Arusha: Polisi wamkamata mfanyabiashara kwa utapeli wa viwanja 51

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1578892251069.png

Polisi Mkoani Arusha limemtia mbaroni mfanyabiashara, Joseph Rwakeza anayemiliki Kampuni ya Kabale Estate, kwa kushindwa kutoa hati za viwanja baada ya kuuza viwanja zaidi ya 51 na kujipatia Sh milioni 590 na kutokomea kusikojulikana kwa zaidi ya miaka saba.

Mfanyabiashara huyo alikamatwa na polisi akiwa kijijini kwao mkoani Kagera na kurudishwa Jijini Arusha, kujibu mashitaka hayo.

Kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kutokana na baadhi ya wananchi waliotapeliwa, kulalamika kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Gambo kuagiza Polisi kumsaka mahali popote alipo, ili aweze kuja Jijini Arusha kujibu mashitaka yake.

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Jonathan Shana alipoulizwa juu ya hilo alikiri na kusema kuwa suala lake linashughulikiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha{RCO} kwani yeye kwa sasa yuko safarini.

Taarifa za kipolisi zinasema kuwa kampuni ya Kabale Estate ilipewa kazi na kampuni nyingine ambayo bado haijajulikana kwa sasa kugawa shamba la ekari 15 kwa ukubwa tofauti na kutafuita hati ya kila kiwanja kazi ambayo kampuni hiyo iliifanya.

Vyanzo vya habari vilisema Mfanyabiashara Rwakeza kupitia kampuni yake ya Kabale Estate ilifanya kazi hiyo na ilikabidhi hati zote kwa kampuni iliyompa kazi na shughuli hizo zilifanyika mwaka 2012 hadi 2013.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa Rwekeza alirudi tena kwa kampuni hiyo na kusema kuwa kuna baadhi ya wananchi wamevipenda viwanja hivyo na wako tayari kulipa fedha taslimu.

Habari zinasema kuwa alikubaliwa kuuza viwanja kwa masharti ya mteja akilipa fedha taslimu atapewa hati yake na alifanya hivyo kwa viwanja 31 tu kati ya viwanja 51 alivyouza .

Habari kutoka polisi zilisema kuwa viwanja hivyo vilikuwa vikiuzwa kati ya shilingi 18,000 hadi 35,000 lakini viwanja 20 vilivyouzwa na kampuni ya Kabale Estate pesa yake haikupelekwa kwa kampuni iliyompa kazi na kufanya mmiliki wa kampuni iliyompa kazi kugoma kutoa hati.

Taarifa ilisema kuwa maana ya kampuni hiyo kugoma kutoa hati na Rwakeza kusumbuliwa na walionunuwa viwanja aliamua kutoweka na ndio wananchi walionunuwa kulalamika kwa Mkuu wa Mkoa kwa utapeli huo.

Habari zilisema kuwa walionunuwa viwanja hivyo wengi wao ni watumishi wa Serikali ,Taasisi za Umma na wananchi wa Jiji la Arusha zaidi ya 45 na viwanja viko katika mtaa wa Olosuruwa kata ya Moshono Jijini Arusha.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mfanyabiashara huyo alikiri katika vikao vya mahojiano kupokea fedha kutoka kwa wananchi hao lakini alishindwa kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho ni kwa nini ameshindwa kuwapa hati kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka saba.

Habari zilisema kuwa kikosi cha askari polisi kanzu,wananchi waliouziwa viwanja,mwanasheria wa serikali,Ofisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa{TAKUKURU} na Ofisi ya Usalama Taifa Mkoa walienda eneo la tukio na kuwataka wale wote waliouziwa viwanja kukaa katika kila kiwanja alichouziwa na kupigwa picha.
 
Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Joseph Abel Rwakeza anayemilikiwa kampuni ya Kabale Estate ametiwa mbaroni na jeshi la polisi Arusha kwa tuhuma za kuuza viwanja na kujipatia shilingi milioni 590 bila ya kutoa hati na kutokomea kusikojulikana kwa zaidi ya miaka saba.

Mfanyabiashara huyo ambaye mpaka sasa yuko rumande kwa zaidi ya wiki alikamatwa na polisi akiwa Kijijini kwao Mkoani Kagera na kurudishwa Jijini Arusha kujibu mashitaka hayo.

Rwakeza alikamatwa na polisi baada ya wananchi waliotapeliwa kulalamika kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Mkuu huyo kuamrisha Polisi kumsaka mahali popote alipo ili aweze kuja Jijini Arusha kujibu mashitaka yake .

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Jonathan Shana alipoulizwa juu ya hilo alikiri na kusema kuwa suala lake linashughulikiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha{RCO} kwani yeye kwa sasa yuko safarini.

Taarifa za kipolisi zinasema kuwa kampuni ya Kabale Estate ilipewa kazi na kampuni nyingine ambayo bado haijajulikana kwa sasa kugawa shamba la ekari 15 kwa ukubwa tofauti na kutafuita hati ya kila kiwanja kazi ambayo kampuni hiyo iliifanya.

Vyanzo vya habari vilisema Mfanyabiashara Rwakeza kupitia kampuni yake ya Kabale Estate ilifanya kazi hiyo na ilikabidhi hati zote kwa kampuni iliyompa kazi na shughuli hizo zilifanyika mwaka 2012 hadi 2013.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa Rwekeza alirudi tena kwa kampuni hiyo na kusema kuwa kuna baadhi ya wananchi wamevipenda viwanja hivyo na wako tayari kulipa fedha taslimu.

Habari zinasema kuwa alikubaliwa kuuza viwanja kwa masharti ya mteja akilipa fedha taslimu atapewa hati yake na alifanya hivyo kwa viwanja 31 tu kati ya viwanja 51 alivyouza .

Habari kutoka polisi zilisema kuwa viwanja hivyo vilikuwa vikiuzwa kati ya shilingi 18,000 hadi 35,000 lakini viwanja 20 vilivyouzwa na kampuni ya Kabale Estate pesa yake haikupelekwa kwa kampuni iliyompa kazi na kufanya mmiliki wa kampuni iliyompa kazi kugoma kutoa hati.

Taarifa ilisema kuwa maana ya kampuni hiyo kugoma kutoa hati na Rwakeza kusumbuliwa na walionunuwa viwanja aliamua kutoweka na ndio wananchi walionunuwa kulalamika kwa Mkuu wa Mkoa kwa utapeli huo.

Habari zilisema kuwa walionunuwa viwanja hivyo wengi wao ni watumishi wa Serikali ,Taasisi za Umma na wananchi wa Jiji la Arusha zaidi ya 45 na viwanja viko katika mtaa wa Olosuruwa kata ya Moshono Jijini Arusha.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mfanyabiashara huyo alikiri katika vikao vya mahojiano kupokea fedha kutoka kwa wananchi hao lakini alishindwa kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho ni kwa nini ameshindwa kuwapa hati kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka saba.

Habari zilisema kuwa kikosi cha askari polisi kanzu,wananchi waliouziwa viwanja,mwanasheria wa serikali,Ofisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa{TAKUKURU} na Ofisi ya Usalama Taifa Mkoa walienda eneo la tukio na kuwataka wale wote waliouziwa viwanja kukaa katika kila kiwanja alichouziwa na kupigwa picha.

Mwisho.
IMG_20200110_112814_2.jpeg
IMG_20200110_113335_2CS.jpeg
IMG_20200110_113124_2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katapeli nusu billion! Una tapeli afu unaenda bush tena hapa hapa nchi...?
 
Hivi mkuu hio Co. Inaitwa kabale au ni kambele ambao ndio wamesponsor vile vibanda vya police wa barabarani kujikinga na jua/mvua.

dodge
BREAK NEWS!!!!! NAPENDA KUTOA UFAFANUZI KUWA KABALE ESTETE SIO KAMBELE Investments....Kwani kwa tarifa nyingi za mgogoro wa Ardhi zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zanazoiusu kampuni ya KABALE ESTETE Wengi wamefikiri ni KAMBELE Investments. Sio KAMBELE Investments ni KABALE ESTETE..ila kwa tarifa zaidi tupigie 0753 899200.... pia unaweza kutusaidia kusambaza ujumbe huu ili uwafikie na wateja wetu wote...

Asante kwa ufafanuzi.

Back
Top Bottom