Arusha wakanusha ufisadi kwenye uzinduzi wa Jiji

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Imeandikwa na na Veronica Mheta, Arusha | HabariLeo | Novemba 18, 2012

HALMASHAURI Jiji la Arusha imekanusha kufanya ufisadi katika sherehe za uzinduzi wa Jiji hilo uliofanyika Novemba mosi mwaka huu. Halmashauri hiyo imesema kwamba ilitumia Sh milioni 86 na si Sh milioni 100 kama ilivyodaiwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Omary Mkombole akiongea na waandishi wa habari juu ya tuhuma za Jiji hilo kutumia zaidi ya milioni 100 kwa ajili ya uzinduzi wa Jiji uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, alisema gharama za sherehe za uzinduzi wa Jiji hilo zilikubaliwa na Baraza la Madiwani.

Alisema shughuli hizo zilifanywa na kamati zilizoundwa kutoka wajumbe wa vyama mbalimbali ambao walipewa majukumu kufanikisha zoezi hilo na kusisitiza kuwa hakuna fedha zilizoliwa.

Alisema fedha hizo walizipata kutoka Mamlaka ya Maji Taka (AUWASA) ambao walichangia Sh milioni 18 kwa ajili ya ukarabati wa eneo la Mnara wa Azimio la Arusha ambao Jiji ndiko lilikozinduliwa.

Alisema fedha nyingine walizipata kwa Kampuni ya Jiangxi-Geo Engeneering ambayo inajenga barabara za katikati ya Jiji na ilitoa Sh 12,000,000 kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi na uboreshaji wa miundombinu na Kampuni ya China Railway Seventh Group ilitoa kiasi cha Sh 4,000,000 na kusema kuwa wadau wote hao watatu walitoa Sh 34,156,500.

Aliongeza kuwa Kundi la Orijinal Komedi lilipewa Sh milioni 12 na Diamond Sh milioni 10 na kuongeza kuwa walikodisha zulia na si kununua kama ilivyodaiwa na pia njiwa walinunuliwa 12 na si 100 kama ilivyodaiwa.
 
Back
Top Bottom