ARUSHA: Tisa mbaroni kwa kuuza sukari kinyume na bei elekezi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
mbaroni.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500 na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

Chanzo:Mwananchi
 
Sasa wote tunajua kuwa sukari ilipanda mno hiki kipindi, kwa muuzaji wa reja reja mfano kaenda kununua mfuko wa sukali kakuta elfu 50 badala ya elfu 40, unategemea ataendelea kuuza kwa bei elekezi?? Hapa cha maana ningeona km wangekamata wauzaji wa jumla.
NB. Huu ni mtazamo wangu so mpunguze mapovu
 
Imefika hadi 6200! Duh! "tumeipenda wenyewe, chaguo letu milele, wacha waisome namba eeee, ccm mbele kwa mbele...."
 
mbaroni.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500 na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

Chanzo:Mwananchi
mbaroni.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500 na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

Chanzo:Mwananchi
Wakimaliza wa sukari wahamie Ngurdoto wanakouza soda Kwa Tshs 2000.
 
Hata sukari ni luxury, ulishaona mtu akakosa kunywa chai akafa?
hapana, wewe kwa nini unadhani hili suala linekuwa kubwa hivi?
soda ikipandishwa umma huwa unajali kiasi hiki?
basi ujue soda na sukari, sukari ni muhimu zaidi
 
Sasa hawa nao wahujumu uchumi!Duuuh!Haya bana tutafika.Sijasikia kama watafikishwa mahakamani au la! au ndo sukari waliyokua wanalangua nayo watu imegawiwa bure!
 
Watumishi wa Umma sasa wamepumua timua timua...issue.sasa ni sukari..sukarii sukariiii weeee...
 
Hao wapigwe pini alafu sukari watu tugawiwe kama kawa.... 6000 ili iweje kama si wizi ni nini
 
Kuepuka kwenda lupango, nitauza sukari kwa bei elekezi ya Tsh 1800 hata kama nitapata hasara japokuwa nimeinunua kwa Tsh 2300 kwa kilo...
Daaa, hii biashara imeshakuwa ngumu... Bora nirudi kwenye kibarua changu cha ualimu...
 
acha kuuza sukari, uza bidhaa nyingine
 
Back
Top Bottom