Arusha: Polisi akiwemo mkuu wa kituo mbaroni Kwa Rushwa ya millioni 6

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Askari Polisi Wawili wa Wilaya ya Arusha akiwemo Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi{Police Post} cha Engutoto Inspekta Msaidizi{ Mrakibu Msaidizi},Alphonce Kashuku wanashikiliwa na jeshi hilo katika kituo kikuu cha polisi Arusha kwa tuhuma za kupokea rushwa ya milioni 6 na kuachia gari aina ya fuso lililokuwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zilisema kuwa mbali ya Inspekta Kashuku mwingine ambaye anashikiliwa ni konstebo James Kinyala ambaye ni askari wa upelelezi kituo Kikuu ya Arusha.


Vyanzo vya habari vilisema kuwa tukio hilo lilitokea novemba 17 mwaka huu majira ya mchana katika kata ya Engutoto baada ya askari Mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupata taarifa juu ya gari hilo ambalo namba zake bado hazijapatikana kuwa gari Hilo Limebeba mzigo huo wa dawa za kulevya wenye thamani ya mamilioni ya pesa.


Habari zilisema kuwa baada ya askari mgambo na viongozi wa mtaa na kata kupewa taarifa hizo kutoka kwa raia wema, walikwenda kumpa taarifa Mkuu wa kituo cha Polisi Engutoto Inspekta Kashuku na gari hilo lilikamatwa na kufikishwa katika kituo hicho cha polisi.


Vyanzo hivyo vilisema kuwa taratibu zote zilifanyika katika kituo cha polisi Engutoto ikiwemo kulipekua gari hilo na wahusika kukiri kusafirisha mzigo huo na kuwekwa rumande.


Habari zilisema watuhumiwa walifanya kila namna taarifa hizo kutofika kituo kikuu cha polisi Arusha na kumshawishi Mkuu wa Kituo cha Engutoto Inspekta Kashuku kuchukua kiasi cha shilingi milioni 6 ili waweze kuachiwa na kuondoka na gari hilo na hatua hiyo waliweza kufanikiwa na watuhumiwa hao kutoweka na gari baada ya kutoa kiasi hicho cha fedha.


Vyanzo vya habari vilisema kuwa kiongozi mmoja wa serikali ngazi ya kata hakushirikishwa katika kupata mgao wa shilingi 200,000 walizopata wenzake na bila kujua alitoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha{OCD} kuomba kamishine kwa kazi waliyoifanya na kumpa picha ya gari lililobeba Mirungi hatua ambayo ilizua kashehe na kuwasaka wahusika wote na kuwatia mbaroni wakimwemo askari hao polisi.


Habari zilisema kuwa OCD alimkabidhi kazi Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Arusha{OC CID} kuchunguza tukio hilo na kugundua kuwa tukio hilo lilitokea na gari kuachiwa baada ya wahusika wote kuhongwa shilingi milioni 6 ila kiongozi wa kata aliyedai kamisheni kwa OCD hakushirikishwa katika mgao huo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justin Masejo alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema kuwa halijamfikia ofisini kwake na kuahidi kulifuatilia na kulitolea taarifa.


’Naomba nifuatilie hilo tukio na nikilipata nitatoa taarifa hiyo na naomba uwe mtulivu maana kwa sasa kuna ugeni na nina wilaya nyingi hivyo kuwa mvumilivu’’ Alisema kamanda

....
 
Hii kweli ya kufungia mwaka 2021!!
Daa! Ama kweli duniani kuna mambo!
Kama Comredi angefufuka na stori ya kwanza masikioni ingekuwa ndio hii, paaaap! tuu!..... papo hapo angekufa tena kwa pressure!
 
RPC Justin Masejo kasema wampe muda wa kutosha kulifuatilia kwa sababu "nina wilaya nyingi na kuna ugeni" ( Rais Samia )

aisee huku dunia ya tatu Public sector workforce is a bad joke....

kazi za serikali na huduma kwa wananchi zina sieze kwa sababu kuna ziara ya kiongozi na RPC ana wilaya nyingi, kwa hiyo IGP nae atasema ana mikoa mingi, Waziri nae ana idara nyingi, katibu kata nae ana vitongoji vingi na Rais nae ana wizara nyingi!

Police Superintendent wa mkoa/jimbo wa dunia ya kwanza there is no way in hell akakutamkia "hiyo kazi yako inabidi isubiri sana kwa sababu nina vitongoji vingi"! Kwani hukujua job description yako kabla ya kupokea appointment? Aisee leo nimeelewa kwa nini ukienda Ulaya Police Sheriff anagombea cheo, na Jaji pia anagombea, mwanasheria mkuu anagombea, kila mtu anagombea... Ukigombea huwezi kutoa majibu ya jeuri kama haya ya nina wilaya nyingi sana.

Mhamishieni RPC Masejo kwenye mkoa wenye wilaya chache basi...
 
RPC Justin Masejo kasema wampe muda wa kutosha kulifuatilia kwa sababu "nina wilaya nyingi na kuna ugeni" ( Rais Samia )

aisee huku dunia ya tatu Public sector workforce is a bad joke....

kazi za serikali na huduma kwa wananchi zina sieze kwa sababu kuna ziara ya kiongozi na RPC ana wilaya nyingi, kwa hiyo IGP nae atasema ana mikoa mingi, Waziri nae ana idara nyingi, katibu kata nae ana vitongoji vingi na Rais nae ana wizara nyingi!

Police Superintendent wa state au county ya dunia ya kwanza there is no way in hell akakutamkia "hiyo kazi yako inabidi isubiri sana kwa sababu nina vitongoji vingi"! Kwani hukujua job description yako kabla ya kupokea appointment? Aisee leo nimeelewa kwa nini ukienda Ulaya Police Sheriff anagombea cheo, na Jaji pia anagombea, mwanasheria mkuu anagombea, kila mtu anagombea... Ukigombea huwezi kutoa majibu ya jeuri kama haya ya nina wilaya nyingi sana.

Mhamishieni RPC Masejo kwenye mkoa wenye wilaya chache basi...
Mkuu mwenyewe anawaomba kutenda haki!!!, Unategemea Nini?.
 
naona walichukua ya kubrashia viatu pamoja na ya kununua vingine vipya. Au nasema uwongo ndugu zangu Ayaaaaaaa
 
Watanzania mna roho mbaya Sana. Yani mnawaombea watanzania wenzenu wanyongwe kwa sababu tu ya mirungi? Hamjui hao ni waume, baba, kaka na shemeji za wengine? Mnapenda kushabikia shabikia mambo ya kufa kufa tu badala ya maendeleo.
Naongelea hao polisi waliopokea rushwa, sio watu waliokuwa na mirungi
 
Back
Top Bottom