Vifaranga vya kuku 6,400 vyateketezwa kwa moto baada ya kukamatwa vikiingizwa nchini kinyume na sheria kutoka Kenya

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
a71539407cc1cb8c7823f3fc7d05d973.jpg
d5c3065e8e7d773a5acb54baf7a963d7.jpg


Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Arusha, imeteketeza kwa moto vifaranga vya kuku wa kisasa 6,400 wenye thamani ya shilingi milioni 12, wanaodaiwa kuingizwa nchini kutoka Kenya kupitia mpaka wa Namanga kinyume na sheria. Vifaranga vilivyoingizwa nchini kinyemela kuteketezwa

My take
Hawa Viongozi ni wa aina gani..!Unachoma kifaranga kwa maana gani? Hii siyo haki kabisa na ni ukatili kwa kiumbe hai kisichokuwa na hatia wala utambuzi.
 
Kuvirejesha vilikotoka ilikuwa busara zaidi kuliko kuviteketeza, we should be kind to animals.

Kwani hata kama ni magonjwa mpaka sasa hakuna quarantine kwa bidhaa za aina hii kutoka Kenya na hata ingekuwepo bado kuna ndege asilia wanaruka kati ya nchi hizi mbili na hawajui cha hizo taratibu wala visa!
 
Wa Africa kama tumelogwa vile yani.... Sheria inasemaje? Ni bora hata wangevitaifisha

Wakikamata bangi na madawa hawachomi.. Wakikamata viumbe hai wanawachoma.... Mungu tusaidie tunapoelekea hii nchi hata wahamiaji haramu wataanza kuchomwa
 
Haki za wanyama hazijazingatiwa. Si busara kabisa. Kuku si vipodozi au electronics uchome hivyo.
Labda kwa sab hakuna chama cha kutetea ndege km kipo toothless. Lkn ni ukatili ulioje. Sijui walikuwa wanajisikiaje wakati vifaranga vinalia kwa uchungu wa kuungua moto? Nilimchoma panya nikiwa mtoto alikuwa anakimbia huku anawaka mpk akaishiwa nguvu na kufa lkn nakijutia kitendo kile mpk leo.
 
Inashangaza sana kuawaua viumbe wakati kuna sheria ya ustawi wanyama inayosimamiwa na wizara ya mifugo kukiwa na mkurugenzi anayelipwa mshahara. Je siku kuna tatizo na Kenya?

Hivi sasa vyombo vya habari vya kenya vinaandika kuwa wafugaji wao wamedhulumiwa mifugo yao nchini Tanzania wanauliza mbona kuna wanyama pori na ndege ambao hutembea Tanzania na kenya na huwa kuna ushirkiano wa transboundaries disease
 
Back
Top Bottom