Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Vituo vya polisi 13, maduka ya JWTZ na hospitaliza serikali wamekatiwa umeme Arusha jana kutokana na kudaiwa madeni na Tanesco, hii ni kutekeleza agizo alilolitoa Rais Magufuli Baadhi ya vituo waliokatiwa umeme ni kwa Central Police, kwa RPC na Trafiki.
Tanesco Arusha wanadai bilioni 8 kwa jumla na 28% ni taasisi za serikali.
=====
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limekata huduma hiyo ya nishati kwa majeshi ya ulinzi na usalama Mkoani Arusha pamoja na hospitali zote za Serikali, ikiwemo ya Mkoa wa Mount Meru kutokana na malimbikizo ya madeni ya Ankara za umeme za zaidi ya sh bilioni 1.4.
Taasisi zilizokatiwa umeme na kiasi wanachodaiwa ni pamoja na Jeshi la Wananchi 'TPDF' (Sh Milioni 538), Makao Makuu ya Polisi Mkoa na vituo vyao (Sh Milioni 271), Jeshi la Kujenga Taifa, JKT-Oljoro, (Sh Milioni 57) na hospitali zote za Serikali (Sh Milioni 58).
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa TANESCO Mkoani Arusha, Saidy Mremi. Alisema kuwa huo ni uetekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuwakatia umeme wadaiwa sugu.
“Rais alituambia tukawakitie umeme wadaiwa sugu hata kama ni taasisi za Serikali au watu binafsi bila kuogopa na alisistiza kwa kutumia maneno haya, TANESCO tunaendelea na operesheni hii kabambe kabisa”, alisema.
Alisema jumla ya madeni sugu ni zaidi ya sh bilioni 8.6 kwa Mkoa mzima huku majeshi yakidaiwa asilimia 28 ya deni lote.
Chanzo: Kwanza Tv