#COVID19 Arusha: Wananchi wajitokeza kwa wingi kupokea chanjo ya Corona

Wakuu, mm pia nmeshafanya booking ya wiki ijayo ila sipo kwenye yale makundi matatu ya muhimu kuchanjwa, je watanikubalia kuchanjwa.?
Hata mm simo kwenye hayo makundi ila nilidhamiria lazima nichanje na nimefanikiwa. Itategemea na watakaokupokea kama watakuelewa sababu kwa nn uchanje.

Wengine hawaulizi sana wanachanja bila kuangalia umri wengine wanazingua
 
Vipi umepewa cheti? Ninapenda kuchua iwapo cheti kinachotolewa kina namba ya kichupa ambacho mtu kachanjwa?
Ukipata chanjo yoyote inatakiwa kumbukumbu ziingizwe kwenye yellow book. Tz hili linafanywa kwa watu wanaosafiri kwenda nje pekee, nadhani corona italazimika iingie humu kwani ni gonjwa la dunia.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hata mm simo kwenye hayo makundi ila nilidhamiria lazima nichanje na nimefanikiwa. Itategea na watakaokupokea kama watakuelewa sababu kwa nn uchanje.

Wengine haulizia sana wanachanja bila kuangalia umri wengine wanazingua

Jamaa zangu wengi Dar hawamo kwenye hayo makundi tayari wamepata chanjo kwa raha zao.

Kweli Tanzania ni Dar.

Mtori umedoda hapa tunapambana na subira, tunaambiwa nyama ziko chini.
 
Wapi wamejitokeza kwa wingi kama si propaganda za kuhamasisha kuchanjwa chanjo inayotiliwa mashaka duniani kote? Watu watachanja lakini si kwa kasi ya harakaharaka hivyo. Wanasubiria kuona madhara kwa waliotangulia kuchanjwa ndio na wao wakachanjwe
Hata yangekuwepo madhara, wewe umeifanyia nn nchi yako mpaka sasa??
 
Ukipata chanjo yoyote inatakiwa kumbukumbu ziingizwe kwenye yellow book. Tz hili linafanywa kwa watu wanaosafiri kwenda nje pekee, nadhani corona italazimika iingie humu kwani ni gonjwa la dunia.
Covid ni kitu kingine mkuu, hii kitu si Yellow book ya TZ bali unaingia kwenye database ya dunia iliyopo pale Washington, kuwa huyu ni mtu wetu mwaminifu anayekubali.
 
Covid ni kitu kingine mkuu, hii kitu si Yellow book ya TZ bali unaingia kwenye database ya dunia iliyopo pale Washington, kuwa huyu ni mtu wetu mwaminifu anayekubali.
Yellow book ni international mkuu. Yellow book ni rafiki yake na passport.
Hata chanjo ya corona inarecordiwa humo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Zoezi la kuzindua chanjo kwa mkoa wa Arusha hatimaye limefanyika na wananchi kadhaa kuhudhuria tukio hilo lililofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa ikiwepo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na viongozi wa dini limeshuhudiwa wananchi walijitokeza kwa wingi na hatimaye chanjo hiyo kuisha kwa kituo hicho.

Hapa ni baadhi ya picha wakati wa uzinduzi huo.

View attachment 1878446
Mh. John Mongera akiongea na Viongozi na wananchi walijitokeza kupata chanjo, hawapo pichani.

View attachment 1878448
Viongozi na wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa akiongea na hadhara kabla uzinduzi wa chanjo hiyo ya uviko.

View attachment 1878445




Aisee, first nikazani wachadema ndiyo wapinga chanjo. Kumbe wafuasi wa magufuri!!!! 😂😂
 
Hamna kitu kama hicho mkuu.

Yaani kinachofanyika wakati unachomwa sindano ya malaria ndicho hicho kinafanyika kwenye covid.

Tofauti ni moja, hii ya Covid19 inanyonywa yote kwenye kichupa na ukipenda unaweza kukiiba kichupa ukaondoka nacho.
Hicho kichupa mpaka ukidokoe, kwani wanakizuia kisifike mtaani?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom