Arusha: Profesa Patrick Lumumba ahimiza uwazi na uwajibikaji kwa viongozi na Serikali

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mataifa ya Bara la Afrika yametakiwa kuendelea kudumisha ushirikiano kwa vitendo ili kuchochea maendeleo ya nchi hizo kupitia misingi ya Uwazi na uwajibikaji.

Hayo yamebainishwa na Profesa Patrick Lumumba Mwananzuoni mbobezi wa masuala ya uchumi Afrika katika Kongamano la Masuala ya Uwazi na uwajibikaji kwa maslahi ya maendeleo ya Bara la Afrika lililoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya WAJIBU na kufanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika kongamano hilo,lililojumisha asasi mbalimbali za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi alisema ipo haja kwa viongozi na wananchi wa Afrika kushikamana ili Kuweza kuwa na matunda ya pamoja.

Naye waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema Tanzania ni miongoni mwa Taifa lililo barikiwa kuwa na Rasilimali nyingi muhimu kwa maendeleo ya uchumi ikiwemo Rasilimali Madini ila Suala la Uwazi na uwajibikaji ni Chachu ya kuongeza wawekezaji katika rasilimali hizo.

Kando na Hilo,Kundi la Vijana nalo halikuachwa nyuma,ambapo Joyce Nnkini ni Mkuu wa Kitengo Cha Masuala ya Uchunguzi na Udhibiti wa majanga barani Afrika anaeleza nafasi ya vijana.

Alisema bara la Afrika linatajwa kuwa Miongoni mwa mabara ambayo uchumi wake utakua mara dufu endapo ushirikiano wake utadumishwa kwa vitendo na kupunguza utegemezi.

Mwisho.
 
Huyu professor sijui nani kampa huo uprofessor? Hamna kitu kabisa zaidi ya hamasa, mihemko na upumbavu. Hawa ndio akina Kabudi, Lipumba nk wote chungu kimoja
 
Back
Top Bottom