Arusha: Wafuasi 12 CHADEMA wafikishwa Mahakamani kwa kumchambulia mgombea udiwani wa CCM

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau,
Wafuasi 12 Wa Chadema Leo Tarehe 6/11/2017 Wamefikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma Za Kumshambulia Mgombea Udiwani Wa CCM Kata Ya Muriet Mhesh Mbise.
mahakama.jpg

Watuhumiwa Hao Waliofikishwa Katika Mahakama Ya Mwanzo Maromboso Mkoani Arusha Ni Pamoja Na Kaimu Katibu Wa Wilaya Ya Arusha Wa Chama Hicho Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper.

Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Karibuni.

====

Wafuasi 12 wa CHADEMA wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo Maromboso leo tarehe 6.11.2017 na kusomewa makosa mawili, kosa la kwanza ni kufanya fujo ambapo inadaiwa walimfanyia fujo ndugu Juma Jumanne.

Kosa la pili shambulio la kawaida ambapo inadiwa walimshambulia mlalamikaji kwa kumpiga ngumi na sehemu mbalimbali za mwili.

Hakimu Obadia Mathias Mongi wa Mahakama ya Mwanzo Maromboso alisema Dhamana ya wafuasi hao ipo wazi kwa sharti lakuwa na wadhamini wawili na ahadi ya shilingi laki sita kwa kila mmoja.
Washtakiwa wote wametimiza sharti la dhamana

Washtakiwa wote wametakiwa kufika Mahakamani tena siku ya Alhamisi tarehe16.11.2017.
 
Mkuu umekuwa na haraka sana kwenye kuleta hii habari embu tulia, then utueleze kwa undani ueleweke
 
Wadau,
Wafuasi 12 Wa Chadema Leo Tarehe 6/11/2017 Wamefikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma Za Kumshambulia Mgombea Udiwani Wa CCM Kata Ya Muriet Mhesh Mbise.Wafuasi Wa Chadema Walifikishwa Katika Mahakama Ya Mwanzo Moromboso Akiwemo Kaimu Katibu Wa Wilaya Ya Arusha Wa Chama Hicho.
Karibuni.
NB: Moderator Na Wafau Wote JF Samahani Heading Ilitakiwa Iwe Wafuasi Wa Chadema Na Sio Madiwani.
Boniphace, ujumbe umetufikia, lakini mbona umetuma mifupa tu
Ebu funguka,Hao wafuasi wa Wapi!
Ilikuaje wakamshambulia Diwani wa ccm!
Walimshambulia kwa maneno au kwa kipigo!
(lai yangu)
Sijashabikii wala sipendelei siasa za fujo au vurugu
Siasa ni hoja, technical, na maendeleo
Mahakama intede haki bila upendeleo.
Siasa oyee
 
wafuasi+pic.jpg


Arusha. Wafuasi 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa mahakamani.

Washtakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha.

Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper.

Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili.


Chanzo:
Mwananchi
 
wafungwe miaka kumi kumi inawatosha, badala wakatafute ugali wao wanaenda kupigana!
 
Sitashangaa nikisikia kuwa kimsingi MCC ndo waliolianzisha wakachapwa na kuweka mpira kwapani na kutimkia kwa Pilato!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom