ARUSHA: Watu saba wapoteza maisha katika maeneo mbalimbali kutokana na mvua

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,664
4,259
Kuna taarifa kwamba jana Arusha maeneo ya Orkokolo mvua ilisababisha madhara makubwa hadi kupelekea vifo kwa raia kadhaa.

Aidha kuna familia nzima ilisombwa na maji wakiwa wametoka harusini na kusombwa wote jumla wakiwa kwenye gari. Baadhi ya miili imepatikana.

More updates to follow..
 
Mvua ya Jana ilikuwa kubwa sana . Nasikia Kuna Bwana na Bibi harus wamepoteza maisha
Hatari tupu, nasikia kifodi"hiace" imesombwa na maji na watu wakiwemo, na corrola iliyokuwa imebeba maharusi. So ni gari 2 zimesombwa na hazijaonekana bado. Na piki piki moja ikiwa na watu wawili. Hadi sasa miili minne imepatikana.
 
Aiseee tumuombe Mungu awanusuru
 
Habari wanaJF,

Watu saba wapoteza maisha katika maeneo tofauti wilayani Arumeru kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.
 
Back
Top Bottom