ARUSHA: Wafanyabiashara maarufu waliofyatuliana risasi wapanda kizimbani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mahakama ya hakimu Mkazi Arusha imewasomea maelezo ya awali washtakiwa Philemon Mollel(Monaban)63,ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na mwenzake Baraka Taitas Mollel(43)wanaokabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya Silaha.

Akisoma maelezo hayo Leo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Salome Mshasha,mwendesha mashtaka wa Serikali,Blandina Msawa alidai kuwa upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi sita na vielelezo 16.

Alidai mahakamani hapo kuwa mnamo Mei, 18 mwaka huu Mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo namba 80/2021 , Philemon katika eneo la kituo Cha mafuta Cha Saiteru kilichopo Ngulelo wilaya ya Arumeru,alifyatua risasi kwa kumwelekezea mshtakiwa wa pili (Baraka) ambaye naye alijibu mapigo Kwa kufyatua risasi hewani.

Alisema tukio hilo lilisababisha taharuki na hofu Kwa Jamii na wakazi wa eneo hilo,ambapo ni kinyume Cha kifungu namba 84 na 35 Cha sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2019.

Alieleza kuwa washtakiwa hao walikamatwa eneo la tukio na kupekuliwa katika maungo Yao na nyumbani kwao na kupatikana na silaha aina ya bastola na risasi.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa mshtakiwa wa kwanza Philemon mollel alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na bastola moja yenye risasi 25 ,Magazini mbili na leseni ya silaha hiyo.

Alidai kuwa mshtakiwa namba mbili Baraka mollel alikutwa na bastola moja na leseni ya silaha hiyo.

Washtakiwa hao Kwa pamoja walikana makosa na kesi imepangwa kuanza kusikilizwa Septembe 27 mwaka huu.

Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Kapimpiti Mgalula anayemtetea mshtakiwa wa kwanza na David Makata anayemtetea mshtakiwa wa pili Baraka Mollel .

Ends
 
Unanitolea silaha na mimi ninayo nikuache?? Hivi mbona vitukio kama hivi sisi hatukutanani navyo?daaa.
 
Sina uhakika kilichotokea lakini aliyeanza kufyatua ndio wa kuweka ndani labda kama kuna mengine tusiyoyajua
 
Back
Top Bottom