Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wazazi Maskini zaidi ya 2000 ambao watoto wao wanafadhiliwa kimasomo katika shule ya St. Jude iliyopo Arumeru Mkoa wa Arusha, wameandamana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakitaka shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ifunguliwe ili Watoto wao waliosimamishwa masomo kwa zaidi ya wiki mbili waweze kuendelea na masomo.

Wazazi hao wamedai kwamba mamlaka ya mapato Tanzania TRA imekausha akaunti yao kwa kuchota fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwa madai kwamba shule hiyo haijalipa kodi ya Serikali kwa muda mrefu na hivyo uongozi wa shule hiyo kulazimika kuwasimamisha masomo Wanafunzi kwa kushindwa kujiendesha baada ya fedha zilizopo kwenye akaunti kuchukuliwa na TRA.

====

Arusha. Wazazi zaidi ya 1,000 wa wanafunzi wanaopatiwa ufadhili wa masomo katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya St. Jude iliyopo Arumeru mkoani Arusha, wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kulalamikia hatua ya watoto wao kusitishiwa masomo kinyume na utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba mosi, 2020 wazazi hao waliituhumu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani hapa kufungia akaunti za mfadhili wao, jambo lililosababisha shule kushindwa kujiendesha ikiwemo kuwahudumia watoto.

Salma Mohamed na Latifa Jafari, wakazi wa jijini hapa wamesema katika kipindi cha wiki mbili watoto wao wamesimamishwa masomo kwa madai shule inadaiwa, hivyo kuiomba Serikali kuwaruhusu kuendelea na masomo.

Wazazi hao pia wanaituhumu TRA kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti ya shule na kusababisha kushindwa kujiendesha.

Akizungumzia tuhuma hizo, meneja wa TRA mkoa wa Arusha, John Mwigura alikiri kuidai kodi ya muda mrefu shule hiyo, lakini St Jude ilikataa deni hilo kwa madai haifanyi biashara, hivyo haiwezi kulipa kodi na kukimbilia ngazi mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Rufaa kupinga tuzo la kodi akibainisha kuwa mahakamani TRA ilishinda kesi hiyo na St Jude iliamuliwa kulipa kodi hiyo.

IMG_20201201_090426.jpg
IMG_20201201_090415.jpg
 

Attachments

  • THE SCHOOL OF ST. JUDE LTD VS THE COMMISSIONER VGENERAL TRA CIVIL APPEAL NO.21 OF 2018 HON.MWA...pdf
    674.1 KB · Views: 38
Hii shule ni Kama NGO inachukua watoto maskini sana, wanasomeshwa hapo mpaka form six na wengine mpaka chuo. Kama kungekua na shida Serikali ingekaa nao kwanza kujua tatizo liko wapi.tunakoelekea hali itakua tete sana.
 
Naomba kuelimishwa ndugu zangu, TRA ina mamlaka gani ya kuchukua hela kwenye akaunti ya shule bila ya kutoa taarifa kwa wahusika? Ina maana serikali ina mamlaka hadi kwenye akaunti zetu binafsi?

Mwenye kuelewa hili naomba anielimishe na mimi.
TRA wanakamata mali ikiwamo fedha taslimu kufidia wanachodai, mali zinapigwa mnada. Wahusika hutaarifiwa na wao wenyewe ndio hutoa orodha ya mali walizonazo au namba ya akaunti ya benki.
 
Naomba kuelimishwa ndugu zangu, TRA ina mamlaka gani ya kuchukua hela kwenye akaunti ya shule bila ya kutoa taarifa kwa wahusika? Ina maana serikali ina mamlaka hadi kwenye akaunti zetu binafsi?

Mwenye kuelewa hili naomba anielimishe na mimi.
Hata ya kwako wanaweza kuchukua, pesa ni ya serikali sio yako, umeazima tu.
 
Mfano mzuri
Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu.ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
Mfano mzuri picha ya hapo juu. Wazazi maskini hao kweli!!
 
Back
Top Bottom