ARUSHA: Wakili wa Serikali aomba muda kuruhusiwa kujibu viapo vya ziada katika kesi ya kupinga sheria za huduma za habari

w0rM

Member
May 3, 2011
46
150
Kesi Namba 2 ya Mwaka 2017 katika mahakama ya Afrika Mashariki, ya kupinga Sheria ya Huduma za Habari, ya Mwaka 2016 Kati ya Baraza la Habari Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyokuwa isikilizwe leo tarehe 10.09.2018 imeahirishwa

Ni baada ya Mwanasheria wa Serikali kuomba aruhusiwe kujibu viapo vya ziada vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Waleta maombi.

Mahakama imemruhusu mwanasheria wa serikali kujibu viapo hivyo ndani ya siku 14 kuanzia leo...Upande wa waleta maombi pia watapata fursa ya kujibu siku 14 baada ya serikali kuleta majibu yao..

Kesi hiyo itapangwa kusikilizwa siku na tarehe ambayo wahusika wa kesi watajulishwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom