Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,703
- 15,156
Rufani ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya imepokelewa mahakama kuu kanda ya Arusha ikiwa na hoja nzito 10 za kupinga kifungo cha miaka 30 jela alichofungwa baada ya kuhisiwa kuiba simu ya Tecno na hela taslimu laki tatu na elfu sitini.
===
Arusha. Ikiwa zimepita siku 22 tangu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imepokea rufaa yao.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Wakili wa utetezi Mosses Mahuna amesema rufaa hiyo imepokelewa na kupewa namba 129 ya mwaka 2021.
Amesema rufaa hiyo iliyowasilishwa wiki hii na kupokelewa na kwamba wana hoja zaidi ya 10 za kukata rufaa hiyo. Hata hivyo, hakuwa tayari kuzielezea kwa undani.
"Rufaa ambayo tumekata ni ya kesi namba 105 ya 2021 na imefunguliwa wiki hii na kupewa namba 129 na sasa tunaendelea kusubiri taratibu nyingine," amesema Mahuna.
Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu likiwemo la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kesi hiyo ya jinai ya unyang'anyi wa kutumia silaha namba 105 ya 2021, ilisikizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo.
Chanzo: Mwanachi