Arusha: Polisi auawa kwa panga akijaribu kumkamata mwizi usiku nyumbani kwake

Anaendaje polisi mmoja kukamata mwizi saa tano usiku! Polisi wengine hakuna wa kusaidiana?
Nadhani ilikuwa kesi ndogo hivyo waliona hakuna hatari kubwa. Sidhani hata ni uzembe kwani duniani kote polisi wamekuwa victims wakati waki-deal na wahalifu. Ila huyo jamaa akikamatwa atajuta. Ni bora ajiue kabla hawajamkamata.
 
Waziri Wa Fedha na Bunge lilivopitisha maongezeko ya kodi na tozo, pamoja na kusitisha ajira kwa miaka 6 kwa wahitimu, walitegemea vijana wafanye kazi gani??? Kama sio kuwa majambazi na vibaka.
We kweli popoma,yaani mtu afanye ujambazi kisa tozo na ajira.Hizo ni tabia tu za watu na ni maisha waliyoyachagua wenyewe
 
Kumuelewa mtoa maelezo inahitajika uwe unatumia vitu vyingi kwa pamoja yaani konyagi,balimi,safari lager, k vant ,serengeti lite kisha uvavyimix vyote kwa pamoja baada ya kunywa unaweza kumuelewa tofauti na hapo na wewe uwe ni askari polisi au mataga
 
Uyo polisi marehemu nae kajitakia kwa nn aende kukamata muhalifu usiku mnene hili hali yupo peke yake ndio kujiamini gani huko
 
Polisi wanalindana sana mkuu. Hata mmoja wao akifanya kosa wanamlinda ili kutoonesha madhaifu yao.
 
Ngoja wawe wanakumbushwa kwamba ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga wanaonea sana laia hawa wadude
 
Ukitaka kukamata mhalifu na rushwa iwe kubwa nenda mwenyewe, ukitaka kukamata mhalifu salama na rushwa mgawane nenda na wenzako
 
Nasema hivi hiyo taarifa Ina ukakasi Polisi wengi hawafuati miaongozo ya kazi zao ubabe wa kijinga umetamaraki miongoni mwao
Unaendaje kukamata mharifu usiku mnene tena nyumbani kwake na hujapitia Kwa uongozi wa mtaa
Mbaya zaidi upo jeshi la mtu mmoja?

Hapana Kuna Jambo linafichwa huyo itakua alikua anania ya rushwa,au mbususu

Nadanganya wadau?
 
Jina la aliyefariki je? Au familia yake bado haijataarifiwa?
Anaitwa afande damas eliakim magoti zamani alikuwa kituo cha usa river, sijui ikawaje akahamishiwa huko mbughuni.

B2944850-2922-424E-93CE-0FB997E08E19.jpeg


37D1D8B8-7427-4572-8D13-F1C758EBACAE.png


3ECB51B9-9EBE-4310-A372-3117F7F13B11.png
 
Inakuwaje kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa akiwa peke yake Tena SAA 5 za usiku? Kwani Sheria Ina semaje kukamata mhalifu baada ya SAA 12 jioni na kabla ya saa12 asubuhi?
 
Askari polisi katika kituo kidogo Cha polisi Mbughuni wilayani Arumeru, Mkoani hapa, ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani wakati akijaribu kumkamata mtuhumiwa.wa wizi.

Tukio hilo limetokea Jana majira ya saa tano usiku katika Kijiji Cha Makiba wakati Askari huyo( jina linahifadhiwa) alipoenda nyumbani kwa mhalifu kwa lengo la kumkamata.

Kwa mujibu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi ACP-Justine Masejo askari huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuvunja damu nyingi.

"Askari wetu katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni alikatwa panga kichwani na kufariki dunia baada ya kwenda nyumbani kwa mhalifu majira ya saa tano usiku lengo la kumkamata, hivi Sasa polisi wanaoendesha operesheni ya kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya dola"alisema Masejo

Kamanda alifafanua kwamba askari huyo alienda Nyumbani kwa mtuhumiwa kwa nia ya kumkamata kuhusiana na matukio ya wizi wa mazao na kwamba wakati akijaribu kumkamata ndipo alipotokea mhalifu mwingine Nyumba ya jirani ambaye alimkata panga moja kichwani askari huyo nakupoteza Maisha.

Aidha Masejo aliongeza kuwa kabla ya tukio hilo mwananchi mmoja alifika katika kituo cha polisi Mbughuni kulalamika.juu ya mtuhumiwa wa wizi wa mazao yake ambapo polisi walianza msako wa kumvizia mtuhumiwa huyo.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa uchunguzi, aliweza kufanikiwa kutoroka baada ya tukio hilo na polisi wameanzisha msako Mkali dhidi ya Watuhumiwa hao .

Ends
Kuna la kujifunza hapa, Askari kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa peke yake usiku tena bila kuwa na search warrant au kibali cha kuingia ndani ya nyumba hiyo ni hatari kabisa .Au alienda kutengeneza mazingira fulani.?

Askari inaonesha hata silaha hakuwa nayo !

Zamani askari mmoja aliweza kusomba mtaa mzima akiwa peke yake, Watu walikuwa,Watiifu sana ,Siku hizi mambo yamebadilika.Siku hizi kwenda kukamata mhalifu mmoja inahitaji polisi zaidi ya. Wawili

Raia wamekuwa na nidhamu mbovu sana, Polisi muwe makini mnapoenda kukamata hasa nyakati za usiku.Bebeni silaha.

Mungu amuweke mahali alipokuwa dakika.
Amina
 
Back
Top Bottom