Arusha wavuka lengo mauzo madini

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1566447429802.png

WIZARA ya Madini imekusanya zaidi ya Sh bilioni 2.7 katika kipindi cha Julai 2018 hadi Juni 30, mwaka huu na kuvuka malengo yaliyokusudiwa soko la mkoani Arusha. Mapato hayo ni kutokana na mauzo ya madini kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo na utoaji wa vibali vya kufanya biashara hiyo. Kaimu Osa Madini Mfawidhi wa Wizara ya Madini Arusha, Robert Erick amesema, malengo ya osi hiyo ilikuwa kukusanya Sh bilioni 2.5, lakini wamevuka malengo na kupata ongezeko la Sh milioni 200.

Erick amesema hiyo inatokana na wafanyabiashara wakubwa na wa kati kuongeza thamani ya madini kwa kuuza madini yaliyothaminiwa nchini. Amesema kuongeza thamani kwa madini kunaisaidia serikali kupata fedha nyingi zaidi na kunasaidia pia vijana kupata ajira kwa kuajiriwa katika osi za wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kukata madini hayo.

Osa Madini huyo aliwataka wafanyabiashara mkoani Arusha wawe na mawazo ya kununua mashine za kukata madini kwa wingi ili vijana wanufaike na ajira na wao wanufaike na serikali pia ipate haki yake. Alisema iwapo wafanyabiashara wakubwa na kati watafanya hivyo fedha nyingi zitabaki nchini kwa serikali kunufaika na wao kunufaika zaidi katika biashara hiyo.

Erick alisema kwa sasa osi yake mkoani Arusha inatoa huduma kwa wakati, vibali vya kununua na kuuza madini vinatolewa kwa wakati pia na ukiritimba katika wizara hiyo haupo kwani kila mmoja anawajibika ipasavyo kwa maslahi ya serikali.

Akizungumzia soko la biashara ya tanzanite mkoani Arusha, osa huyo alisema haijapanda na wala haijashuka liko katikati hivyo ni jitihada za wafanyabiashara wenyewe kutafuta namna ya kuipandisha biashara hiyo na kuishauri serikali nini kifanyike ili soko la madini hayo lipande zaidi katika soko la nje ya nchi.

Katibu wa Chama cha Wauzaji na Wanunuzi Wakubwa wa Madini Tanzania (TAMIDA), Benny Mtalemwa aliwataka wafanyabiashara wa madini kote nchini kuhakikisha wanafanya biashara halali ikiwamo kulipa kodi kwani serikali chini ya Raisi John Magufuli iliondoa kodi zote ambazo zilikuwa kero kwao katika biashara ya madini. Mtalemwa alisema itasikitisha kuona mfanyabiashara wa madini atadiriki kufanya biashara haramu bila leseni na kutorosha madini kwani njia ya panya kwenda nje ya nchi hilo haitavumiliwa na Tamida na hatua kali zitachukuliwa.
 
Back
Top Bottom