Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,106
2,000
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na wenzake wamefikishwa leo mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayowakabili.

Kesi itaanza kusikilizwa mfululizo. Upande wa Jamhuri una mashahidi 10.

===

Ushahidi kesi ya Sabaya: Shahidi aeleza alivyokimbilia kujificha Msikitini masaa matatu

Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili leo imeanza kusikilizwa huku shahidi wa kwanza alieleza alivyokimbia kujificha Msikitini.

Arusha. Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili leo imeanza kusikilizwa huku shahidi wa kwanza alieleza alivyokimbia kujificha Msikitini.

Akitoa ushahidi katika kesi hiyo ya unyang'anyi wa kutumia silaha, shahidi ya kwanza, Mohamed Saad amesema alikimbilia Msikitini wa Kijenge baada ya Sabaya na wenzake kuingia dukani kwake na kumpa dakika tano afike dukani.

Shahidi huyo akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo alieleza Mahakama kuwa alikimbia kwa hofu kwani baada ya Sabaya kufika dukani kwake alipigiwa simu na ndugu yake Ally Saad kuwa Sabaya yupo dukani na amekuwa akiwasumbua wafanyabiashara.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Abdallah Chavula shahidi huyo amesema Februari 9, mwaka huu, Sabaya na wenzake walivamia dukani na kuchukua kiasi cha Sh 2,769,000 milioni.

Amesema baada ya Sabaya kuingia dukani na wenzake walijitambulisha kuwa ni maofisa wa Serikali ambapo walianza kumtafuta ndipo ndugu yake Noman Jasin alimpigia simu kuwa anatakiwa dukani.

Alisema wakati anazungumza naye ndipo Sabaya alichukuwa simu na kumtaka ndani ya dakika tano afike dukani.

Alisema alikimbia kwenda kujificha Msikiti wa Kijenge na alikaa kuanzia saa 12 jioni hadi saa mbili na baadaye alikwenda kulala kwa rafiki yake eneo la Esso Makaburini.

Alisema baada ya upekuzi wa Sabaya dukani na kuchukua fedha na mashine ya EFD walikwenda hadi nyumbani kwake kufanya upekuzi.

Alisema alipigiwa simu na mke wake kuwa Sabaya na wenzake walivunja nyumba wakiwa na bastola na kuingia ndani wakimtafuta na wamesema hawatalala hadi wampate.

Amesema kutokana na hofu alikimbilia Wilaya ya Simanjiro kujificha na baada alirudi Arusha Februari 17 mwaka huu na kuichukuwa familia yake na kuipeleka Nairobi nchini Kenya na inaishi huko hadi sasa.

Sehemu ya mahojiano na Wakili wa utetezi, Moses Mahuna ilikuwa hivi.

Mahuna: Kwanini ulipopigiwa simu uende dukani kwako hukwenda.
Shahidi: Nilisikia mabishano pale dukani ndio nikapata hofu.

Mahuna: Je? Baada ya tukio hilo uliliripoti polisi

Shahidi: Hapana.

Wakili Dancon Oola: Una uthibitisho gani kuwa Sabaya na wenzake waliiba Sh 2,769,000 milioni.

Shahidi: Niliwaona kwenye CCTV camera

Oola: Je wewe uliamini vipi kama wao ndio wameiba?

Shahidi: Niliambiwa na Noman Jasin.

Wakili: Je uliripoti polisi?

Shahidi: Sijaripoti lakini niliandika barua TRA

Wakili: Unasema Februari 17 ulirudi Arusha na kuipeleka familia Kenya, Je? Ulipima Covid maana siku hiyohiyo umetoka Simanjiro ulikwenda Nairobi.


Shahidi: Hapana.
Wakili Chavula aliieleza Mahakama kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha Sabaya na wenzake

Chanzo : Mwananchi
 

Mwizukulu jilala

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
1,097
2,000
Kesi yenye mashahidi kuishinda huwa ni asilimia chache...ufungwe sabaya ukate rufaa utaenda kutokea mahakama kuu..
 

nsibirwaha

Member
Jun 10, 2021
57
125
Kikubwa ndio hicho,hata ikitokea muujiza akashinda Kesi zote lakini cha moto amekipata na atakuwa amejifunza,Ubabe na kujifanya mjuaji wa kila kitu,ubabe nk hatakuja kuvifanya tena,Jela isikie kwa mwenzio
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
6,499
2,000
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Silivester Nyegu na Daniel Mbula, leo wamepandishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kesi yao kuhamishwa kutoka Mahakama ya Mkoa wa Arusha.Kutokana na ufinyu wa nafasi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, kesi hiyo imepelekwa kusikilizwa katika vyumba vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo inatarajiwa kusikilizwa kwa siku 14 mfululizo.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,253
2,000
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Silivester Nyegu na Daniel Mbula, leo wamepandishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kesi yao kuhamishwa kutoka Mahakama ya Mkoa wa Arusha.Kutokana na ufinyu wa nafasi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, kesi hiyo imepelekwa kusikilizwa katika vyumba vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo inatarajiwa kusikilizwa kwa siku 14 mfululizo.
Naona Dogo anatupia tu suti ili kuendeleza Legacy ya Ukuu wake wa Wilaya!!
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,636
2,000
Naona Dogo anatupia tu suti ili kuendeleza Legacy ya Ukuu wake wa Wilaya!!
Bado ni Mfanyakazi wa idara flani,na hizo ni uniform za idara hiyo,na hata confidence aliyonayo inatokana na mbeleko anayoshikiziwa na wana idara,siku idara ikiamua kumtema mutamuonea huruma,huwa hawakutemi kienyeji enyeji,lazima wahakikishe kwanza umenyooka na utaendelea kuwa mnyoofu milele,au usiwepo milele!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom