakini shule ikasema wao lama NGO hawaruhusiwili kisheria kuegemea chama chochote cha siasa..Sasa kwa kuwa kijani wako madarakani wameamua kuanza nal kuwa wanakwepa kodi hivyo shule ifilisiwe na watoto elf 1 inabidi warudi kwao nawafanyakazi zaidi ya 300 kukoswa ajira.Je TRA kwa hili anafanya haki.?je wanmkomoa nani?
Wewe sema ukweli kwamba walifanya makosa ya kutofuata sheria acha kukurupuka hadi unakosea.
Ona sasa kichwa cha habari umeandika nini🤣🤣
 
Hiyo shule haiwezi kusajiliwa kama charitable Organisation sababu haina sifa za kuwa charitable. Hivi shishi food ya Shilole inauza chakula kwa rate za market value, halafu atokee Mo Dewji aseme naomba uwe unawalisha kituo cha watoto maskini na wasiojiweza halafu Mo dewji anakulipa kwa rate ileile unayowachaji watu wengine, utasema shishi food inafanya charity?
Mfano mzuri Sana. Watu hawaelewi hili
 
Angekuwa Lema ndio mbunge wao ningesema ni siasa wanaleta ila Lema hayupo yupo Mrisho Gambo,Hapo ni serikali imeamua kufanya ivyo kwaiyo wananchi muwe wapole tu
 
Mlipoambiwa na lisu kwamba mfumo wa kodi umekaa kiharamia mlidhani anaota!?
 
Wazazi Maskini zaidi ya 2000 ambao watoto wao wanafadhiliwa kimasomo katika shule ya St. Jude iliyopo Arumeru Mkoa wa Arusha, wameandamana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakitaka shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ifunguliwe ili Watoto wao waliosimamishwa masomo kwa zaidi ya wiki mbili waweze kuendelea na masomo.

Wazazi hao wamedai kwamba mamlaka ya mapato Tanzania TRA imekausha akaunti yao kwa kuchota fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwa madai kwamba shule hiyo haijalipa kodi ya Serikali kwa muda mrefu na hivyo uongozi wa shule hiyo kulazimika kuwasimamisha masomo Wanafunzi kwa kushindwa kujiendesha baada ya fedha zilizopo kwenye akaunti kuchukuliwa na TRA.

====

Arusha. Wazazi zaidi ya 1,000 wa wanafunzi wanaopatiwa ufadhili wa masomo katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya St. Jude iliyopo Arumeru mkoani Arusha, wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kulalamikia hatua ya watoto wao kusitishiwa masomo kinyume na utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba mosi, 2020 wazazi hao waliituhumu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani hapa kufungia akaunti za mfadhili wao, jambo lililosababisha shule kushindwa kujiendesha ikiwemo kuwahudumia watoto.

Salma Mohamed na Latifa Jafari, wakazi wa jijini hapa wamesema katika kipindi cha wiki mbili watoto wao wamesimamishwa masomo kwa madai shule inadaiwa, hivyo kuiomba Serikali kuwaruhusu kuendelea na masomo.

Wazazi hao pia wanaituhumu TRA kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti ya shule na kusababisha kushindwa kujiendesha.

Akizungumzia tuhuma hizo, meneja wa TRA mkoa wa Arusha, John Mwigura alikiri kuidai kodi ya muda mrefu shule hiyo, lakini St Jude ilikataa deni hilo kwa madai haifanyi biashara, hivyo haiwezi kulipa kodi na kukimbilia ngazi mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Rufaa kupinga tuzo la kodi akibainisha kuwa mahakamani TRA ilishinda kesi hiyo na St Jude iliamuliwa kulipa kodi hiyo.

View attachment 1638958View attachment 1638959
Hawa ndio wazazi Maskini waofadhiliwa?


No products in the cart.

Menu


Gemma-Winrose-Banner-Overview.png

Supporter Accountability​

We are committed to providing high standards of accountability to our sponsors and donors​

Every year, The School of St Jude is independently audited in accordance with International Financial Reporting Standards (IFRS). Our 2016 audit was conducted by Ernst & Young, one of the world’s largest and most trusted international auditing firms. Our Australian fundraising partner is also now known as The School of St Jude and is responsible for all funds raised in Australia. All donations made to our Australian partner are made available to The School of St Jude in Tanzania.
  • The School of St Jude Australia board monitors school finances on a monthly basis.
  • Two of The School of St Jude Australia board members sit on The School of St Jude Board in Tanzania, an entity that has statutory governance over the management of the school.
  • In Australia, The School of St Jude Limited is audited annually by Roberts & Morrow, Armidale.
  • More than 98.5 cents in every Australian dollar raised is directed towards The School of St Jude.
The School of St Jude strongly believes in accountability and has put in place safeguards to prevent money ending up in the wrong hands. Theses controls are constantly being reviewed and improved in line with best practice.
As per our Memorandum of Understanding, The School of St Jude in Tanzania and The School of St Jude Australia share mutual responsibility to:
  • Ensure that, where applicable, donated funds are expended on behalf of donors in an efficient and cost effective manner and for the purpose for which such funds were donated. The funds are to be used for development purposes and never for evangelical or partisan political activities.
  • Plan for the long term financial stability of the school so that its continued growth and sustainability are assured for future generations of students; to this end the Future Fund was established in 2016, to underwrite the long term future of the school.
  • Carry out the function for which the school was established, that is, solely for the relief of poverty through the provision of education for the children of Tanzania.
We are always happy to respond to any questions or requests for information from supporters.
Simply, contact us with your queries
 
Nilikuwepo kwenye hyo misa
Vicar General alisema shule inategemea mapato yake kutoka kw wafadhili wa Australia. Na hakuna mwanafunzi anaelipa ada, ni kwa ajili tu ya kusaidia watoto wanaotoka familia za kipato cha chini
Asa sijui kwa nn hadi misaada inatozwa kodi, wakati hamna faida wanayopata
Hapa kuna school fees ambayo inalipwa na wafadhili au mfadhili, hivyo hiyo school fees inayolipwa na mfadhili ni mapato kwa Shule
 
Angalia Fanya tafiti hata Magari yao yanapack wapi hapa mjini kama siyo st Theresa Cathedral usibishe usiyojua.
Kwa hiyo yale Magari yanayo park St Joseph Cathedral Dsm ni ya Kanisa Katoliki?? Au Magari yanayo park ksnisa la kilutheri hapo Arusha mjini ni ya Kanisa
 
Hilo darasa hamna asiye jua umuhimu wa kodi nchi hii, pia hiyo hiyo taasisi inaweza kuwa fimbo kuonea watu.
Sasa wewe umepewa mpaka kesi ya 2012 , lakini wewe na akili yako bado unashadadia siasa za Mwaka huu
 
Sasa wewe umepewa mpaka kesi ya 2012 , lakini wewe na akili yako bado unashadadia siasa za Mwaka huu
Mimi nasema jinsi issue ya siasa ilivochochea kukomoana, tena juzi tu before uchaguzi ilikuwa Moto sasa imetoka juzi hii.
 
Back
Top Bottom