Arusha: Polisi akiwemo mkuu wa kituo mbaroni Kwa Rushwa ya millioni 6

Hiyo mln 6 wangegawana vizuri wala kusingetokea timbwili
Tatizo hapo kuna mmoja alitaka wazidi wenzake
Ale zaidi,ndiyo kuchomana

Ova
 
Kilakitu kwao wanashindwa wanaweza nn hawakujua Kama walengeshaji ni watu muhimu ktk zoezi lamgao
 
Askari Polisi Wawili wa Wilaya ya Arusha akiwemo Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi{Police Post} cha Engutoto Inspekta Msaidizi{ Mrakibu Msaidizi},Alphonce Kashuku wanashikiliwa na jeshi hilo katika kituo kikuu cha polisi Arusha kwa tuhuma za kupokea rushwa ya milioni 6 na kuachia gari aina ya fuso lililokuwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zilisema kuwa mbali ya Inspekta Kashuku mwingine ambaye anashikiliwa ni konstebo James Kinyala ambaye ni askari wa upelelezi kituo Kikuu ya Arusha.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa tukio hilo lilitokea novemba 17 mwaka huu majira ya mchana katika kata ya Engutoto baada ya askari Mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupata taarifa juu ya gari hilo ambalo namba zake bado hazijapatikana kuwa gari Hilo Limebeba mzigo huo wa dawa za kulevya wenye thamani ya mamilioni ya pesa.

Habari zilisema kuwa baada ya askari mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupewa taarifa hizo kutoka kwa raia wema, walikwenda kumpa taarifa Mkuu wa kituo cha Polisi Engutoto Inspekta Kashuku na gari hilo lilikamatwa na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi.

Vyanzo hivyo vilisema kuwa taratibu zote zilifanyika katika kituo cha polisi Engutoto ikiwemo kulipekua gari hilo na wahusika kukiri kusafirisha mzigo huo na kuwekwa rumande.

Habari zilisema watuhumiwa walifanya kila namna taarifa hizo kutofika kituo kikuu cha polisi Arusha na kumshawishi Mkuu wa Kituo cha Engutoto Inspekta Kashuku kuchukua kiasi cha shilingi milioni 6 ili waweze kuachiwa na kuondoka na gari hilo na hatua hiyo waliweza kufanikiwa na watuhumiwa hao kutoweka na gari baada ya kutoa kiasi hicho cha fedha.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa kiongozi mmoja wa serikali ngazi ya kata hakushirikishwa katika kupata mgao wa shilingi 200,000 walizopata wenzake na bila kujua alitoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha{OCD} kuomba kamishine kwa kazi waliyoifanya na kumpa picha ya gari lililobeba Mirungi hatua ambayo ilizua kashehe na kuwasaka wahusika wote na kuwatia mbaroni wakimwemo askari hao polisi.

Habari zilisema kuwa OCD alimkabidhi kazi Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Arusha{OC CID} kuchunguza tukio hilo na kugundua kuwa tukio hilo lilitokea na gari kuachiwa baada ya wahusika wote kuhongwa shilingi milioni 6 ila kiongozi wa kata aliyedai kamisheni kwa OCD hakushirikishwa katika mgao huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justin Masejo alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa halijamfikia ofisini kwake na kuahidi kulifuatilia na kulitolea taarifa.

’Naomba nifuatilie hilo tukio na nikilipata nitatoa taarifa hiyo na naomba uwe mtulivu maana kwa sasa kuna ugeni na nina wilaya nyingi hivyo kuwa mvumilivu’’ Alisema kamanda

....
Kama afisa kata kamfuata ocd, kumlalamikia juu ya kukosa mshiko wake, huu ni mtandao wa uhalifu na rushwa, si ajabu ocd ana mchezo huo huo ila kawachoma baada ya yeye pia kuzungukwa.
 
Hivi aliyechomoa betri nae si alikuwa miongoni mwao? Sheria haimfungi kama kajikamatisha maana nae ni muhusika?
 
Askari Polisi Wawili wa Wilaya ya Arusha akiwemo Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi{Police Post} cha Engutoto Inspekta Msaidizi{ Mrakibu Msaidizi},Alphonce Kashuku wanashikiliwa na jeshi hilo katika kituo kikuu cha polisi Arusha kwa tuhuma za kupokea rushwa ya milioni 6 na kuachia gari aina ya fuso lililokuwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zilisema kuwa mbali ya Inspekta Kashuku mwingine ambaye anashikiliwa ni konstebo James Kinyala ambaye ni askari wa upelelezi kituo Kikuu ya Arusha.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa tukio hilo lilitokea novemba 17 mwaka huu majira ya mchana katika kata ya Engutoto baada ya askari Mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupata taarifa juu ya gari hilo ambalo namba zake bado hazijapatikana kuwa gari Hilo Limebeba mzigo huo wa dawa za kulevya wenye thamani ya mamilioni ya pesa.

Habari zilisema kuwa baada ya askari mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupewa taarifa hizo kutoka kwa raia wema, walikwenda kumpa taarifa Mkuu wa kituo cha Polisi Engutoto Inspekta Kashuku na gari hilo lilikamatwa na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi.

Vyanzo hivyo vilisema kuwa taratibu zote zilifanyika katika kituo cha polisi Engutoto ikiwemo kulipekua gari hilo na wahusika kukiri kusafirisha mzigo huo na kuwekwa rumande.

Habari zilisema watuhumiwa walifanya kila namna taarifa hizo kutofika kituo kikuu cha polisi Arusha na kumshawishi Mkuu wa Kituo cha Engutoto Inspekta Kashuku kuchukua kiasi cha shilingi milioni 6 ili waweze kuachiwa na kuondoka na gari hilo na hatua hiyo waliweza kufanikiwa na watuhumiwa hao kutoweka na gari baada ya kutoa kiasi hicho cha fedha.

Vyanzo vya habari vilisema kuwa kiongozi mmoja wa serikali ngazi ya kata hakushirikishwa katika kupata mgao wa shilingi 200,000 walizopata wenzake na bila kujua alitoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha{OCD} kuomba kamishine kwa kazi waliyoifanya na kumpa picha ya gari lililobeba Mirungi hatua ambayo ilizua kashehe na kuwasaka wahusika wote na kuwatia mbaroni wakimwemo askari hao polisi.

Habari zilisema kuwa OCD alimkabidhi kazi Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Arusha{OC CID} kuchunguza tukio hilo na kugundua kuwa tukio hilo lilitokea na gari kuachiwa baada ya wahusika wote kuhongwa shilingi milioni 6 ila kiongozi wa kata aliyedai kamisheni kwa OCD hakushirikishwa katika mgao huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justin Masejo alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa halijamfikia ofisini kwake na kuahidi kulifuatilia na kulitolea taarifa.

’Naomba nifuatilie hilo tukio na nikilipata nitatoa taarifa hiyo na naomba uwe mtulivu maana kwa sasa kuna ugeni na nina wilaya nyingi hivyo kuwa mvumilivu’’ Alisema kamanda

....
PGO inafanya kazi
 
PGO noma sema mtendaji nae kawatibulia ingawa alikuwa na nia ya kufaidika lakini imekula kwao atabaki kuwa shahidi
 
Back
Top Bottom