Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi

hebu tumieni akili basi je eneo lake la kazi ni Arusha?.....alienda arusha kama nani na kuvamia duka kama nani?

uzuri Cctv znaonesha uwepo wake alienda hapo na kuonesha risasu nje akiwa na bunduki kwani wale ni majambazi? na hata kama ni majambazi je anahusika na usalama wa Arusha?
kwani huwajui POLIFISIEM? ukionekana kwenye tukio wewe ni mhusika.
 
Jamaa ni kichwa kweli...kaulizwa alijuaje ni Sabaya ndiye aliyeiba, akajibu nilimuona kwenye CCTV....Akaulizwa una uhakika gani jamaa alichukua hela...akajibu niliambiwa na Norman.


Akasema kwa sababu ya hofu, tarehe 17 alikimbilia Nairobi na familia yake...

Akaulizwa: Ulipima COVID19 maana kipindi hicho kuingia Kenya ilikuwa lazima utumwe....je aliingiaje Kenya?

Kama alipitia njia za panya, ana kesi ya kujibu.
Kama alipitia njia halali, watu wa mpakani upande wa Kenya wana Kesi ya kujibu kwa kupokea rushwa.

Takukuru anzieni hapo...nimewapa hints kidogo.
Umefafanua vzr we unaijua sheria utakuwa kada mzuri sana bdae
 
Mnahangaika sana kumsafisha huyo Sabaya, nawashauri muache huu utoto wenu, ushahidi wa uhuni wa Sabaya upo kila mahala mpaka kwenye video, ushahidi wa mtu mmoja ndio mnautumia kama kielelezo cha kushinda kesi, punguzeni ushabiki mandazi.
Acha uchawi ww
 
Sehemu ya mahojiano na Wakili wa utetezi, Moses Mahuna ilikuwa hivi.

Mahuna: Kwanini ulipopigiwa simu uende dukani kwako hukwenda.

Shahidi: Nilisikia mabishano pale dukani ndio nikapata hofu.

Mahuna: Je? Baada ya tukio hilo uliliripoti polisi

Shahidi: Hapana.

Wakili Dancon Oola: Una uthibitisho gani kuwa Sabaya na wenzake waliiba Sh 2,769,000 milioni.

Shahidi: Niliwaona kwenye CCTV camera
Oola: Je wewe uliamini vipi kama wao ndio wameiba?

Shahidi: Niliambiwa na Noman Jasin.

Wakili: Je uliripoti polisi?

Shahidi: Sijaripoti lakini niliandika barua TRA

Wakili: Unasema Februari 17 ulirudi Arusha na kuipeleka familia Kenya, Je? Ulipima Covid maana siku hiyohiyo umetoka Simanjiro ulikwenda Nairobi.

Shahidi: Hapana.

Wakili Chavula aliieleza Mahakama kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha Sabaya na wenzake.

NB. Uongo hauishi milele
Acha kutetea upumbavu
 
Wakili anauliza maswali ya covid bila hata kuuliza kama alienda na passport iligongwa au laa...
 
Mnahangaika sana kumsafisha huyo Sabaya, nawashauri muache huu utoto wenu, ushahidi wa uhuni wa Sabaya upo kila mahala mpaka kwenye video, ushahidi wa mtu mmoja ndio mnautumia kama kielelezo cha kushinda kesi, punguzeni ushabiki mandazi.
Wanahangaika sana hawa vyawa.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom