Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai , Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya na wasaidizi wake wawili.

Kesi hiyo ya jinai namba 66/2021 ilikuja mahakamani hapo leo kwa ajili ya kusikilizwa,lakini ilishindwa kuendelea kutokana na shahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kufika mahakamani.

Mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ,Salome Mshasha wakili wa Serikali, Tarcilla Gervas aliiomba mahakama hiyo kuahirisha shauri hilo kutokana na shahidi wao kutofika mahakamani,ambapo hakimu Mshasha aliahirisha shauri hilo hadi Julai 16 mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kusikilizwa huku akisisitiza upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha mashahidi wao.

Awali wakili wa utetezi,Mosses Mahuna na Dancan Oolah wakiwakilisha washtakiwa wote watatu wamelalamikia upande wa mashtaka kupoteza muda wakati walishaiambia mahakama hiyo kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba Jambo hilo lisijirudie.

Washtakiwa wengine katika shauri hilo ni wasaidizi wa Sabaya,Silvester Nyegu (26) na Daniel Mbura(38) ambapo kwa pamoja wanaokabiliwa na kosa la Unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la mfanyabiashara Saad Mohamed baada ya kumpiga na kumtishia kwa silaha diwani wa kata ya Sombetini Bakari Msangi na Kumpora kiasi Cha shilingi 390,000.

Wakati huo huo kesi namba 27/2021ya uhujumu Uchumi, Utakatishaji fedha haramu,na Rushwa,inayomkabili Sabaya na wenzake saba imeahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili wa Serikali Tarcilla Gervas Mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirisha Hadi Julai 16 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

Akiongea nje ya mahakama wakili wa Serikali Tarcilla Gervas,alisema kuwa shauri hilo awali lilikuwa na washtakiwa Sita ila June 21mwaka huu,upande wa mashtaka umeongeza washtakiwa wengine wawili na kufikia nane.

Aliwataja washtakiwa hao ni Jackson Macha (24) na Nathan Msuya (31) wote wakati wa Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wengine ni Enock Togolani Mnkeni {41} Watson Stanley Mwahomange {27} John Odemba Aweyo na Syliverster Nyengu{26} .


IMG_20210702_103649_176.jpg
IMG_20210702_103646_796.jpg
 
Kwa mwenendo ulivyo namshauri mama amuachie Sabaya na amrudishie cheo chake cha mkuu wa wilaya pale Hai... na ikimpendeza pia amrudishe Makonda pale Dar es salaam a awape mamlaka zilezile walizopewa na mwendazake...
Nchi inahitaji watu wa aina hii hakika. Nilimpinga magufuli na kuchukizwa na aina ya utawala wake.

Ila kinachoendelea sasa hivi, kwa pande zote ni upumbavu aisee. Sema wa Tz tunaakili za kushikiwa.
 
Anapigishwa tarehe kwanza ili asote ndani kama kina Singa Singa na Rugemarila. Wala sio kwamba mashahidi wamemuogopa mchumba tu huyo.

Kwanza kama ulikua hujui, Sabaya katika geraza la kisongo ni mke wa mtu.
Kwa kina Lema, Mbowe, Mdude na wengine waliopo/waliokuwepo rumande walikuwa wake za watu humo ndanj?
 
Leo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai bwana Lengai Ole Sabaya amefikishwa mahakamani kwa mara ya tatu huku mashahidi wakishindwa kufika mahakamani na kusababisha kesi kusogezwa mbele hadi tarehe 16/7/2021.

Kwa tuhuma alizokuwa akiporomoshewa Sabaya inashangaza kusikia kuwa hamna mhanga hata mmoja wa Sabaya aliyefika mahakamani kutoa ushahidi wake.

Hata Mbowe ameshindwa kufika kutoa ushahidi?
 
Leo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai bwana Lengai Ole Sabaya amefikishwa mahakamani kwa mara ya tatu huku mashahidi wakishindwa kufika mahakamani na kusababisha kesi kusogezwa mbele hadi tarehe 16/7/2021...
Hii kesi kwanini inatajwa mahakamani mwezi mara mbili,? Ili takiwa itajwe Sept na Dec 2021. Pia uhujumu uchumi , mahakama inahitaji mashahidi wapi?
 
Hapa kuna siasa inaendelea "underground" kutaka kuimaliza hii kesi mapema jamaa yao aachiwe huru, kama vile wale waandishi wa habari waliolalamika kutishwa wakiripoti habari za Sabaya, vipi kwa hao mashahidi watakuwa na usalama gani? wao hawajaanza kutishwa?

Hapa ni vyema watu wakajiandaa mapema kisaikolojia, hii kesi siku ya hukumu ni either jamaa ataachiwa huru, au atahukumiwa kifungo cha muda mfupi baadae aje kuachiwa mbele ya safari kwa msamaha wa Rais, mazingira ya hii kesi ni maigizo matupu.
 
Ole Sabaya mtu mwenye tuhuma zisizo na idadi , leo tena amefikishwa mahakamani huko Arusha akiwa amevaa Suti iliyopauka ili kusikiza kesi zinazomkabili...
Huyu jamaa ataigalagaza serikali vibaya sana. Huwezi kuendesha kesi mahakamani kisha unaruhusu mtuhumiwa kuhukumiwa na watu binafsi wanapandisha ushahidi wa picha mwendo kwenye mitandao ya kijamii. [You can't be a judge on your own cause]

Mashahidi wote wa kutengeza watakimbia kwa mtindo wa udhuru. Eti kipenyo anapandishwa mahakama ya uraia kwa njia ya udhalilishaji, kila mmoja mwishoni ataanza kuikimbia kesi kwa visingio mbalimbali.
 
Leo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai bwana Lengai Ole Sabaya amefikishwa mahakamani kwa mara ya tatu huku mashahidi wakishindwa kufika mahakamani na kusababisha kesi kusogezwa mbele hadi tarehe 16/7/2021.
...
Too much politics
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom