Arusha: Rufani ya Sabaya yapokewa Mahakama Kuu

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,352
14,629
Rufani ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya imepokelewa mahakama kuu kanda ya Arusha ikiwa na hoja nzito 10 za kupinga kifungo cha miaka 30 jela alichofungwa baada ya kuhisiwa kuiba simu ya Tecno na hela taslimu laki tatu na elfu sitini.
===

Arusha. Ikiwa zimepita siku 22 tangu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imepokea rufaa yao.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Wakili wa utetezi Mosses Mahuna amesema rufaa hiyo imepokelewa na kupewa namba 129 ya mwaka 2021.

Amesema rufaa hiyo iliyowasilishwa wiki hii na kupokelewa na kwamba wana hoja zaidi ya 10 za kukata rufaa hiyo. Hata hivyo, hakuwa tayari kuzielezea kwa undani.

"Rufaa ambayo tumekata ni ya kesi namba 105 ya 2021 na imefunguliwa wiki hii na kupewa namba 129 na sasa tunaendelea kusubiri taratibu nyingine," amesema Mahuna.

Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu likiwemo la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Kesi hiyo ya jinai ya unyang'anyi wa kutumia silaha namba 105 ya 2021, ilisikizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo.

Chanzo: Mwanachi
 
Kwa hiyo umefurahi kuwa sasa atashinda Kesi na atatoka uendelee kwenda kupiga mizinga ya hela za ujambazi.
Aisee !
Only in TZ jambazi anashangiliwa
Appeal kupokelewa sio tatizo. Tatizo ni je? Atashinda au ni kusumbua mahakama tu? Sabaya kesi yake ilikuwa wazi sana na ushahidi wa wazi wazi. Hapo hana anachokitafuta zaidi ya usumbufu tu na yale ya mfa maji haishi kutapatapa.
 
Acha na yeye avune alichopanda bado 5 mbeke hizo bil 3 anazotambia zitaisha tu....muda mwalim mkuu
 
Yaani hawa mawakili wameamua kula pesa za jambazi. Maana hapo sasa mvua zinakwenda kuongezeka hadi 60. Hakuna jinsi Sabaya ana chomoka kwenye mashtaka.
Atapigwa mvua za kutisha, OCD Hai aajiandae kupandishwa kizimbani
 
Ni sawa na hao wanaomtetea gaidi mbowe, niwapuuuzi kama wapuuuzi wenginee

Huo ugaidi wa mbowe umeshathibitishwa wapi? Ujambazi wa sabaya umethibitishwa wazi kabisa pasipo shaka!
Kusema Mbowe ni gaidi ilihali haijathibitishwa hata chembe utakuwa mpuuzi na mburula zaidi...una ufala mwingi sana!
 
Hahahaaaa,na hapo bado kesi ya uhujumu uchumi!
Huyo hatoki mpaka awe na miaka 80!
Etiiiiii?

20211015_203338.jpg


2965134_1634322688181.png
 
Niliomba humu hukumu ya kesi hiyo sijapatiwa.Lakini Mimi naamini kuwa anaweza kushinda yake hiyo
 
Huo ugaidi wa mbowe umeshathibitishwa wapi? Ujambazi wa sabaya umethibitishwa wazi kabisa pasipo shaka!
Kusema Mbowe ni gaidi ilihali haijathibitishwa hata chembe utakuwa mpuuzi na mburula zaidi...una ufala mwingi sana!
Kilichomuweka stooo mpaka Leo ni bonanza??
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom