Arusha: Wakuu wa Shule ambao Shule zao zimefanya vibaya kitaifa wapewa vinyago vya sokwe

Hayo mambo ya kumotisha hivyo ni ujima, ni mambo ya kizamani na hayahamasisi walimu kupata matokeo mazuri. Mwalimu anatakiwa apate mshahara mzuri na posho za kujikimu pamoja na stahiki zingine ndio atahamasika kupata matokeo mazuri, sio hivyo vichekesho
 
Kama kuna kada inajua kudharauliwa basi ni ualimu.

Wakuu wa Shule katika halmashauri ya Arusha Dc wamepewa vinyago vya nyani ili kuongeza kiwango cha ufaulu baada ya shule zao kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha 2, cha 4 na cha 6 mwaka jana.

Hii imekaaje kitaalamu?

Hii inaonesha jinsi tusivyojitambua na kuutambua utu wetu, watu wote waliopo kwenye picha wanaonekana kulifurahia jambo hilo bila kuelewa madhara yake! Hii ndiyo hali halisi kuwa mtanzania anaweza kutawaliwa vyovyote vile na akawa kainamisha kichwa kama kondoo!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom