Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,342
- 5,536
Katika kile kinachoelezwa kuwa ni kuimarisha ulinzi katika jiji na kujihami na machafuko yoyote yanayoweza kuhatarisha amani, polisi wameweka doria katika maeneo ya Kikatiti na Kia kwenye barabara itokayo Moshi kuelekea Arusha na wanapekua magari yanayoelekea Arusha yanayotiliwa shaka. Binafsi nimekutana na vizuizi hivyo na kusimamishwa kisha kupekuliwa kabla ya kuniruhusu kuendelea na safari. Nilipouliza kulikoni kutoka kwa askari aliyekuwa anatukagua nikaelezwa ni mkakati wa kuhakikisha hakuna silaha zinazopelekwa Arusha ili kuzuia machafuko yanayoweza kutokea. Na mkakati huo unalenga kupekua gari zote watakazozitilia shaka ilimradi tu zinaelekea jiji la Arusha.
Mytake: Kama jeshi limeingiwa na hofu kiasi hicho, kwanini wasiishauri mahakama kupitia serikali kumwachia Lema ili hali irudi kuwa ya kawaida!?
TAFAKARI!
Mytake: Kama jeshi limeingiwa na hofu kiasi hicho, kwanini wasiishauri mahakama kupitia serikali kumwachia Lema ili hali irudi kuwa ya kawaida!?
TAFAKARI!