Arusha: Vinara waliokamatwa na gunia 15 za Mirungi wachomolewa usiku wa manane Polisi

mie nataka anzisha biashara ya juice ya mmea wa bhangiiii.
hapa nafwatilia vibali vya kupewa eneo la kulima ka hekari 500, na kuleta mashine za kusindika ili kuzalisha juice. Juce ya mmea huo wa Cha R-chuga inaaminika kupunguza magonjwa mwilini
 
Ok unaenda sambamba na mpango wangu wa kashata za Bangi
 
Kama serikalini wanaiba wao wafanye nini, tumerudi zama za chukua chako mapema
 
Inanikumbusha kesi Moja kuna dalali alimpiga mama mmoja shamba milion 60.yule dalali alijua yule mama atakwenda polisi kuripoti dalali akawahi polisi akaongea na MKUU wa kituo akamwambia atampa milion 5 .yule mama alipofika kituoni akaripoti akapewa Askari wakamkamate dalali .wakamkuta kwake wakamkamata wakampeleka kituoni .yule dalali anakaa mahabusu kuanzia asubuhi mpaka usiku anatolewa anakwenda kulala nyumbani kwake saa 11alfajiri anarudi kituoni.yule mama akiripoti anamkuta kituoni.
(Ili tukio lilitokea Senegal)
 
Duh, noma sana
 
Wafanyabiasha vinara wa dawa za kulevya aina ya Mirungi kutoka Nchini Kenya waliokamatwa na magunia 15 mei 14 mwaka huu katika Mji wa Namanga, wanadaiwa kuachiwa katika mazingira ya utata, usiku wa manane huku gari lililokuwa likisafirisha mihadarati hiyo likitoweka kituo cha polisi .

Wafanyabiashara hao{majina tunahifadhi kwa sasa} waliachiwa usiku wa mei 16 mwaka huu saa 6 usiku kwa maagizo kutoka kwa viongozi wa juu wa jeshi la polisi Arusha.

Kamanda wa polisi Arusha,Justin Masejo alipoulizwa juu ya watuhumiwa hao kuachiwa muda huo alidai kuwa polisi inatoa dhamana muda wowote kwani haina kikomo cha muda wa kutoa dhamana .

Masejo alipoulizwa kama watuhumiwa wa madawa ya kulevya kisheria wanadhamana alidai wanayo kwa mujibu wa sheria na alipoulizwa gari lililobeba madawa hayo nayo linapaswa kuachiwa katika Kituo Kikuu cha Arusha alisema litapatikana kesi itakapopelekwa mahakamani .

‘’Tunatoa dhamana muda wowote hata iwe usiku wa manane na kuachiwa kwa gari lililobeba madawa sina taarifa lakini kesi ikipelekwa mahakamani litapatikana’’ alisema Masejo

Wafanyabiashara hao walikamatwa katika mji wa Namanga na kikosi kazi cha polisi Arusha kilichokwenda kufanya kazi hiyo maalumu kwani walikamatwa majira ya saa 1.30 asubuhi wakiwa tayari wameingia Nchini kwa ajili ya kusambaza mzigo huo katika Mikoa Mitatu ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.

Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa katika gari ndogo aina ya Toyota Foresta yenye namba za Usajili KDC 922T iyokuwa ikiongoza gari kubwa{ ambalo limeachiwa} lililokuwa limebeba shehena hiyo ya Mirungi.

Habari za uhakika zilisema kuwa gari iliyobeba Mirungi iliachiwa katika kituo Kikuu cha Polisi Arusha katika mazingira ya utata ambayo sio sahihi kwa mujibu wa sheria ya kusafirisha .

Kwa mujibu wa chanzo magunia hayo mara baada ya kukamatwa yalihifadhiwa stoo ya polisi na gari ndogo inayomilikiwa na wafanyabiashara hao bado iko kituo cha polisi Kituo kikuu Arusha hadi sasa ila gari kubwa lililokuwa na mzigo huo limetoweka

Hata hivyo habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi Arusha zinasema kuwa kukamatwa kwa Wafanyabiashara hao hakukuwafurahisha baadhi ya vigogo wa jeshi hilo Arusha na Longido{majina tunayo} kwani walikuwa wakifaidika kila wiki na biashara hiyo.

Habari zaidi zilisemakuwa vigogo hao wa Polisi kwa na sasa wanahaha na kuhangaika huko na kule kuhakikisha wanawanasua Wafanyabiashara hao katika kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kupindisha ukweli kwa kusema kuwa askari waliwakamata wafanyabiashara hao Nchini Kenya kitu ambacho sio ya kweli kwani walikamatwa wakati tayari wamevuka mpaka na kuingia Nchini.

Vyanzo vya Habari viliendelea kusema kuwa kutokana na vigogo hao wa Polisi ambao mmoja wao inadaiwa yuko Mkoani hapa kwa zaidi ya miaka 15 bila kuhamishwa katika kitengo cha Operesheni kwa sasa wanawasukia ajali askari waliokwenda kuwakamata kwa madai kuwa sio eneo lao la kazi wakati askari hao kabla ya kukamata wafanyabiashara hao walilipoti Longido na kusaini lakini hawakusema wanakwenda kufanya kazi gani katika Mji wa Namanga kwa kuepuka taarifa kufuja.

Hata hivyo Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi Kituo Kikuu Arusha zilisema kuwa Wafanyabiashara hao usiku wa juzi kuamkia jana majira ya saa 3.45 usiku Wafanyabiashara walifanikiwa kudhaminiwa na jana asubihi walikaa katika ofisi ya masijala wakisikilizia hatima yao.

Baadhi ya Askari Polisi Arusha na raia wengine ambao waliomba kutotajwa majina yao walionyesha kukerwa na jinsi kesi hiyo inavyoendeshwa kwani ni kinyume kabisa cha sheria na kuna upendeleo mkubwa.

Walidai watuhumiwa wengine wa Madawa hufikishwa mahakamani haraka na kunyimwa dhamana kwa mujibu wa sheria lakini wafanyabiashara hao wanaishi rumande kama wako majumbani mwao kwani wanapata mahitaji yote ikiwemo mawasiliano ya simu hatua ambayo sio sahihi.

Askari mmoja alisema kwa mujibu wa sheria ya madawa ya kulevya iwe bangia au mirungi ukikamatwa unasafirishwa kesi hiyo haina dhamana polisi wala Mahakamani lakini cha kushangaza vigogo polisi ndio wanaongoza kuvunja sheria.
dah hii nchi
 
Kilicho badlika , ni lugha baina ya mtuhumiwa na Polisi .
Sasa hivi mtuhumiwa hatishwi sana kwa like swali " unataka ni tumbuliwa kwa pesa ndogo hivyo?
Na Ile taalifa ya nyongeza ya "utapata kesi ya uhujumu uchumi"

Mengine yote yalikuepo TU.
 
Tanzania si waruhusu tu mirungi iwe biashara halali ila Kodi iwe juu
 
Acheni ukuda, tuacheni tuburudike.
snoop-dogg-weed.gif
 
Back
Top Bottom