Taswira
JF-Expert Member
- Sep 23, 2012
- 1,198
- 447
Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa M bunge wa Arusha Lema ndiye chanzi cha vurugu ndani ya CHADEMA Kwakuanzisha kikundi cha vijana kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika utendaji wa chama hapa Arusha.
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA sasa imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la Viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto).Basi kila Mwanachadema tambue kuwa ndani ya chama hicho kuna block mbili(pande mbili)CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY).
Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamekiri kuwa chama sasa kimefikia hatua mbaya kwa kuwa watu wanatimuliwatimuliwa tu kwa sababu zisizoeleweka na bila kufuata utaratibu wa katiba ya nchama.
Hivyo wanainga hatua ya Zitto kuvuliwa vyeo na wanasisitiza kuwa Lema ndiye tatizo ndani ya chadema kwa hizi choochoko zinazoendelea.