Arusha: Watu 11 mbaroni kwa kula njama za kufanya fujo Oktoba 28

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,008
9,873
Polisi Mkoani Arusha wamekamata watu 11 kwa makosa ya kula njama ya kufanya fujo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Salum Hamduni alisema watu hao walikamatwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha na tayari jalada lao limefikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lakini amesema hakuna vurugu kwenye mkoa huo na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku.

Pia Oktoba 28 hakukuwa na maandamano ya wapinzani mkoani humo na amehimiza wananchi waendelee na shughuli zao.
 
watwange ili wapate akili maana wanaamini maisha yao yako mikononi mwa wanasiasa kuliko hata Mungu
 
Back
Top Bottom