Arusha - Nalaani vikali kauli zilizotolewa na viongozi wa CUF

Naendelea Kulaani vikali kauli zilizotolewa na Viongozi wa CUF kwanyakati tofauti kwenye mkutano wao wa ndani.......... . sorry mkutano wao wa wazizi hivi majuzi hapa Arusha eti Vijana na nguvu kazi ya Arusha inatumiwa vibaya na wanasiasa na eti tunaongwa Viroba ya pombe ili tufanye fujo! kwakweli kauli hizi zimejeruhi nafsi yangu na vijana wapenda mabadiliko wa Arusha kwa sababu

1) Vijana wa Arusha hatuja wahi kufanya fujo yeyote ya kisiasa zaidi ya kuunganisha sauti zetu na kukataa dhuluma na ufisadi
unaofanywa na chama Tawala kwa wananchi wa Tanzania

2) Pili hatuja wahi kuongwa viroba na kiongozi yeyote yule wakisiasa ili tukafanye fujo na wala hatupo tayari kuhongwa viroba ili
tufanye fujo yeyote.

3) Tatu hakuna kijana yeyote mkoani Arusha anatumika au kutumiwa kisiasa Vijana wa Arusha tunajielewa na tunataka ukombozi wa kweli wa kifikra, uhuru,na uchumi.

4) Nne harakati za kutafuta ukombozi hapa Arusha si kazi ya vijana peke yake, kuna Wazee, Umri wa kati, Vijana na watoto. baada ya kutabanaisha haya Natoa Rai kwa uongozi wa CUF popote pale walipo: Kwana wafute kauli na matamshi yao waliyo yatoa
hadharani Pili uongozi wa CUF uwaombe radhi Vijana wa Arusha na wapenda maendeleo kwa ujumla kwa kudhalilishwa na kwa
nafsi zao zilizo jeruliwa kwa kauli hizo.

Nawasilisha.
hayo maneno ya uswahilini yasikutishe mkuu arusha sio bububu hawatfanya chochote chugga watu wamesha komaa
 
Aim sorry to say this but vijana wa arusha wanatumika vibaya na wanasiasa .. maneno ya cuf Yamaha ukweli ndani yake

Je CUF wanawatumiaje vizuri vijana ambao wengine huwatumia vibaya?!!!! TAFAKARI. Ni kwa kuwapa TENDE na HALUA???
 
Kusema kweli nilicikiliza kauli za Viongozi wa CUF nikaona hazina tofauti na za CCM.. Ila wakae wakijua wananchi wanajua jinci ya kudai haki zao ciku hizi.. Mwisho wa kutumika itakuwa ni aibu kwao..
 
Aim sorry to say this but vijana wa arusha wanatumika vibaya na wanasiasa .. maneno ya cuf Yamaha ukweli ndani yake

Ina maana ukiikataa CCM ni kutumika vibaya na wanasiasa? Achane siasa za kipuuzi zisizojenga nchi na kuwajenga ninyi wenyewe, angalieni matatizo yenu na mjipange upya.
 
Usikasirike ila ni kuvumiliana tu kwa siasa zetu za kitanzania.Ukisema CUF wameongea maneno mabaya kwa CHADEMA na CUF wanasema CHADEMA wanaongea vibaya kuhusu CUF huku na CCM na wao ndio hivohivo kama mchezo wa mduara ni kuzunguka tu mpaka uchoke mwenyewe ukae chini.Kiufupi bado hatujakomaa kisiasa ila tunachojua ni mafumbo mpaka sasa na kutumia nguvu na fujo zisizo na maana.Bado hatupo tayari ku-challenge sera ambazo ndio muhimu zaidi kuliko mayowe na fujo kwa kutumia matusi,mawe na hata cha moto kama polisi wetu.Labda tuelimishane zaidi nini maana ya kufuata chama kwasababu wengine kufuata chama ni kama mkumbo zaidi na sio kuangalia sera zinazotumika ndani ya chama na malengo yao ni nini.Kwa hiyo mimi hapa naona ngoma droo kwa vyama vyote.
 
Kwahiyo hapa unamaanisha yale mauwaji ya Janualy 2001 na moja kule Zanzibar CUF na hasa huyu Maalim Seif alikuwa anawatumia Wapemba kufanikisha Political Agenda na sasa amefanikiwa anakula mpaka amevimbiwa ndio anakuja na style ya nyani halioni kundule?

Hivi kuwasafirisha vijana kutoka Buguruni mpaka Arusha huku kama siyo kuwatumia tuwaitaje? CUF wanapaswa kuwaomba radhi vijana wa Arusha otherwise sintoshangaa next time nikisikia wamechezea mkong'oto kama alivyofanywa Mtikila kule Tarime.

Agggrrrr! Multiple ID's at work.
 
