Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Sasa naanza kuamini huyu jamaa alisingiziwa.

Chadema na wafuasi wao wakamzishia Bashiru kuchukua mabilioni ya pesa bank kuu kumbe uongo...
Subiri tumkomoe kwanza, ni mwendo wa siku 14 ,14 tu. Mpaka hukumu itoke ashachezea mwaka. Na akimaliza Arusha tunae Moshi
 
Bahati nzuri next tarehe imetajwa ni 16 July 21 na hao mashahidi bila shaka watafikishiwa habari na upabfe wa zmashataks ambao ni Serikali

Kama kuna janjajanja, itajulikana tu
 
Leo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai bwana Lengai Ole Sabaya amefikishwa mahakamani kwa mara ya tatu huku mashahidi wakishindwa kufika mahakamani na kusababisha kesi kusogezwa mbele hadi tarehe 16/7/2021...
Tulisema lazima Sabaya atoke kama pamba...in Raila Odinga's voice.
 
Kheeee haya sasa maajab
Ila kuna jambo ovu linaendelea katika hii nchi,inahitaji kuweka pembeni ushabiki wa kisiasa na utulivu wa hali ya juu kuelewa
 
Wiki moja kabla m-chato hajaanza kuvumishwa kuwa yupo hospitalini kenya, sabaya alivumishwa(na kigogo wa twitter) kuwa kala udongo.

inawezekana jamaa wanaigiza kuficha uhusika wake(sam-baya) kwa .... cha wa kitovu cha utalii.
 
Naona wamemfundisha kucheza movie

action = awe anatabasamu akitoka na kuingia kwenye basi la wanalupango
nyosha ngumi juu huku akitazama wananchi wanaomkodolea macho kama mwewe
 
Eti atashinda Kesi, ashinde kivipi wakati Ushahidi dhidi ya tuhuma zake umenyooka kama rula!!!atachukua mvua ili aolewe kabisa Jela matako huyu, katutesa sana mjini hapa
Isije ikwa unaiishi dar unajifanya hapa jf eti ni mkazi wa hai.
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika CCM ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei mahabusu huyu mwizi
Huyo jamaa inadaiwa ni TISS kweli. Huyo na katambi
 
Ole Sabaya mtu mwenye tuhuma zisizo na idadi , leo tena amefikishwa mahakamani huko Arusha akiwa amevaa Suti iliyopauka ili kusikiza kesi zinazomkabili.

Kesi za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo.

Mashitaka mawili ambayo leo yanatarajiwa kuanza kusikilizwa ni ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo mawakili wa Serikali, Tumaini Kwema, Abdallah Chagula na Tarsila Garvas walieleza kuwa upelelezi wake umekamilika.

Mashitaka hayo yatafikishwa leo mbele ya mahakimu wawili tofauti; Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha.

-----UPDATE-----

Mahakama ha Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi inayomkabiri aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya mara baada ya mashahidi wa kesi ya unyanganyi wa kutumia silaha kutofika Mahakamani.

Mawakili wa Serikali waliiambia Mahakama kuwa Shahidi amepata udhuru na kuahidi kuwa atakuwepo siku nyingine itakayopangwa kesi hiyo.

Kesi imeahilishwa mpaka Tarehe Julai 16, 2021.

--
Hiv mashahidi wasipofika mahakamani dalili ni njema kwa mtuhumiwa.siku si nyingi DC Sabaya atakuwa huru.Naomba mtunze hii meseji
 
Back
Top Bottom