harakat
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 2,888
- 1,347
Uwanja wa Sheikh Abeid unatarajiwa kufurika watu siku ya tarehe 30/5/2015 kwa kuwa kipenzi cha watanzania na Rais Mtarajiwa atasimama mbele ya umati huo kukubali kutumwa kwa kuwatumikia watu hao kwenye kiti cha urais.
Moja ya changamoto kubwa ambayo atakutana nayo Rais ajaye ni pamoja na
1. bomu la ajira kwa vijana.
2. Suala la matumizi mabaya ya fedha za umma
3.Ukwepaji kodi na matumizi mabovu ya rasilimali za Nchi yetu.
4.Suala la kupuuzwa kwa elimu na watendaji wake.
5. Kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo kiongozi wa Nchi hii anayekuja atakutana nayo na bila shaka tutataka ayatatue kwa kiwango chake.
Uwezo wa Mh.lowasa kiutendaji si wa kubeza na ukiangalia nyadhifa alizowahi kushika serekalini na uwezo wake kisiasa utagundua kwamba hamna mtu ambaye anaweza kusimama nae katika kinyang'anyiro cha Urais na kumzidi.
Tukubali kwamba hili ni fungu jema chaguo la watu chaguo la Mungu.
Jitokeze uje umsikilize
Moja ya changamoto kubwa ambayo atakutana nayo Rais ajaye ni pamoja na
1. bomu la ajira kwa vijana.
2. Suala la matumizi mabaya ya fedha za umma
3.Ukwepaji kodi na matumizi mabovu ya rasilimali za Nchi yetu.
4.Suala la kupuuzwa kwa elimu na watendaji wake.
5. Kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo kiongozi wa Nchi hii anayekuja atakutana nayo na bila shaka tutataka ayatatue kwa kiwango chake.
Uwezo wa Mh.lowasa kiutendaji si wa kubeza na ukiangalia nyadhifa alizowahi kushika serekalini na uwezo wake kisiasa utagundua kwamba hamna mtu ambaye anaweza kusimama nae katika kinyang'anyiro cha Urais na kumzidi.
Tukubali kwamba hili ni fungu jema chaguo la watu chaguo la Mungu.
Jitokeze uje umsikilize
Zikiwa zimebaki siku mbili, masaa kadhaa, dakika kadhaa na sekunde kadhaa kuanza kwa safari ya matumaini joto limezidi kupanda Nchi nzima.... Joto hilo linatokana na kiu kubwa waliyonayo maelfu na mamillioni ya wananchi kusikia ujumbe wa matumaini na kisha kuanza safari ya matumaini ambayo itazinduliwa siku ya Jumamosi tarehe 30.05.2015....
Tarehe 25.05.2015 alipokuwa anaongea na wahariri wa vyombo vya habari, Lowassa alisema anatarajia kuzungumza na wananchi tarehe 30.05.2015 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo atazungumza mambo mbalimbali pamoja na kutangaza nia ya kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.....
Ni jambo la wazi ya kwamba, kwa hili joto lililopo siku ya jumamosi Nchi itazizima na kusimama kwa masaa kadhaa; tayari mpaka sasa kuna mlipuko wa shangwe, furaha na shamrashamra Nchi nzima wakijiandaa kuhudhuria ama kuangalia au kusikiliza kupitia vyombo vya habari tukio hilo la kihistoria tokea tupate uhuru, 1961..... Ni safari ambayo itagusa kila kona ya nchi kutoka Mbinga mpaka Ukerewe, Sirari~Katavi, Namanga~Tunduma, Karagwe~Nanyumbu, kwa uwingi wao wataelekea Arusha...
"Ndugu yangu nakwambia mpaka sasa huu mkoa wote wa Kigoma moto ushawaka. Kuna makundi ya mamia ya watu washaondoka tayari kwa safari ya Arusha... Lowassa ndiyo kiongozi jasiri tunayemtaka kwa sasa, ni mtendaji mzuri sana, ni mtu wa maamuzi magumu na sahihi, na kwa kweli lazima twende mpaka Arusha tukamsapoti katika hili" alisema Mzee Lukindo, kutoka Kigoma....
Katika hatua nyingine naye Mzee Mole kutoka kijiji cha Likokona, Nanyumbu (Mtwara) naye kapaza sauti na kuonyesha furaha ya hali ya juu sana kuhusu tukio hilo la Jumamosi "Bwana mdogo kesho asubui sana nawai kwenda Mtwara mjini naenda kununua Tv na kingamuzi, manake nimesikia ITV watarusha matangazo hayo moja kwa moja ili na mimi pia nipate kushuhudia tukio hilo... Hilo ni tukio la karne, ni tukio ambalo ni mwanzo wa ukombozi na mabadiliko katika nchi hii, kamwe siwezi kukosa kuangalia, ndiyo mana nimeamua kuchukua fedha zangu za mauzo ya korosho ili nikanunue Tv na kingamuzi kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo" alisema Mzee Mole, kutoka Nanyumbu, Mtwara...
Kwa hakika hili joto halijawahi kutokea, kila kona ya Nchi mamia na maelfu ya watu wana kiu na shauku kubwa ya kuanza safari hiyo ya matumaini..
Siku hiyo wakulima kwa uwingi wao, wafugaji kwa uwingi wao, bodaboda nchi nzima, wavuvi, wafanyakazi, MamaLishe, wanafunzi, vijana wasiyo na ajira na wenye ajira, watumishi wa umma, walimu, madaktari, manesi, wabunge, wakina mama, wazee na makundi mbalimbali wataelekea Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kupata neno la matumaini na lenye kuleta faraja katika maisha yao na vizazi vijavyo...
Ni wazi na kama inavyotarajiwa ya kwamba katika safari hiyo ya matumaini ndiyo watanzania tutapata majawabu ya ndoto za kuwa na elimu bora na bure, tutapata majawabu ya ndoto za watanzania kuwa na maji safi na salama, tutapata majawabu ya ndoto za watanzania kuwa na afya bora, tutapata majawabu ya ndoto za watanzania kuwa na kilimo kikichobora zaidi na cha kisasa, tutapata majawabu ya ndoto za watanzania kuondokana na umasikini na vile vile siku hiyo ya jumamosi watanzania tutapata majawabu ya ndoto ya kuwa na matumaini ya maisha bora kwa kila mtanzania...
Mytake:.. Ndugu Mtanzania mwenzangu, huu ndiyo wakati wa mabadiliko na katika nyakati hizi kama Taifa lazima tusimame na yule ambaye bila shaka ana uwezo, ana nia, na ana dhamira ya dhati kutuvusha hapa tulipo.... Huyo siyo mwingine bali ni yule ambaye tarehe 30.05.2015, siku ya Jumamosi atanguruma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha..... Jumuika nasi katika mapambano haya ya kuondoa umasikini kwa watanzania kwa kuungana pamoja katika safari ya matumaini.....