Kwa hiyo hizo ndo sera za CUF huko Arusha? Nilitegemea CUF wanene kwa mapana watawafanyia nini wana wa Arusha iwapo watachukua nchi. Mbona hizo sera zimekaa kinafiki
 
Na huo ndiyo ukweli, nawaunga mkono CUF kwa kusema ukweli, mnatumiwa vibaya na wanasiasa mnasahau haki na wajibu wenu kuendeleza nchi

Hao waliosafirishwa kwa malori na mabasi kutoka sehemu mbalimbali wanatumika vizuri, leo wakipata ajali kama iliyotokea ya dar express nani atawalipa.Prof.kwishne hana jipya ndiyo maana alishindwa kumshauri mzee mwinyi uchumi ukawa mikononi mwa walanguzi.Cuf wamechemsha sana wao wamesafirisha watu wakaacha kazi zao za kiuchumi kisa siasa za ngunguri pumbafu zao
 
Alichosema prof Lipumba Arusha kipo claer, wewe ndo hujaelewa , na wala wewe huna mamlaka ya kuwakilisha vijana wote wa Arusha. Vijana wa Arusha wana akili na baadhi yao wanamuunga mkono, ila wewe ndo unajifanya chizi mwenyewe.

kama Maalim alivyosema " mtanuna na mpasuke kabisa, lakini CUF Arusha ndo tumeingia rasmi"
 
Hakika Cuf ni wakusamehe na washangaa kwa nini wanapambana na cdm!

Mimi nilidhani ni peke yangu ndio nina swali hilo ! Nadhani CUF wanataka kwenda Ikulu, aliyeko Ikulu ambaye wanatakiwa kumg'oa ni CCM, lakini nguvu zao kubwa, mashambulizi yao makubwa ni kwa CDM. Sasa huko Ikulu wataendaje ? kwa kuing'oa CDM, TLP, NCCR, au mimi sielewi ? wanatakiwa kuishambulia CCM ! Siasa za hapa nyumbani ... sijui ni umaskini ?
 
Ndugu yangu Mwitaz,
Kwanza kabisa ningependa nikupe pole kwa kuumizwa na kauli za viongozi wa CUF. Mimi pia ni mkazi wa Arusha ila sikuumizwa na kauli walizozitoa kwa sababu kubwa mbili:

1. Wametumwa na kugharamiwa na ccm ili kujaribu kudanganya wananchi wa Arusha kuwa CHADEMA ni chama cha
vurugu na wao bila kutafakari wameingia kichwa kichwa. Lengo lao lilikuwa ni kuaminisha wajinga wenzao kuwa
wananchi wanaopinga udhalimu wa mume wao (chama cha mauaji) huhongwa pombe. Wanafikra kuwa bado watu wa
Arusha ni wajinga wasiotambua haki zao na kusahau kuwa ccm haikuwahi kushinda uchaguzi wa ubunge toka mfumo
wa vyama vingi ulipoanzishwa TZ (1995 alishinda Makongoro Nyerere akiwa TLP lakini baada ya miaka miwili alitolewa
kihuni kama walivyofanya kwa Lema na hakukata rufaa. 2005 Lema alishinda kwa tiketi ya TLP akafanyiwa tena uhuni mwenyekiti
wake Mrema akahongwa akakataa kugharamia rufaa hivyo kuipa ccm jimbo)

2. Wametoa kauli za kipumbavu kutokana na hasira. Wao wamegharamia mamia ya watu kutoka mikoa mingine waje
kujaza mikutano yao ili wavute umati mwingine wa watu kutoka Arusha lakini haikuwezekana kwani walibaki tu na watu
waliokuja nao pamoja na magari yao. Mtu yeyote anayefikiri vizuri angetarajia hasira kwani lengo lao halikutimia na pia
wakaanza kutoa kauli kuwa wamepigwa mawe na wafuasi wa CHADEMA ili kukipaka matope lakini haikusaidia.

Ningependa kukushauri kuwa adhabu nzuri kwa mjinga siku zote ni kumpuuza tu, hivyo hao Mrs. ccm wanastahili kupuuzwa tu kwani ndio adhabu inayowastahili. Sikuumizwa na kauli zao kwani nimewapuuuza tu kama wajinga wengine.
 
Waambie vijana wa arusha wana makazi na majumba yao,hawakai vibarazani kwa wazazi kama temeke na zenji.
 
Hakuna chama ambacho hakiwatumii vijana kwenye mambo yake ya siasa tutadanganyana hapa, mfano ccm wanawatumi uvcc, cdm wanawatumia Bavicha na cuf wanawatumia watu kama UAMSHO na wengineo! Wanasiasa bwana ni vigeugeu!
 
Watu wa ars acheni propaganda ccm ndio baba aw nchii fanyeni kazi hizi Siasa za kudanganywa mnauwawa alafu wengine mkono unaenda kinywani pole sana . Sisi life goes on and life is good!
 
Waambie vijana wa arusha wana makazi na majumba yao,hawakai vibarazani kwa wazazi kama temeke na zenji.

s-t-u-p-i-d, kama ban wacha ije. Ukiendelea kuisakama Zbar n..t...a...k...u....t....u....k...a.....n...a..... Mungu atakuua kwa dhambi yako ya ubaguzi iliyojengeka moyoni mwako. UMEONA WAPI WA-ZBAR WANAKAA TU VIBARAZANI. Hv hawana kazi ya kufanya wao? Lakn kwa nini watu na elimu zenu muendelee kutoa kauli zenu za dharau kwa baadhi ya watu wanaotoka maeneo.
 
Hahahaaaa! Mtatiro UONGOZI WA UDSM ulimshinda itakuwa NCHI????? CUF bwana, badoooo sanaaaa!
 
mwitaz! usiwasemee vijana wote wa Arusha, kwa sisi tuliopo hapa mjini tunaona mengi.sema hakutakiwa hatujumuishe vijana wote!
 
Back
Top Bottom